Firmino bobby
JF-Expert Member
- Mar 7, 2018
- 228
- 594
Muda mrefu nimekua msomaji tu wa mada zenu nikifuatilia karibu kila post inayowekwa katika mtandao huu, nina circle ndogo sana ya marafiki na watu ninao fahamiana nao kwa muda mrefu sasa hali inayo ni fanya muda mwingi ninao upata niwe nautumia kuwasomeni enyi wakuu wangu, ninavyo vingi vya kuandika lakini hua nnaona mengi mme yasema tayari.
Nimesema hivyo kwa sababu nilipaswa kurejesha mrejesho humu tangu muda sana, ila mara zote nilikua nikisita nasema nifanye baadhi ya vitu kwanza, siku nikitoa mrejesho watu waone hii kweli kulikua kuna sababu kubwa ya mimi kufanya hivyo.
Miaka miwili iliyopita, nilikuja hapa jukwaani kuwaombeni msaada wa kielimu na kimawazo, nilikua nimetoka kuhitimu chuo kikuu ngazi ya shahada ya sheria na sikuwa na ishu mtaani, niliwaelezeeni jehanamu niliyokua napitia, na ntaiambatanisha mwisho wa stori hii kama kithibitisho. Wakati naleta uzi huo sikutegemea kama ungeweza kua mkubwa kiasi kile, niliuandika uzi ule saa 10 alfajiri nikiwa nimekosa usingizi kwa stress, na niliandika, just kuandika tu ukweli, then nipate relief tu. Najua toka mwanzo kusaidiwa sio jambo jepesi.
Niliandika uzi ule na nikaendelea na ishu zangu zingine, baadae siku hio naingia nakukutana na meseji kama 50 ivi, ilinistua hata mimi mwenyewe kwa kweli, sasa toka hapo nikaanza ku-chat na watu wengi sana, kufikia usiku huo niliona maisha mbona kama yamebadilika kiutani sana, ni watu wengi waliguswa na masimulizi yangu yale mpaka mimi mwenyewe nikaanza kuogopa, nikasema kumbe kuandika ukweli hali huwa ni tofauti sana na stori za kutunga.
Nilikuja hapa jukwaani nikiomba msaada kutoka kwenu kwamba nahitaji kuendelea na elimu ya sheria, hasa mfumo wa nchi yetu ulivyo ni kwamba ukihitimu Degree ya Sheria hautaruhusiwa kufanya uwakilishi wa kisheria mahakamani au kua na muhuri ni mpaka uende ukajiendeleze Shule ya Vitendo vya Sheria (Law School of Tanzania) Sasa basi, baada ya wadau kusoma maswaibu yangu, niliwasiliana nao kwa uwingi sana, nilipata meseji chungu mzima watu wakiniambia nipambane, wakinipa moyo sanaa na wengine waliniahidi vingi sanaa sanaa, sijapata kuona upendo wa vile.
Asikwambie mtu bhana, Watanzania ni tunapendana yakija masuala ya matatizo. Nilipata simu watu wananiambia njoo nimefungua banda langu la mishikaki, njoo nikuajiri hata uwe meneja wa grocery yangu, ili mradi tu kila mtu ahusike na mchango wa namna moja au nyingine. Wengi wakiniambia utapata ada kisha utaenda zako kujiendeleza, ada wakati huo ilikua ina hitajika milion 1.7 na bado mengine ya kumfanya msomaji aendelee kuwa eneo lile, na niliweka wazi kwamba nilikuwa kijana wa geto tu sina ishu yoyote wala ndugu wa kupiga tafu. Mpaka baada ya siku tatu nilipiga hesabu ya ahadi pekee ya pesa ambazo ntazipata kama ada ilifika karibu milion 4, nikasema mambo ndio haya, na kwa kweli nilikua na furaha kupita kiasi.
Kufupisha stori, michango niliyoipata sikumbuki kama ilifika hata robo ya ada iliyokua inakusudiwa, na wachangiaji hawakufika watano, licha ya kupata ahadi karibu 70 huko, lakini kwenye wengi kuna mengi, kuna Mtu mmoja aliguswa kupita kiasi, ukiondoa wengine watatu ambao mpaka kesho tumeshakua ndugu kabisaa, ila huyu mmoja alikua special sana. Ni mwanamama naomba atambulike kama 'mtu special', aliniambia jambo moja tu "mimi nataka kukusaidia, nimeona spirit iliyoko ndani yako, mara kadhaa nimepanga kuku-ignore tu ila nikilala usiku najiona kama nna deni ambalo ninapaswa kulilipa, nahisi ni wewe", sitasahau hili, japo mwanzo nae nilimtilia mashaka nikaona ni sawa tu na wale wazee wa ahadi ila utekelezaji ni ngumu mno.
