GE2025 Mahakama yaamuru mashahidi kesi ya Tundu Lissu walindwe

GE2025 Mahakama yaamuru mashahidi kesi ya Tundu Lissu walindwe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mahakama Kuu imeamuru mashahidi ambao ni raia wanaotarajiwa kutoa ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, walindwe kwa maana ya kutoa ushahidi wao kwa kificho (bila kuonekana), majina yao kutokutajwa mahakamani wala taarifa zao zinazoweza kuwafanya wakatambulika, wao, familia zao, marafiki zao na watu wengine wa karibu yao.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu, Agosti 4, 2025 na Jaji Hussein Mtembwa kufuatilia maombi yaliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mshitaka (DPP), imezuia pia taarifa zao kusambaza, kuchapisha na kutangazwa na chombo chochote cha habari, bila ridhaa ya Mahakama.

Lissu, ambaye anakabiliwa na kesi ya uhaini alikamatwa Aprili 9, 2025 akiwa kwenye mkutano wa Chadema huko Mbinga kisha kusafirishwa hadi Dar es Salaam na baadaye kupandishwa kizimbani Aprili 10, 2025.

SOURCE: MWANANCHI​

Tunahitaji rais mwenye kuyaelewa mapungufu mahakamani kama haya kuhakikisha tutakuwa na sheria za haki kwa kila mtu mahakamani.

binti kiziwi anazijua kero hizi?
 
Mnajenga chuki pasipo sababu.

Halafu Lissu naye anapambania wasiostahili kupambaniwa.
Ndio sababu Mtume Muhammad saw yeye hakutaka kubeba misalaba ya wengine alisimama na lile andiko la Yesu Kristo alisema “ auwaye kwa Upanga ataangamia kwa Upanga “

Nchi ya Kenya kwa mfano Katiba yake imesema kila Mtu atawajibika yeye binafsi kwa kila atendalo ndio sababu Kenya Askari Polisi anaruhusiwa kutotii Amri ya mkubwa wake kama inaelekea kuvunja Katiba
 
Maana yake kesi haitaoneshwa tena, wala haitakuwa na waangaliaji tofauti na yeye na mawakili zake.
Hapo ni Mahakama ya Rufaa tu ili hili swala lifutiliwe mbali maana wataumiza watu wengi kwa hizo kanuni.

Masaju kabariki hilo swala na Usabato wake
 
Ila hiyo sheria ya mashahidi wa siri, kuna siku itamtokea mtu puani na ndio watajua sheria ni msumeno, kwa sheria hii hamna alie salama, na zitaibuka kesi nyingi sana za watu kutaka kuficha mashahidi na hii ndio ya kwanza, kwa kumficha shahidi huwezi kutoa wala kupata haki
 
Hivi lissu wakimfikisha mahakama na akaamua kukaa kimya tu mwanzo mwisho nini kitatokea!?
 
Maana yake kesi haitaoneshwa tena, wala haitakuwa na waangaliaji tofauti na yeye na mawakili zake.
Hapo ni Mahakama ya Rufaa tu ili hili swala lifutiliwe mbali maana wataumiza watu wengi kwa hizo kanuni.

Masaju kabariki hilo swala na Usabato wake
Lissu alishasema hili hawezi kulikubali,yupo tayari kukaa ndani zaidi ili akate rufaa,huu ujinga ukipita inamaana watu watahukumiwa na Mashahidi 'mahurani' ambao hujawahi hata kuwaona
 
Back
Top Bottom