Maisha yangu mabaya sana nakaribia kujiua

Maisha yangu mabaya sana nakaribia kujiua

Pole sana.kuna wengine wana matatizo zaidi kuliko wewe.punguza misaada. Jiwekee malengo. Hiyo hiyo laki mbili ipunguzie matumizi .kama unaweza biashara fikiria unachoweza ili ufanye na huku una kazi yako.nina rafiki yangu mshahara wake ni chini ya huo ila yeye ni mpishi Wa keki ilimchukua miaka 8 kuweza kujenga kisehemu kununua vifaa na kuajiri mtu Wa biashara hiyo ya keki.maana alidunduliza miaka yote. Usiwe na haraka ukajihisi umechelewa.
we umesoma vzr kwel, yan umeona lak 2 apo
 
Isee unapokea hella yote Hiyo halafu hauna amani na maisha, mpunga mrefu huo kujua sana kunakupa tabu. Kuna Jamaa hapa anakazi yakuunga unga lakini anatoka kitambi. Usitake kuwa kamafulani wakati uwezo huo huna. Ni ndoto ya vijana wengi wakitanzania kupata mshahara kama huo
Robert Nesta Marley
Screenshot_2018-04-18-03-06-59.jpg
 
Ushirikina uko apii hapo alipozungumzia mshana au umekurupuka
Duuuh! Wewe kuogea maji ya chumvi na mzeituni kuondoa mikosi unaona sio ushirikina? Ina maana yana supernatural power ya kuondoa hiyo mikosi, ila yote kwa yote, nimejaribu kutoa ushauri tu nikiamini kila kitu kina mwanzo, Leo utaogea maji ya chumvi, kesho utaambiwa uvae chupi nyekundu, keshokutwa uchinje mbuzi mweupe na mwisho utavaa tunguri
 
Kama usemayo yana ukweli,
Lakini wewe unauhitaji na kazi anayoweza kukufanyia Shekhe,
Au kazi na Maisha ya Shekhe?

Kuchanganya Upumbavu kwenye mambo ya Msingi ni umajununi.
Kama maisha yao hayareflect wanacho kifanya mbele ya jamii kuna haja gani ya hiyo huduma. Si ni kuongopeana hapo.?
 
Kama wewe ni mhehe, hata kama ntakuzuia, utajiua tu maana kwenu kujiua ni ushujaa wa kuukimbia ukweli.

Ndugu, huna sababu ya kujiua, maana Mungu anayo sababu ya kukufanya uwe hivyo ilivyo. Cha msingi, stahimili, punguza wanaokutegemea na kama wapo isiwe katika kuishi bali katika kuwajengea uwezo, then kama umedate na wabebez hafu wote wakaugua severely, jitathmin, punguza mahusiano au wacha kwanza upumue.

Pia uwe mtu wa ibada japo yakupasa pia kuabudu kitu sahihi na siyo kufuata mkumbo, bali abudu katika roho na kweli, na biblia iwe kiongozi wako na siyo mwanadam maana wanapotosha walio wengi.

Mwisho wa siku utafanikiwa tu
 
Achana kwanza na hao wa upako ,,mtafute sheikh akusaidie kukuingiza katika dini ya haki na kweli ( uislam) uitamke shahada na uingie katika dini kwa imani yakini baada ya hapo upate visomo mujarabu. Kwa uwezo wa mwenyez Mungu insha Allah hayo matatizo yako yatafika mwisho. Fikiri sana juu ya comment hii ndugu yangu.

Acha kumpotosha mwenzio

na propaganda zenu
 
Sikushauri kwenda kwa hao watu, maana kuna mdada anajiita super women ndio kansela wao wanawake lakini matendo anayoyafanya yeye ndio anahitaji kukanseliwa kuliko mtu mwingine yoyote.
Sawa nashukuru, ukipata referral ntashukuru sana kaka. Maana nna mtoto wa dada yangu anahitaji sana hii session.
 
Pole sana.kuna wengine wana matatizo zaidi kuliko wewe.punguza misaada. Jiwekee malengo. Hiyo hiyo laki mbili ipunguzie matumizi .kama unaweza biashara fikiria unachoweza ili ufanye na huku una kazi yako.nina rafiki yangu mshahara wake ni chini ya huo ila yeye ni mpishi Wa keki ilimchukua miaka 8 kuweza kujenga kisehemu kununua vifaa na kuajiri mtu Wa biashara hiyo ya keki.maana alidunduliza miaka yote. Usiwe na haraka ukajihisi umechelewa.

Ni milion 2 sio laki 2
 
Changamoto zingekua chanzo cha kujiua Dunia isingekua na watu...wewe inaonekana umejikita sana kwenye ushirikina sasa ndio yanakutesa na hujui ufanyaje kusaidia ndugu sio tatizo nani awasaidie kama sio wewe swala jipange na uongeze kipato maisha yaende 2m sio nyingi kuona umemaliza au unatumia kipato kikubwa sana kumbuka na wewe umesaidiwa ujakaa hapo kwa miguu yako...
 
