USHAURI: Ndoa inaelekea kunishinda sina namna, naumia sana

Mr_Plan

Senior Member
Oct 2, 2021
140
194
Habari Wanajamvi Leo naomba niwasilishe mkasa wangu unaonisibu hivi Sasa katika Maisha Yangu....Ndoa...Ndoa..Ndoaaa..

Baada ya kusaka Life Miaka 2 Nyuma na kujihakikishia Uwezo wa Kula kuvaa, Malazi, Starehe Nikiwa na Miaka 24 tu Nikaamua kumtafuta Mwenza wa Kujenga nae Life..

Nikampata binti Mmoja kabila Mzaramo umri miaka 20...Sikuchukua Muda sana Kumfahamu Yeye na Familia Yake Tangu Nimjue Ilichukua miezi kama 6 Tu ya kufahamiana. Mungu Akajaalia kweli kidume nikafanikisha Taratibu zote za Ndoa, nikalitwaa Jiko.

Maisha Yakaanza kwa Upendo Wote Tukapendana ilienda kama miezi mi3 baada ya Ndoa Ndipo Mabalaa Yakaanza.

Aliniomba Pesa ya kuwafanyia Birthday Wadogo zake nikimwaidi Lakini Mambo Yalibuma, Nikamtuliza kuwa Tutawafanyia Wakati Mwingine kwa Sasa mambo Yamegoma na Tumetoka kwenye harakati za Magarama ya Ndoa punde tu, kwaiyo Uchumi bado Aujakaa sawa, Aliniitikia Lakini kumbe Sivyo.

Siku ya 3 Mbele Nilishtuliwa na Jirani Kuwa Mke wangu Ameuza nguo zake kwa baadhi ya Majirani, nilishtuka Sana Sababu Kama ni pesa ya kula Nampa Tatizo Ni nini...Nilipojaribu kumuoji bado Alinificha..hadi pale Nilipoenda kufungua kabati lake na kukuta kweli Nusu ya nguo zake hazipo

Nilijawa na hasira sana...Baada ya kuendelea kutazama vizuri nikaja kuta keki na zawadi nyingin za Birthday Chini ya kabati zimefichwa kwa hasira kali bila Majadiliano Nilizivuruga Vuruga..Ndipo tifu LilipoanzA Nae aka Juu akachezea makofi....akapiga simu kwao Usiku huo huo Aiseeee skuamini familia nzima ilikuja Mamamkwe Alikuwa kama mbogo mjomba Mtu ndo usiseme.

Nilishambuliwa Sana Usiku huo Mpaka Mtaa mzima Uliamka kwa kweli ilikuwa Aibu Isiyokuwa na kifani nilijuta Sana na Nikaamuliwa Ili kesi isiwe kubwa na Isiende Polis Nilipe zile Garama kweli kidume Nikalipa na Nauli Yao Juu ndo Wakasepa...kwa Kweli kesho yake Niliamka na homa kali Sana...ila Mungu Alisaidia.

Kuanzia hapo Bibie akaanza Ujeuri Akawa anamskiliza Mamaake Kwa Kila kitu Misuko Suko..Minuno na Adha nyingine Zikaja kwa Kasi ndani. Msukumo Mkubwa Ukitoka kwa Mamaake ikafika kipindi mpaka akamwambie adai Talaka ili Nimuache Japo Yeye Alikuwa anasita.

Nikaona mambo Yanazidi kwenda Mrama ikabidi mpaka Nihame,nnapokaa nihamie karibu na kwa Mamaangu mzazi iliniweze kupata Msaada Japo kidogo.

Hiyo haikusaidia Kitu Yule Mama akazidi mshawishi mwanae adai Talaka..Naye Akajaa Upepo kweli akadai japo kishingo upande mana akitoka apo anaenda kuomba Ushauri kwa Majirani kuwa Nampenda Mume wangu na Yeye ananipenda ila Mama Ananilazimisha Tuacheni Eti IPO Siku nitamtelekeza.

Ile Hali ilienda ikawa 2much kikao kikaitishwa upande wangu na Upande wake tukakutana...na Masheikh Juu...Akaulizwa Sababu inayomfanya adai Talaka ni nini Jibu hana..Gafla Mamamkwe akadakia kuwa apewe Talaka hata kama Sababu hakuna...Nikaona ananipanda kichwani Tifu Likaanza na Kikao kikaishia hapo hapo Huku kila Mtu akimtoa Akili Mamamkwe ndo kuona kumbe Yeye ndio chanzo kila mtu akamkataaa.

