Maisha yangu mabaya sana nakaribia kujiua

Maisha yangu mabaya sana nakaribia kujiua

Alien pilot

Senior Member
Joined
Dec 29, 2017
Posts
194
Reaction score
225
Ndugu zangu,

Kama nilivoandika kichwa cha habari mimi ni kijana niliye ajiriwa na mapato yangu kwa mwezi nikama 2,000,000 hivi.

Lakini nimekosa furaha kiasi kwamba sina furaha na maisha pamoja na watu wanaonizunguka hata hiyo pesa yote huishia kumaliza matatizo ya ndugu na kila mwanamke naingia naye kwenye mahusiano basi hata anza kuumwa kiasi pesa yote inaenda kumhudumia mgonjwa.

Sasa najiuliza nitakuwa nimerogwa au na kipindi hiki ndo nimekosa kabisa ujasiri wa maisha sasa je hiyo hali ya kawaida au kuna michezo ya kiswahili nafanyiwa na kama yupo mganga anitibie nikipona ndo namlipa maana nimeenda kwa hawa wa upako naona maigizo kabisa mtu ananiombea sijazimia ananilazimisha kuniangusha na wale wasaidizi wanashika kwa nguvu kama nina matatizo wakati nipo vizuri, ndo nikaona wote hawa maigizo.

Nimeenda kama kwa wa upako wa nne hivi wote hivohivo.

Sijui nifanye nini.
 
Pole sana.kuna wengine wana matatizo zaidi kuliko wewe.punguza misaada. Jiwekee malengo. Hiyo hiyo laki mbili ipunguzie matumizi .kama unaweza biashara fikiria unachoweza ili ufanye na huku una kazi yako.nina rafiki yangu mshahara wake ni chini ya huo ila yeye ni mpishi Wa keki ilimchukua miaka 8 kuweza kujenga kisehemu kununua vifaa na kuajiri mtu Wa biashara hiyo ya keki.maana alidunduliza miaka yote. Usiwe na haraka ukajihisi umechelewa.
 
Ndugu zangu kama nilvoandika kichwa cha habari mm ni kijana nilye ajiriwa na mapato yangu kwa mwezi nikama 2000000hv lakini nimekosa furaha kiasi kwamba cna furaha na maisha pamoja na watu wanao nizunguka hata hiyo pesa yote huishia kumaliza matatizo ya ndugu na kila mwanamke naingia naye kwenye mahusiano basi hata anza Ku umwa kiasi pesa yote inaenda kumhudumia Mgonjwa sasa najiuliza nitakuwa nimerogwa au na kipindi hiki ndo nimekosa jabisa ujasiri wa maisha sasa je hiyo hali ya kawaida au kuna michezo ya kiswahili nafanyiwa na kama yupo mganga anitibie nikipona ndo namlipa maana nimeenda kwa hawa wa upako naona maigizo kabisa MTU ananiombea sijazimia ananilazimisha kuniangusha na wale wasaidizi wanashika kwa nguvu kama Nina matatizo wakati nipo vizuri c ndo nikaona wote hawa maigizo nimeenda kama kwa wa upako wa nne hv wote hvohvo cjui nifanye nn
Kuna wenzako wana matatizo kama hayo na hawana kipato kama chako na bado wana survive... Achana na wazo la kujiua
Kuna tiba moja rahisi sana lakini very effective.... Ni tiba maarufu na imewasaidia wengi na mfanyaji ni wewe mwenyewe
Tiba ya kuogea chumvi hasa nzuri ni ile ya mabonge... Hicho tu.. Ogea mara mbili kwa siku kwa mwezi mzima huku kila ukiogea unanuizia mabaya yakuondoke na uwe na ladha kama chumvi
Mafuta yako yawe ya mzeituni... Jaribu hiyo hutojuta na haina side effects wala gharama za kazi
 
Mkuu siku unapojiua basi kama ni chumbani usifunge mlango au jiulie peupe ili watu wasihangaike kutafuta mwili wako na pia andika sababu ya kujiua kabisa ili watu wasianze kutafutana uchawi.....

Tatizo lako unawaza kishirikina ndo maana unasumbuka hivyo..hujarogwa wala nii ni wewe umwjaza ujinga kichani mwako, kuhusu swala la kuwahudumia ndugu jaribu kuwa mkatili tu ukizidi kuendekeza unakufa maskini.
 
Ndugu yangu nimebadili nyumba za kupanga nikifikiri labda zina madudu yaani Nina ajira lakini bado nakosa furaha na cjui ni marafiki nilionao nikanunua usafiri lakini cku nimepaki nyumbani nikakuta kitu cha ajabu bonet ya mbele imefunguliwa mtu kachomoa oil stick tu kisha kaweka juu ya injini aikupita cku tatu nilipata ajali mbaya lakini nikapona ucku naota mambo ya ajabu naona sura lakini czfahamu nimeshakutana nazo wapi na ndoto moja inaweza kuja kujirudia mwezi mmoja baadae alafu isitoshe maisha ya utotoni niliteseka sana na uchawi sumbawanga ikiwemo kujikuta nimelala nje wakati nilikuwa ndani isije kuwa bado na andamwa maana kuna vifo vilitokea kwenye familia ni vyakutatanisha koo yangu inaendekeza ushirikina sana hata ndugu upande wa baba hawashikamani mpaka utokee msiba hapo patakuwa na majungu na ugomvi yaani kifupi naichukia family tree yangu inanifanya nisi ishi maisha yangu halisi ya upendo na amani
 
Tumia tiba ya chumvi kila kitu kitakwisha
 
Wacha niache neno....hiyo ela mbona kubwa mi nipo kazini napokea chini ya hapo Na napoishi mpaka kazini nauli haipungui elfu 4500 ukijinyima Sana 3000 hakuna nimepanga Na makorokocho kibao kwa ela hiyo hiyo,lakini bado tuna survive,ngojea kidogo kwanza........
 
