GE2025 Mahakama yaamuru mashahidi kesi ya Tundu Lissu walindwe

GE2025 Mahakama yaamuru mashahidi kesi ya Tundu Lissu walindwe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Ila hiyo sheria ya mashahidi wa siri, kuna siku itamtokea mtu puani na ndio watajua sheria ni msumeno, kwa sheria hii hamna alie salama, na zitaibuka kesi nyingi sana za watu kutaka kuficha mashahidi na hii ndio ya kwanza, kwa kumficha shahidi huwezi kutoa wala kupata haki
Itakuwa kutumika kwao walioitunga na kuipitisha
 
Hivi duniani kuna kitu kama hichi katika utoaji wa haki au sisi ndiyo wa kwanza kuvumbua utaratibu huo? Wanafanya hivyo ili kesi iwe ndefu sana
Rejea kesi ya uhaini ya akina maganga, hans pope{rip}, utaratibu huo ulitumika
 
Watajulikana tu kwa maneno ya ushahidi wao. Mbona wanaovaa Musk pale kizimbani picha zao mpaka walizokuwa shuleni zinaanikwa mitandaoni?
Kuna watu watavujisha serikalini sio kila mtu aliyepo serikalini wanafurahia suala la Lissu huyu Lissu ni Mtanzania mwenzetu kwao Ikungi hana makandokando yoyote shule alizosoma zinajulikana uraia wake hauna mashaka yoyote Lissu hajawai hata kumiliki bastora Istoria yake inaonyesha hajawai kua na kesi yayote tofauti na za kisiasa anajulikana mpenda haki Amuache aende zake Lissu hana shida na mtu anataka hii Nchi tufaidike wote kinachoendelea kura kwa wajumbe CCM ni aibu reforms zitakuja ni suala la Mda watu wa sasa ni tofauti na Wazamani
 
Inaonekana kabisa wanachezea mahakama yaani siku nzima vinavyoongelewa hata havieleweki...
Na wanajua tarehe ingine watasema nini kwa wamekuja kuwalinda watoa ushahidi na si mtu ambae anatuhumiwa kesi ya uhaini..
 
Kuna watu watavujisha serikalini sio kila mtu aliyepo serikalini wanafurahia suala la Lissu huyu Lissu ni Mtanzania mwenzetu kwao Ikungi hana makandokando yoyote shule alizosoma zinajulikana uraia wake hauna mashaka yoyote Lissu hajawai hata kumiliki bastora Istoria yake inaonyesha hajawai kua na kesi yayote tofauti na za kisiasa anajulikana mpenda haki Amuache aende zake Lissu hana shida na mtu anataka hii Nchi tufaidike wote kinachoendelea kura kwa wajumbe CCM ni aibu reforms zitakuja ni suala la Mda watu wa sasa ni tofauti na Wazamani
Anatakiwa sasa akayathibitishe hayo mahakamani
 
Kesi ambayo mshitakiwa akikutwa na hatia atanyongwa hadi kufa kwa nini mashahidi wawe wa GIZANI. Nini kitakata kufichwa?

Hapa kateni rufaa - ngoma hadi ifike rufani.
Wanaweza kua wanataka ichi mda uendelelee kwenda
 
Fear of the unknown...! Wenye hatia huogopa hata vivuli vyao
 
..Ni kweli kuna sheria ya kulinda mashahidi.

..Je, ni sahihi kwa utaratibu huo kutumika katika kesi dhidi ya Tundu Lissu?

..Ndio maana tukakumbusha kwamba ktk kesi ya uhaini ya mwaka 1984 kulikuwa na mashahidi wengi lakini waliolindwa ni wawili tu, shahidi X, na shahidi Y, ambao walikuwa wakuu wa idara ya usalama.

