Maisha yangu mabaya sana nakaribia kujiua

Maisha yangu mabaya sana nakaribia kujiua

Ni kweli kabisa.Hali yangu mie mkuu mpaka nafika hatua mbaya kabisa lakini najipa moyo nitasimama tu Mungu yupo.
Watu tunatembea tu lakini vichwa si vyetu unaweza kuta mtu anacheka lakini siri ni yake
 
Kuna wenzako wana matatizo kama hayo na hawana kipato kama chako na bado wana survive... Achana na wazo la kujiua
Kuna tiba moja rahisi sana lakini very effective.... Ni tiba maarufu na imewasaidia wengi na mfanyaji ni wewe mwenyewe
Tiba ya kuogea chumvi hasa nzuri ni ile ya mabonge... Hicho tu.. Ogea mara mbili kwa siku kwa mwezi mzima huku kila ukiogea unanuizia mabaya yakuondoke na uwe na ladha kama chumvi
Mafuta yako yawe ya mzeituni... Jaribu hiyo hutojuta na haina side effects wala gharama za kazi
Mkuu Mshana, kwa muda wangu wa ziada ningependa nijifunze hiyo taaluma toka kwako, tafadhali.
 
Pole sana.kuna wengine wana matatizo zaidi kuliko wewe.punguza misaada. Jiwekee malengo. Hiyo hiyo laki mbili ipunguzie matumizi .kama unaweza biashara fikiria unachoweza ili ufanye na huku una kazi yako.nina rafiki yangu mshahara wake ni chini ya huo ila yeye ni mpishi Wa keki ilimchukua miaka 8 kuweza kujenga kisehemu kununua vifaa na kuajiri mtu Wa biashara hiyo ya keki.maana alidunduliza miaka yote. Usiwe na haraka ukajihisi umechelewa.
Mkuu umeona ameandika mshahara wake laki mbili umesoma vizuri sio milioni 2 hiyo Bos?
 
Duuuh! Wewe kuogea maji ya chumvi na mzeituni kuondoa mikosi unaona sio ushirikina? Ina maana yana supernatural power ya kuondoa hiyo mikosi, ila yote kwa yote, nimejaribu kutoa ushauri tu nikiamini kila kitu kina mwanzo, Leo utaogea maji ya chumvi, kesho utaambiwa uvae chupi nyekundu, keshokutwa uchinje mbuzi mweupe na mwisho utavaa tunguri
Acha kukariri umagharibi wewe hizo ni mila na desturi za mwafrika
 
Pole sana.kuna wengine wana matatizo zaidi kuliko wewe.punguza misaada. Jiwekee malengo. Hiyo hiyo laki mbili ipunguzie matumizi .kama unaweza biashara fikiria unachoweza ili ufanye na huku una kazi yako.nina rafiki yangu mshahara wake ni chini ya huo ila yeye ni mpishi Wa keki ilimchukua miaka 8 kuweza kujenga kisehemu kununua vifaa na kuajiri mtu Wa biashara hiyo ya keki.maana alidunduliza miaka yote. Usiwe na haraka ukajihisi umechelewa.
Laki mbili au milion mbili ?
 
Ndugu zangu,

Kama nilivoandika kichwa cha habari mimi ni kijana niliye ajiriwa na mapato yangu kwa mwezi nikama 2000000 hivi.

Lakini nimekosa furaha kiasi kwamba sina furaha na maisha pamoja na watu wanaonizunguka hata hiyo pesa yote huishia kumaliza matatizo ya ndugu na kila mwanamke naingia naye kwenye mahusiano basi hata anza kuumwa kiasi pesa yote inaenda kumhudumia mgonjwa.

Sasa najiuliza nitakuwa nimerogwa au na kipindi hiki ndo nimekosa kabisa ujasiri wa maisha sasa je hiyo hali ya kawaida au kuna michezo ya kiswahili nafanyiwa na kama yupo mganga anitibie nikipona ndo namlipa maana nimeenda kwa hawa wa upako naona maigizo kabisa mtu ananiombea sijazimia ananilazimisha kuniangusha na wale wasaidizi wanashika kwa nguvu kama nina matatizo wakati nipo vizuri, ndo nikaona wote hawa maigizo.

Nimeenda kama kwa wa upako wa nne hivi wote hivohivo.

Sijui nifanye nini.
Nilichogundua watanzania tunapenda kulala mika sana kuliko kufuatilia, ukifuatilia id yako unapata tena kwa haraka tu ukikaa nyumbani utakaa sana id zinapatikana kwa muda mfupi tu na katka utaratibu unaokubalika duniani huwez pata passport bila kuwa na id, huo ndio utaratibu dunia nzima, nikwambie passport ya Tanzania ni nzuri sana wageni wengi wameibeba kujifanya watz mwisho wao umefika kwenye id, maana kule utajulikana asiki yako ni wapi, wengi wanafanya uhalifu wakijifanya watz namshukuru rais sana anakomesha hili, tafuta id ndugu ndio utaratibu mahali popote pale sio agizo toka juu ni utaratibu unaokubalika na inapataikana wala haichukui muda...ila ukikaa chini utalalamika sana.
Mtafute pastor katunzi..si wa upako kanisa liko mbagala stand ya shamba juu inapita reli eagt city center hapoo utapona tu.
 