Ebu acha kuwa na roho ya kike ya uoga uoga ww, uoga ndio unakusumbua hakuna kingine, kuwa na roho ngumu ngumuuuu sana kunizidi mm, hayo mawazo ya kiuoga uoga na hofu za kipuuzi zitakimbia na kukuacha, kuwa na roho ngumu kunizidi mm nimekwambia, acha ujinga mtoto wa kiume unalegea legea, ningekuwa nakujua ningekuwasha vibao vikali kali kabisa ukomae uwe mwanaume mgumu, simama very strong acha ujinga na uoga kuwa na roho ya chuma cha pua na mkono nyundo kama mm, narudia acha kulegea legea mtoto wa kiume, kuzaliwa mwanaume ni kuwa mgumu sana, akili kubwa & smart na katili ikibidi kuliko shetani then maisha yanakuwa bora kabisa.. Uoga ni ugonjwa mbaya sana, Be very strong
 
Pole sana.kuna wengine wana matatizo zaidi kuliko wewe.punguza misaada. Jiwekee malengo. Hiyo hiyo laki mbili ipunguzie matumizi .kama unaweza biashara fikiria unachoweza ili ufanye na huku una kazi yako.nina rafiki yangu mshahara wake ni chini ya huo ila yeye ni mpishi Wa keki ilimchukua miaka 8 kuweza kujenga kisehemu kununua vifaa na kuajiri mtu Wa biashara hiyo ya keki.maana alidunduliza miaka yote. Usiwe na haraka ukajihisi umechelewa.
Nahisi ni milioni mbili hebu soma zile zero vizuri
 
Achana kwanza na hao wa upako ,,mtafute sheikh akusaidie kukuingiza katika dini ya haki na kweli ( uislam) uitamke shahada na uingie katika dini kwa imani yakini baada ya hapo upate visomo mujarabu. Kwa uwezo wa mwenyez Mungu insha Allah hayo matatizo yako yatafika mwisho. Fikiri sana juu ya comment hii ndugu yangu.
 
Umetaja kiwango cha pesa na kusema kinaisha haraka, kwa hapa nikadhani unaona pesa yako haikufaidii wewe.

Na nafikiri hii ndiyo big deal hapa.

Ruge (lecturer siyo wa Clouds) alisema uchawi ni coincidence na bahati, yaweza kua ni bahati mbaya au nzuri.
Mfano, umekuta boneti liko wazi oil stick imechomolewa siku kadhaa mbele ukapata ajali yaani hapo ni tukio limekutana na bahati mbaya ukapata ajali ambayo ulivyoitrace coincidence yake ni imetokea soon baada ya kukuta oil stick juu ya boneti.

Akasema kuamini au kutoamini uchawi ni uchaguzi wako.
 
Ebu acha kuwa na roho ya kike ya uoga uoga ww, uoga ndio unakusumbua hakuna kingine, kuwa na roho ngumu ngumuuuu sana kunizidi mm, hayo mawazo ya kiuoga uoga na hofu za kipuuzi zitakimbia na kukuacha, kuwa na roho ngumu kunizidi mm nimekwambia, acha ujinga mtoto wa kiume unalegea legea, ningekuwa nakujua ningekuwasha vibao vikali kali kabisa ukomae uwe mwanaume mgumu, simama very strong acha ujinga na uoga kuwa na roho ya chuma cha pua na mkono nyundo kama mm, narudia acha kulegea legea mtoto wa kiume, kuzaliwa mwanaume ni kuwa mgumu sana, akili kubwa & smart na katili ikibidi kuliko shetani then maisha yanakuwa bora kabisa.. Be very strong
Hahahaha..aisee..hope mleta mada atagrab some points here
 
Kuna wenzako wana matatizo kama hayo na hawana kipato kama chako na bado wana survive... Achana na wazo la kujiua
Kuna tiba moja rahisi sana lakini very effective.... Ni tiba maarufu na imewasaidia wengi na mfanyaji ni wewe mwenyewe
Tiba ya kuogea chumvi hasa nzuri ni ile ya mabonge... Hicho tu.. Ogea mara mbili kwa siku kwa mwezi mzima huku kila ukiogea unanuizia mabaya yakuondoke na uwe na ladha kama chumvi
Mafuta yako yawe ya mzeituni... Jaribu hiyo hutojuta na haina side effects wala gharama za kazi
Umenikumhusha miaka 3 iliyoisha baada ya kulalamika sana ukanipa hii tiba na ikafanya kazi,,, kikubwa n kuamin na kujithamn ,,mana kutaman kufa/kujiua n roho mbaya ya shetan inamvaa
 
Back
Top Bottom