Hapa nilijifunza kuwa watu wengi ni wazuri kwenye ahadi ila kutimiliza ni ngumu mnoo mnoo, kuna watu waliwahi kuniita mpaka kwenye ofisi zao ili wanione tu nafananaje, wakanipa ahadi nyingi na tena wakani-drive mpaka geto kwangu uswahilini wakaona kila kitu ila kwenye ahadi wakapotea, wengine waliahidi mwisho wakawa wanasema yawezekana wewe ni tapeli tu; hahaha! daa wabongo. Huyu mama alikua tofauti sana, mwanzo alisema ata top up michango ntakayo ipata, nae alisoma comments zote akajua tayari sikosi chini ya milion 2, ila nilivyo mueleza ukweli wa kiasi nilicho pata akasema chukua hii milion kalipe ada alaf tuone hio nyingine itakuaje hahahaaahh nilichizi, nikasema haya masikhara, lakini nikazichukua nikaenda kulipa.
Yule mtu special alifurahi sana, basi siku zikawa zinakimbia za kujiunga pale na hela haionekani, waahadi wamekata mawasiliano, out of nowhere jamaa mmoja akaniomba namba inbox, tukawasiliana, yuko Botswana akanitumia laki tatu akaniambia kijana nakuamini nenda kasome utafika mbali sana, huyu mtu sitokuja kumsahau maishani na tunawasiliana mpaka leo ofcoz. Yule mtu special akafanya fund raising kwa jamaa zake wengine wako ughaibuni, kufumba na kufumbua ada imekamilika na hela kiasi ya kwenda kunipiga tafu mambo ya msosi.
Nilifanikiwa kujiunga na Law School, huku mtu special akiniambia nawekeza kwako ili wewe uje uwasaidie wengine, nitabarikiwa kwa kupitia wewe, mimi nina maisha tayari sina nitakalo hitaji toka kwako, mtu special akaniambia nitakupangishia karibu na icho chuo na usome, so yote yakawezekana kwa msaada wake, alinisaidia kiasi sijapata kuona mtu akisaidiwa vile, yote ikiwa hata hajawai kuniona tunaishi maeneo tofauti mbalii, sikufanya ajizi wala, nilikua ninaenda darasani saa 12 asubuhi natoka saa 2 usiku, nilisoma kiasi sijawai kusoma vile katika maisha yangu, ilifikia point nikawa naona kwenye sheria mbona hakuna mtu ananikuta kabisa. Mind you, mimi nilikua nimetoka uswazi nimeona gap ni lipi nifanye vipi kutoboa na nikajua kabisaa mchawi ni nini.
Nilimaliza Law School kwa msaada mzito, msaada wa hali na mali na kila kitu anachohitaji mwanafunzi, na nilihitimu vyema na niweke wazi tu kuwa nilifaulu mitihani yote niliyoingia darasani kuifanya, mitihani zaidi ya arobaini yote niliifaulu, na katika wanafunz 600 tuliofaulu tulikua chini ya 60 tu, sawa na asilimia 8 mpaka 10 ya wanafunzi wote, wenyewe tunasema first seating.
Nilifanya mchakato wa kuapishwa kuwa wakili na nilifanyiwa interview na Jaji Mkuu wa nchi ambaye katika mazungumzo yetu katika ofisi yake nilimgusia namna nilivyofika mpaka mbele ya ofisi yake siku hio kwa ajili ya kupitishwa kua wakili, Jaji Mkuu alifurahi sana, baada ya interview yake mwisho akaniambia nimekukubali kuwa Wakili wa Mahakama Kuu na Mahakama zingine za chini yake isipokua Mahakama ya mwanzo, hii siku nilirudi gheto kwangu uswazi nililia sana, sitoisahau hii siku na ule usiku wa matokeo ya Law School.