Ndugu yangu nimebadili nyumba za kupanga nikifikiri labda zina madudu yaani Nina ajira lakini bado nakosa furaha na cjui ni marafiki nilionao nikanunua usafiri lakini cku nimepaki nyumbani nikakuta kitu cha ajabu bonet ya mbele imefunguliwa mtu kachomoa oil stick tu kisha kaweka juu ya injini aikupita cku tatu nilipata ajali mbaya lakini nikapona ucku naota mambo ya ajabu naona sura lakini czfahamu nimeshakutana nazo wapi na ndoto moja inaweza kuja kujirudia mwezi mmoja baadae alafu isitoshe maisha ya utotoni niliteseka sana na uchawi sumbawanga ikiwemo kujikuta nimelala nje wakati nilikuwa ndani isije kuwa bado na andamwa maana kuna vifo vilitokea kwenye familia ni vyakutatanisha koo yangu inaendekeza ushirikina sana hata ndugu upande wa baba hawashikamani mpaka utokee msiba hapo patakuwa na majungu na ugomvi yaani kifupi naichukia family tree yangu inanifanya nisi ishi maisha yangu halisi ya upendo na amani
Mkuu mm nimekuelewa na mwili umesisimka.
Ujue wabongo unafiki tume weka mbele, lakini ushirikina upo kaka. Usilale na wewe pambana ila cha msingi sali sana kwa imani yako unayo amini.
Ila hayo mambo yapo kaka pole sana sana.
 
Usimlaumu mtu yoyote unapomuona yupo katika mtihani, iyo mil 2 sio ishu. Muhimu ni nafsi je vipi itakuwa salama.

Humu nawaona wamo weng wanaishangaa mil 2 eti pesa nyingi. Kama wewe ukipewa mtihan kama wake pengine hata ungelipwa mil10 ndio ungejutia zaid. Kila kitu mnakiwaza kiurahs tu

Haitakiwi kuiwaza 2 mil yake unatakiwa umsaidie vip atoke hapo alipo kwa shetani.
Inasikitisha sana kuona Taifa hili bado kuna viumbe wenye akili na mawazo kama yako. Mungu awaepushe na adhabu za kabri.
 
Ni kweli ndugu?

Kuna ndugu yangu ana matatizo sijui niite nuksi kama yy mwenyewe anavoelezea! Inaweza kumsaidia hii?
Ni kweli nafikiri umeona shuhuda za watu fanya ajaribu utaona matokeo yake
 
Ndg kwa maelezo haya ni kuwa tatizo lako ni la kisaikolojia na kiroho.

Maelezo yako kwenye mada pia inaonyesha bado hujamwamini Mungu na nguvu zake na bado unaamini mizimu na uchawi.

Ukweli ni kuwa unahitaji msaada wa Mungu ili ukutoe hapo ulipofikia.

Anza kwa kufanya yafuatayo.

1. Tubu dhambi zako zote kwa matendo ya kishirikiana uliyoshiriki kwa kujua au kutokujua.

Pili anza kumuamini Mungu kwa Yesu kristo na msaada wake.

Tatu chukua hatua huku ukiwa umekusudia kusaidiwa na Mungu muone mtu wa mungu ambaye ana good reputation ktk mazingira yako. Si lazima awe Celebrity preacher.

Nne tambua uponyaji ni mchakato, hivyo kuwa mvumilivu.kama ulivyoshiriki ushirikina kwa muda mrefu....itachukua muda mpaka uwe free...kabisa kwani uponyaji wako pia lazima uende kwenye fahamu yako na mfumo wa kiimani. Jambo j
Hili uchukua muda

My guarantee...Mungu lazima atakusaidia. Lakini anza kumuamini.

Katu usifuate njia za kishirikina. Utakufa dhambini
Nashukuru nitajitahidi kushinda kanisani huwa nafarijika sana nikiwa kanisani maana moyo wangu una hofu nakosa hata ujasiri wa kufanya maendeleo nikiamini nakufa muda wowote kichwa kina uma muda wote na sipati usingizi was maana cjui ni nn hiki
 
Ndiyo maana wahenga wanasema ukiwa na tatizo usijifungie ndani. Utadhani wewe ndiyo mwenye shida pekee lakini ukitoka na kuzungumza na watu wenye shida utajiona kumbe wewe ni kama uko peponi.
Nilitafuta sehemu zile watu wenye matatizo wanakutana na kuzungumza cjui wanaita rehab hapa. Nchini hamna maana ningeshea matatizo na wengine ningetambua nasumbuliwa na nn
 
Back
Top Bottom