Hapo Sasa Maamuzi Yakawa kwangu Nikaona Isiwe Tabu kufika nyumban chukua peni na karatasi Niandike Talaka Nashangaa Mke Anaanza Kulia kuwa Anajuta sana na Mamaake alikuwa anampotosha na Anasema alikuwa adi anamchoma Sindano kimya kimya ili asizae ivo Nimsamehe Alifunguka Mengi Sana adi Nisiyo Yajuaa...kuona simsikilizi akakimbilia kwa Bi Mkubwa wangu uku machozi ya Yakimbubujika.

Kweli baada ya Muda Nikaitwa na wakanisihi nimsamehe na nimpe nafasi Nyingine kweli nikakubali kwa Roho safi nikamsamehe mke wangu Tuendeleze ndoa Yetu kwani Nampenda Sana na bado Ndoa Yetu Changa Yapata ilikuwa kama miezi 8.

Ma Mkwe kwa hasira akamtaa mwanae kuwa asimjue na akampora kila kitu alichomtunza siku ya harusi huyo akasepa zake

Maisha Yaliendelea kwa Furaha na Amani Tele bila kuwa na Misuko suko Yoyote ile na kipindi chote icho tUkiwa mbali na Mama mkwe tena bila kuwa na Mawasiliano Yoyote.

Baada ya Miezi kupita Mamamkwe Akaanza tena Kujipenyeza kimya kimya Naye Mke Wangu Akaanza Vijitabia ambavyo Nilikuwa sivielewi akazidisha mpaka Akapitiliza..ikafika kipindi mpaka nikawa naishi na Hasira Moyoni ila nikazidi kuweka uvumilivu na kumsihi abadilike.

Ile Hali ilizidi adi ikawa kama manyanyaso kwangu..siku moja Nilimwambia aniandalie Chakula kwakweli Alichokifanya Sikutegemea kile Chakula alivyokipika ni kama cha kula mnyama na Si Binadamu.Nilijikuta Najawa na hasira na Jazba kali kufani kwangu kiasi cha kushindwa kujizuia nilimwita Alipoingia tu Ndani.

Sikumuuliza Nilimpa Kata Funua Alipoinuka Nikapiga Jeb right nikafunua Kidevu Gafla naona damu zinamiminika kwenye mdomo Nikaona huu Msara fasta nikasepa..baada ya Muda napigiwa simu mkeo kaenda Polisi..nikaona hii Sasa Jelaaaaa

Kesho Yake Nikapigiwa simu kuwa Naitajika Nilipoti polisi....Nikafikiri Nikaona kukimbia sio Dawa nimepiga moyo konde adi kituoni kweli kufika wakanipa Maelekezo Yaliyoandikishwa na mke wang pamoja na Mama Mkwe wangu.

Nilishangaa Sana Ma Mkwe Wangu kafikaje tena Huku na Mengi Yaliandikwa Yalikuwa ya Uongo Asilimia 100 na kubwa zaidi Mama Mkwe anatak nimpe Talaka mwanae ili afute kesi nikalipa zamana nikaambiwa Nilipoti kesho Asubui.

Asubui na Mapema nìkafika mimi pamoja na ndugu zangu Mara paaah namwona Ma Mkwe na mke wangu hao...Polisi Wakasema Tukae Pembeni Tumalizane kisha tuwape Jibu kamili.

Mama Mkwe Msimamo wake Talaka itoke ili kesi ifutwe...Pale pale Nikamuuliza Mke wangu je Umerizia nikupe Talaka akajibu Ndio na anitaki ata Kuniona Nikaona sawa kesi ikafutwa Nikaona isiwe Tabu Twendeni nyumbani ukachuke Vitu vyako na Talaka yako Tukaongozana akabeba kila kitu chake nikamchenjia nikamwambia Talaka Nitaitoa kesho yake Sio Leo wakakubali wakaondoka.

Kwa Kweli Niliishi kwa Tabu sana kwa Kuwa Nilimpenda Sana Mke Wangu na Nilimzoea sana..Nikaanza Kujichaganya na Anasa za Dunia kama Pombe na Wanawake....kwa Kweli Nilibadilika sana.

Baada miezi kama Miwili nikaanza kupokea Jumbe Mbali mbali kutoka Majirani na ndugu zangu wakisema Mke wang anawasumbua wamwombee Msamaha kwangu kuwa Anajuta Sana huko Alipo.