Kuna wenzako wana matatizo kama hayo na hawana kipato kama chako na bado wana survive... Achana na wazo la kujiua
Kuna tiba moja rahisi sana lakini very effective.... Ni tiba maarufu na imewasaidia wengi na mfanyaji ni wewe mwenyewe
Tiba ya kuogea chumvi hasa nzuri ni ile ya mabonge... Hicho tu.. Ogea mara mbili kwa siku kwa mwezi mzima huku kila ukiogea unanuizia mabaya yakuondoke na uwe na ladha kama chumvi
Mafuta yako yawe ya mzeituni... Jaribu hiyo hutojuta na haina side effects wala gharama za kazi
Sasa hiyo Mshana haina tatizo na mahusiono na Mungu?
 
Ndugu zangu,

Kama nilivoandika kichwa cha habari mimi ni kijana niliye ajiriwa na mapato yangu kwa mwezi nikama 2000000 hivi.

Lakini nimekosa furaha kiasi kwamba sina furaha na maisha pamoja na watu wanaonizunguka hata hiyo pesa yote huishia kumaliza matatizo ya ndugu na kila mwanamke naingia naye kwenye mahusiano basi hata anza kuumwa kiasi pesa yote inaenda kumhudumia mgonjwa.

Sasa najiuliza nitakuwa nimerogwa au na kipindi hiki ndo nimekosa kabisa ujasiri wa maisha sasa je hiyo hali ya kawaida au kuna michezo ya kiswahili nafanyiwa na kama yupo mganga anitibie nikipona ndo namlipa maana nimeenda kwa hawa wa upako naona maigizo kabisa mtu ananiombea sijazimia ananilazimisha kuniangusha na wale wasaidizi wanashika kwa nguvu kama nina matatizo wakati nipo vizuri, ndo nikaona wote hawa maigizo.

Nimeenda kama kwa wa upako wa nne hivi wote hivohivo.

Sijui nifanye nini.
Alien pole sana. Kwanza angalia positives nyingi ulizonazo. Una mshahara mkubwa, naamini umesoma na mengine mengi binadamu usituone hupitia changamoto nyingi lakini binadamu tumeumbwa kukabilianan nazo. Aidha usione watu wanatembea wana matatizo ila tu hawayasemi. Ungetegemea campaign ya Makonda kuibua maelfu ya wanawake? na mamia ya wanaume sasa inakubidi kukabiliana nayo. Mimi ni Professional Counsellor - Njoo inbox
 
Ndugu yangu achana kabisa na hao wanaojiita waombezi(wachungaji), hao watu ni waongo kuliko Nabii Tito, hawaponyi chochote pumbavu hao.
 
Ndugu zangu,

Kama nilivoandika kichwa cha habari mimi ni kijana niliye ajiriwa na mapato yangu kwa mwezi nikama 2000000 hivi.

Lakini nimekosa furaha kiasi kwamba sina furaha na maisha pamoja na watu wanaonizunguka hata hiyo pesa yote huishia kumaliza matatizo ya ndugu na kila mwanamke naingia naye kwenye mahusiano basi hata anza kuumwa kiasi pesa yote inaenda kumhudumia mgonjwa.

Sasa najiuliza nitakuwa nimerogwa au na kipindi hiki ndo nimekosa kabisa ujasiri wa maisha sasa je hiyo hali ya kawaida au kuna michezo ya kiswahili nafanyiwa na kama yupo mganga anitibie nikipona ndo namlipa maana nimeenda kwa hawa wa upako naona maigizo kabisa mtu ananiombea sijazimia ananilazimisha kuniangusha na wale wasaidizi wanashika kwa nguvu kama nina matatizo wakati nipo vizuri, ndo nikaona wote hawa maigizo.

Nimeenda kama kwa wa upako wa nne hivi wote hivohivo.

Sijui nifanye nini.

Habari mkuu.

2 m per month unafikiria kujiua? You don't have a purpose in life mzee! find one! Hauko peke yako kwenye hiyo situation, just kumbuka tatizo halikimbiwi. Hayo ni machangamoto ya maisha ambayo bila kuyashinda binadamu hatuwezi kufika dream land!
Amka asubuhi, sali sana kumshukuru Mungu aliyekuumba, kunywa chai, tafuta gazeti..soma ukifika ofisini. Fanya kazi iliyokupeleka, nenda lunch, rudi...sikilizia some musics to pass time, kunywa glass ya maji....fikiria ni nini utakifanya kesho then lastly STAY POSITIVE!
 
kabla hata sijasoma ulichoandika nasubutu kisema ""Acha upuuzi dgo""
 
Pole sana.kuna wengine wana matatizo zaidi kuliko wewe.punguza misaada. Jiwekee malengo. Hiyo hiyo laki mbili ipunguzie matumizi .kama unaweza biashara fikiria unachoweza ili ufanye na huku una kazi yako.nina rafiki yangu mshahara wake ni chini ya huo ila yeye ni mpishi Wa keki ilimchukua miaka 8 kuweza kujenga kisehemu kununua vifaa na kuajiri mtu Wa biashara hiyo ya keki.maana alidunduliza miaka yote. Usiwe na haraka ukajihisi umechelewa.
Laki mbili au milioni 2? Acha kutupunguzia kodi yetu watanzania
 
Unapata mshahara wa 2mil kwa mwezi unawaza kujiua!? Jiue tu aisee hakuna namna.
 
Back
Top Bottom