Baada ya hapo kila kitu kikawa historia, njia nilikua naijua tayari, na siku maliza hata wiki moja nikapata kesi madai Kisutu hapo na nikaimaliza kesi ndani ya miezi miwili tu na nikalipwa hela ambayo kwa wakati huo sikuwahi kulipwa mahala kokote duniani toka nizaliwe, nika hisi kwamba hakuna linalo shindikana, zilikua ni baraka za ajabu lakini ilinifikirisha sana na nikajua kua yote yanawezekana kwenye juhudi kuna fanikio lolote lile.
Kufupisha stori kabisa ni kwamba, sasa ni muda kiasi tangu niapishwe kuwa wakili, wale watu wangu niko nao karibu sana, tumeshakua ndugu kabisaa na wao wana amani na kujivunia mimi, lakini mpaka naandika uzi huu usiku huu leo nikutaka kusema tu kuwa, bado sijafanikiwa kwa kiasi hicho ila nimeanza kurudisha nilichokipata toka kwenu, mpaka sasa nina karibu kesi sita nimeshinda, na ninazo endelea nazo mahakamani ziko katika upande mzuri kwangu kushinda japo mahakama ndio mwamuzi wa mwisho.
Sijawahi kushindwa kesi yoyote mpaka muda huu, na katika hizi kesi nilizoshinda tatu kati yao niliwasaidia watu ambao hata hela ya kununua chai tu hawana, bure kabisaa, kisa kimoja kati ya hizo kesi ni kile cha familia moja huko Pugu kudhulumiwa mali zao zote ikiwemo nyumba ya kuishi na walikutana na mimi katika wiki ya sheria nikawasaidia nyumba yao ikarudi bure bure bila hata wao kunipa chochote, hata nauli nilitumia za kwangu.
Lakini kuna kijana mmoja alikua amesingiziwa kesi ya kubaka na yeye hakua hata na shilingi mia, nashukuru nae sasa hivi ni mtu huru, lakini bado kuna kesi zingine ziko mahakamani za hawa watu wachache wasio jiweza kabisaa nawapambania na inshaAllah tutashinda tu.
Kuna mengi yana endelea tangu nikutane na hawa watu wa kutoka jamii forums, mimi binafsi maisha yangu yamekwisha badilika pia, nisingependa kusema yote ila kwa uchache tu nilipokua miaka miwili iliyopita sipo huko tena, toka kwenye geto uswaz mpaka nyumba nzima nje kidogo ya mji na mengine mengi ambayo Mungu anaonesha ukuu wake kwa kupitia mimi.
Na imefikia hatua kila nInapo enda kulala najiskia kabisa kuWa kuna watu wanaombea nisiumwe ata maralia nikakosa kwenda mahakamani kuwasaidia hawana msaada wowote kwa wakati huu isipokua mimi, watu wengi ni wana vipato vidogo mnoo ambavyo hata wao kula haviwatoshi ila ukiona ninavyo watetea mahakamani utasema wamenilipa mamilion, najitoa kwa hawa wote yote ni kwa sababu ya Jamii Forums, ni JF ndio imenipa moyo mpya huu nilio nao na bado kuna dogo yuko Law School na mimi ninampiga tafu sababu stori yake ni sawa na yangu kwa kiasi fulani.
Mwisho kabisaa, nipende kumshukuru kila mmoja wenu kwa nafasi yake na kujitoa kwake kwangu na kwa watu wengine ambao wako kama mimi nilivyo kuwa, msichoke kusaidia, hamjui hao mnao wasaidia kesho yao kuna nini, ukijihisi unaweza kumsaidia mtu tafadhali usisite, fanya hivyo mara moja, ni maono Mwenyezi Mungu kakupatia, tafadhali hakuna msaada unaopotea hivi hivi, usichoke kusaidia kunaleta faraja na amani sana, na tukumbuke mwisho wa siku sote tutakufa tu, we are nothing. Tuache legacy na kila kitu kizuri kwa ajili ya hawa wajao.
Poleni sanaa kwa gazeti hili reefuuu, ila nasema AHSANTENI SANAAA, siku zote nitakua hapa, nitaendelea kuiheshimu JF kupita jambo lolote na hata mtoto wangu wa kwanza atapata jina lenye maana sawa au inayo endana na Jamii Forums. Kama nawe una ushuhuda unaweza uka-share tu kwa ajili ya expirience kwa watu wengine na ukawa-inspire sanaa watu wakaendelea kuwasaidia wenye mahitaji.
Wakili.