Nikawa Napuuzia..Lakini hakuchoka akahamia kwa wazazi wangu akawa anawasumbua Usiku kucha ikawa kero Sasa kila Siku anawaangushia kilio na kuzingatia wazazi wangu ni watu wa dini wakaanza kuingiwa na Imani wakaanza nao kunisihi kama ni funzo Ashalipata ivo nimsamehe tuu..

Nikaanza Kulegeza Mke wangu naye Akaanza kunichek direct Msamaha mwing lakini nikawa namkatisha tamaa na maneno makali lakini hakuchoka Alilia Sana Simu Usiku kucha Anajuta sana kumsikiliza Mamayake.

Kwa Kweli Kibinadamu Nilishindwa kuhilimili nikarudisha moyo na Nikaruusu Arejeee Maisha Yaendelee japo Nilishaanzisha Mahusiano na Wanawake Wengine Wengi.

Kweli akarudi maisha Yakaendelea Tukasau Matatizo Yote Tukaishi kwa Furaha sana kama miezi 8 ivo Mungu Akajaalia akashika Ujauzito Tulifurahi Sote na Tukaona ndoa Imenoga SAS ata Maendeleo ya kiuchumi Yakaongezeka.

Na kipindi chote icho Tulikuwa mbali Sana na Ma Mkwe na Sikuruusu ata Awasiliane nae kweli naye akatii Maisha Yakasonga vemaa.Japo Kuna kipindi Nilikuta sms akimjulia hali mke wang...kwa hasira simu yenyewe nikampokonya na akatiii maisha yakendelea akabadilika sana Yaani mke Bora Kwelikweli kila Mtu Alimsifia.

Sasa Mimba ikaendelea kukua yapata kama miezi 6 ivi..siku moja akaenda Clinic asubui na Mapema kufika mchana Nashangaa anarudi Analia na kunambia kuwa mimba imeharibika na Cha Ajabu zaidi Eti Iliacha kukua Tangu mwezi Mmoja Uliopita...hili likawa Jipya Kila Mtu Aiieskia Alishanga.

Na Yeye aliendelea Julia kuwa Akubali baadae akaja funguka kuwa Mamaake mzazi Almtamkia kuwa hawezi Jifungua salama au akijifungua atajifungua chura...kwa kweli Nilitahamaki na Hasira na Jazba Juu..Wazazi kwa kuwa ni watu wa dini wakampigia Ma mkwe Aje kweli alifika Wakamsema Sana kwa Kauli alizozitoa na Ma mkwe akaomba Radhi kwa Kauli Alizozitoa na Kusema Tusahau Yaliyopita na Tugange Yajayo kwani hata Yeye sasaivi anamsapoti mwanaye kwenye Ndoa Yake.

Lakini Chaajabu Nilichoshanga Ma Mkwe Akaanza kuongea Kauli za Ajabu Eti kuwa si bure kuna watu watakuwa wamemfanyia mchezo mwanaye ili mimba itoke Kwaiyo Ataenda kwa Mganga Kuangalia vizuri ili amkinge.

Mimi Kuskia ivo nikakataa kabisa Mambo ya Waganga staki tena Staki nimemwachia mungu...Ma Mkwe akaondoka kwa hasira kwanini Nimempinga.

Ikapita Siku Kazaa Sasa ivi Majuzi nimepigiwa Simu na Daangu niende anajambo ZITO anataka nambie,kufika Pale Nilichokiskia Aiseeeeh naweza Kuchukua Maamuzi magumu Muda Wowote

Eti mke wangu anatangaza kwa ndugu na Jamaa zangu kuwa Nimeenda kwa mganga nimetoa kafara Mtoto ili Nipate Utajiri....na kila Mtu anajua ila Wanaogopa kunambia Jambo ZITO kama ilo.

Kwa Kweli Nililia kama Mtoto tena mbele ya Dadaangu nikaomba Msaafu Niape...ivi Uyu Mwanamke Ana nini Kwa Kweli Imetosha Imetoshaaaa kama Nafasi Nishampa Sana...Japo Wazazi Wangu Wanamtetea na kunisihi sasaivi abadilike Kwaiyo nimsamehe Niendelee kuishi nae.

