Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kustaafu siasa pamoja na utumishi wa umma.

Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa leo, Dkt. Nchimbi amesema amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kumjulisha uamuzi wake wa kuachia nafasi hiyo.

Amesema uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 50(2)(c) ikisomwa pamoja na Ibara ya 149(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kujiuzulu kwake kutaanza rasmi Septemba 4, 2026.

Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa wakati alipomuahidi Rais Samia mwaka 2025 kuwa atamsaidia katika kutekeleza majukumu yake kwa uwezo na uaminifu wake wote, pia aliahidi kuwa angeachia nafasi hiyo siku ambayo Rais angeona anahitaji Makamu mwingine.

Amesema amefanya uamuzi huo pasipo shaka baada ya kubaini kuwa Rais anatarajia mabadiliko.

View attachment 3656524
Tuko papaya sana....yaani ni papaya kuliko watu wanavyofikiria.
 
Ni maamuzi yake hata kikao na Kikwete aliitwa ili atulie yeye akasimamia msimamo wake wa kujiuzuru..
Lakini tetesi za mwanzo ambazo zilikuwa zinatajwa ni kwamba kulikuwa na shinikizo la kumtaka ajiuzulu.

Na shinikizo hilo lilikuja baada ya kauli zake tata. Ni kauli hizo hizo ambazo ziliwahi kumfanya aitwe Yuda pale Bungeni.

Hata yule kada wa CCM aliyetekwa na kuteswa alidai, waliomteka walimlazimisha amtukane Nchimbi.

Haya ni matukio ambayo yanasapoti hoja ya "kushinikizwa kujiuzulu" kuliko hoja ya "kujiuzulu kwa hiari"
 
Maswali ambayo najiuliza.

Ni trick ipi waliyotumia kum force Nchimbi mpaka kuachia ngazi?

Maana huko nyuma kumekuwa na tetesi za Nchimbi kulazimishwa kujiuzulu.

Je usalama wake ulitishiwa? Au pengine ameamua kukubali kwa lengo la kulinda familia yake kwasababu ni easy target?

Kwasababu hili swala ukilitafakari kuwa ni maamuzi ya hiari, hali make sense kabisa.
Kama mpishi mkuu wake wamemwondoa. Labda aligoma kumu-magoti
 
Utabiri wayule shehe kama unatimia vile.Alisema 2015 atatokea rais mwanaume mzalendo na atapendwa na watz wengi na hatamailza muda wake atarithiwa na mmama ambaye hatakuwa kipenzi cha watanganyika kwa sababu ya low performance capacity na atakimbiwa na makamu wake then na yeye atajiuzulu
 
Back
Top Bottom