..Je, kwa kuzingatia mashahidi, na nature ya ushahidi, ktk shauri dhidi ya Tundu Lissu kuna uhalali wa mahakama kutumia sheria ya kulinda mashahidi.
Lissu alitamka azarani akasema kukinukisha sasa kwa nini wafiche Mashaidi inakiwa wawambie mahakamani mchana kweupe bila kuficha kwamba uhaini aliufanya wapi na washirika wake Uhaini hawezi kua mtu mmoja kwanza Lissu ana kiapo gani cha serikali mpaka hawe Muhaini ana siri gani za Serikali ujinga ujinga tu
 
Wanaosema ni Social media wao awapo ata mahakamani. Tujua kua Lissu si malaika inawezekana akateleza akakosea kwahiyo tusimuone kama malaika
Ingekuwa ni kweli sio malaika na anaweza kuteleza leo hii kesi yake ingekuwa imeisha na ameshanyongwa. Unapoona danadana ujue ni siasa chafu za ccm ndani ya hizo mahakama zinazotumika.
 
..Ni kweli kuna sheria ya kulinda mashahidi.

..Je, ni sahihi kwa utaratibu huo kutumika katika kesi dhidi ya Tundu Lissu?

..Ndio maana tukakumbusha kwamba ktk kesi ya uhaini ya mwaka 1984 kulikuwa na mashahidi wengi lakini waliolindwa ni wawili tu, shahidi X, na shahidi Y, ambao walikuwa wakuu wa idara ya usalama.

..Je, kwa kuzingatia mashahidi, na nature ya ushahidi, ktk shauri dhidi ya Tundu Lissu kuna uhalali wa mahakama kutumia sheria ya kulinda mashahidi.
Kama mashahidi hao ni kama hao hao uliowataja kuna shida.Lakini kumbuka kuna Protection of witness and whistleblower's act mkuu.
 
Hii nchi tunakoelekea ipo siku wataomba mahakama itoe majaji wasionekana
 
Ndiyo maana sheria ya jinai kama treason nk kuna sheria ya kulindwa kwa shahidi.Protection of the witness and whistleblower act
Mkuu, Nakubaliana na wewe.. uwepo wa sheria kama Protection of Witnesses and Whistleblowers Act, hasa kwa kesi nyeti kama uhaini au ugaidi. Lakini hata sheria hizo ziko chini ya Katiba zinapaswa kusikiliza haki ya mshtakiwa kupata haki ya kujitetea ipasavyo, ambayo ni fair trial.

Ukilinda mashahidi kwa kuwaficha majina, uso, sauti, na kila kitu kisijulikane, unamnyima mshtakiwa haki ya msingi ya kuuliza maswali. Hii sheria inaweza kutumika vibaya na historia ya nchi nyingi duniani inaonyesha hivyo.

Kwa hiyo swali si kama sheria ipo au haipo, swali ni: sheria hiyo inatumika kwa haki au kwa kulinda maslahi fulani ya kisiasa?
 
Mahakama Kuu imeamuru mashahidi ambao ni raia wanaotarajiwa kutoa ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, walindwe kwa maana ya kutoa ushahidi wao kwa kificho (bila kuonekana), majina yao kutokutajwa mahakamani wala taarifa zao zinazoweza kuwafanya wakatambulika, wao, familia zao, marafiki zao na watu wengine wa karibu yao.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu, Agosti 4, 2025 na Jaji Hussein Mtembwa kufuatilia maombi yaliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mshitaka (DPP), imezuia pia taarifa zao kusambaza, kuchapisha na kutangazwa na chombo chochote cha habari, bila ridhaa ya Mahakama.

Lissu, ambaye anakabiliwa na kesi ya uhaini alikamatwa Aprili 9, 2025 akiwa kwenye mkutano wa CHADEMA huko Mbinga kisha kusafirishwa hadi Dar es Salaam na baadaye kupandishwa kizimbani Aprili 10, 2025.

Chanzo: Mwananchi
Vyovyote vile watashindana ila hawatashinda
 
Back
Top Bottom