Kwa kweli Siwezi Moyo wangu Unauma sana hadi kula Nashindwa...Kuna muda Nikikaa naisi kifua Kinaniwaka Moto....Nashindwa Vumilia Kabisa Safari hii Nimeona Isiwe Nimehama Pale home karibu na wazazi na nimemwaambia mke Ande kwao...Lakini kagoma na mpaka ivi Sasa yupo kwa wazazi wangu.

Na Leo hii Ndo Nataraji kwenda kufanya Maamuzi ya mwisho mana wamenishawishi kwa Kila namna Nimsamehe lakini nimegoma kwa kweli Siwezi Aende Tu kwao ameniumuza amenitesa
 
Kwa kuwa ni hadithi unasimua sawa endelea..

Kama ni uhalisia basi nadhani Mzaramo na sherehe ni kama bahari na chumvi haviachani uvumilie. Angalizo ukiona mwanamke anasumbua sanaa angalia upande wa kikeni kwao pana nguvu hasa mama mtu..

Kijana ukioa sehem mama mkwe anasauti kuliko babamkwe ACHANA NA HIYO NDOA UTAZEESHA AKILI.
 
Habari Wanajamvi Leo Naomba Niwasilishe Mkasa wangu unaonisibu hivi Sasa katika Maisha Yangu....Ndoa...Ndoa..Ndoaaa..

Baada ya kusaka Life Miaka 2 Nyuma na kujihakikishia Uwezo wa Kula kuvaa,Malazi,Starehe Nikiwa na Miaka 24 tu Nikaamua kumtafuta Mwenza wa Kujenga nae Life..



ITAENDELEAAAAA
ITAENDELEA???? Kwani hii ni hadithi au maswahibu unataka ushauri?? Au siku hizi JF ndio fashion kuweka itaendelea??
 
Habari Wanajamvi Leo naomba niwasilishe mkasa wangu unaonisibu hivi Sasa katika Maisha Yangu....Ndoa...Ndoa..Ndoaaa..

Baada ya kusaka Life Miaka 2 Nyuma na kujihakikishia Uwezo wa Kula kuvaa,Malazi,Starehe Nikiwa na Miaka 24 tu Nikaamua kumtafuta Mwenza wa Kujenga nae Life..


Kwa Kweli Nililia kama Mtoto tena mbele ya Dadaangu nikaomba Msaafu Niape...ivi Uyu Mwanamke Ana nini
Mzee mmoja wa kichaga alikuwa anampa wasaa mwanae wa kiume kwenye harusi yake. Akamwambia "Mwanangu mimi sitaki kupindisha maneno. Nakuambia ukweli. Ukubali ukatae shauri yako. Akamwambia kwenye ndoa yako ukiona vituko vimezidi cheki mfukoni mwako au katika account yako ya benki.Ukiona mfuko uko vizuri na benki uko vizuri na bado vituko haviishi ujue wewe ndio tatizo. Lakini ukiona mfukoni hauna kitu na benki hauna kitu na vituko haviishi tafuta hela.

Ukishindwa muache mtoto wa watu aende. Kama ni wako atarudi. Kama sio wako sio wako tu hata ukeshe unaomba. Sikubaliani na "conclusion" ya huyu mzee wa kichaga lakini siwezi kumpinga kwa sababu ni mzee na ameona mengi.
 
Habari Wanajamvi Leo naomba niwasilishe mkasa wangu unaonisibu hivi Sasa katika Maisha Yangu....Ndoa...Ndoa..Ndoaaa..

Baada ya kusaka Life Miaka 2 Nyuma na kujihakikishia Uwezo wa Kula kuvaa,Malazi,Starehe Nikiwa na Miaka 24 tu Nikaamua kumtafuta Mwenza wa Kujenga nae Life..
Achana na mwanamke wa kizaramo mkuu. Mm mzaramo nawajua fika hawa watu. Achana nao Hao watakusumbua na kukusanya ndondocha hao
 
Habari Wanajamvi Leo naomba niwasilishe mkasa wangu unaonisibu hivi Sasa katika Maisha Yangu....Ndoa...Ndoa..Ndoaaa..

Baada ya kusaka Life Miaka 2 Nyuma na kujihakikishia Uwezo wa Kula kuvaa,Malazi,Starehe Nikiwa na Miaka 24 tu Nikaamua
Katika upuuzi ambao siupendi na sitaki kuusikia ni huu wa masuala ya birthday

Kijana m nakushauri kma uloyasema yana ukweli ni bora ukamuacha huyo mkeo na utafute mwengine tu
 
Back
Top Bottom