GE2025 Mahakama yaamuru mashahidi kesi ya Tundu Lissu walindwe

GE2025 Mahakama yaamuru mashahidi kesi ya Tundu Lissu walindwe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Tatizo ndugu zangu mnashindwa kutambua kua sheria inaruhusu ushahidi au shahidi asionekane. Ilo sio kinyume na sheria

..Ni kweli kuna sheria ya kulinda mashahidi.

..Je, ni sahihi kwa utaratibu huo kutumika katika kesi dhidi ya Tundu Lissu?

..Ndio maana tukakumbusha kwamba ktk kesi ya uhaini ya mwaka 1984 kulikuwa na mashahidi wengi lakini waliolindwa ni wawili tu, shahidi X, na shahidi Y, ambao walikuwa wakuu wa idara ya usalama.

..Je, kwa kuzingatia mashahidi, na nature ya ushahidi, ktk shauri dhidi ya Tundu Lissu kuna uhalali wa mahakama kutumia sheria ya kulinda mashahidi.
 
Wakati mwingine mashahidi wa siri wataweza kufanya watu waanze kutafuta mchawi na hivyo kulaumiana bila sababu.

Amandla...

..inawezekana sheria imetungwa kwa nia nzuri kulinda faragha za watoto au wanawake waliodhalilishwa wakati wakitoa ushahidi, sasa Dpp anataka kuitumia kukandamiza wanaharakati.

..Nimesikia hata katika kesi dhidi ya Boni Yai Dpp anataka " kulinda " mashahidi. Sasa katika kesi hiyo inadaiwa Mahakama imekataa ombi hilo la Dpp.

..Pia unaweza kuwa mtego kwa Tundu Lissu. Wanategemea katika kupinga mashahidi wa kificho anaweza kutenda kosa ambalo ni la wazi hivyo mahakama imkute na hatia.
 
Mahakama Kuu imeamuru mashahidi ambao ni raia wanaotarajiwa kutoa ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, walindwe kwa maana ya kutoa ushahidi wao kwa kificho (bila kuonekana), majina yao kutokutajwa mahakamani wala taarifa zao zinazoweza kuwafanya wakatambulika, wao, familia zao, marafiki zao na watu wengine wa karibu yao.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu, Agosti 4, 2025 na Jaji Hussein Mtembwa kufuatilia maombi yaliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mshitaka (DPP), imezuia pia taarifa zao kusambaza, kuchapisha na kutangazwa na chombo chochote cha habari, bila ridhaa ya Mahakama.

Lissu, ambaye anakabiliwa na kesi ya uhaini alikamatwa Aprili 9, 2025 akiwa kwenye mkutano wa CHADEMA huko Mbinga kisha kusafirishwa hadi Dar es Salaam na baadaye kupandishwa kizimbani Aprili 10, 2025.

Chanzo: Mwananchi
Walindwe dhidi ya nani 🏃🏃🏃 huku ni kujitia dole na kulinusa.... Upumbafu mtupu wacheni kuchezea Kodi zetu

Muwaweke wazi huku street tuwanyonye vijambio
 
HIi ni video baada ya Joseph Mobutu kupinduliwa akiwa mbio mbio kuwahi airport kupanda ndege ili akimbilie uhamishoni alipohaidiwa hifadhi ya ukimbizi wa kisiasa.

Kutoka mtu aliyekuwa akiogopwa kwa ukatili wa kutesa wapinzani na kuwaua wakosoaji wake aliondoka katika nchi yake aliyozaliwa kama kibaka.

Hata alipokufa haikupatikana nafasi ya mwili wake kurudishwa na kuzikwa ardhi ya nyumbano badala yake ikamuuliwa azikwe uhamishoni Morocco.

Madikteta na historia zao zinajirudia maana ilianza kwa Mobutu , Idd Amin na sasa kuna atakayefuatia kufunfua kurasa mpya za kihistoria.

View: https://youtu.be/Cb44jYhfYe4?si=L_BaZRIjDMe7rx49
 
Mahakama Kuu imeamuru mashahidi ambao ni raia wanaotarajiwa kutoa ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, walindwe kwa maana ya kutoa ushahidi wao kwa kificho (bila kuonekana), majina yao kutokutajwa mahakamani wala taarifa zao zinazoweza kuwafanya wakatambulika, wao, familia zao, marafiki zao na watu wengine wa karibu yao.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu, Agosti 4, 2025 na Jaji Hussein Mtembwa kufuatilia maombi yaliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mshitaka (DPP), imezuia pia taarifa zao kusambaza, kuchapisha na kutangazwa na chombo chochote cha habari, bila ridhaa ya Mahakama.

Lissu, ambaye anakabiliwa na kesi ya uhaini alikamatwa Aprili 9, 2025 akiwa kwenye mkutano wa CHADEMA huko Mbinga kisha kusafirishwa hadi Dar es Salaam na baadaye kupandishwa kizimbani Aprili 10, 2025.

Chanzo: Mwananchi
Wala hakuna chochote wana nunua muda tu
 
Nchi inaenda kuwa ya Kusadikika
Dunia inaenda kupata kiroja Cha Karne

Haya yanayoendelea yanatisha
 
Niliandika hivyo, kuwa Lissu hasipoteze muda kwenda mahakama ya rufani akubali mashahidi wa Siri wakishamaliza kubwabwaja hasiwaulze chochote means no cross examination,hii itafanya kesi iende chap, na tuone hio hukumu.
Itakua huku ya aina gani
 
Kikubwa kesi itoke mahakama hakimu mkazi iende mahakama kuu ,rufaa zikatwe
 
Kwa technologia ilipo watajulikana tu, labda wageuke mabubu. Tayari wameshatambua kutoa tu ushahidi wa uongo dhidi ya lisu unakuwa Adui wa taifa.
Wanasema ni yule aliyemtupa nje wakati wa Kinyanganyilo na wengine maisha aya buana.Mimi kama mshauri wa Mama amteme tu Lissu maisha ni Fumbo kubwa Sana
 
Mahakama gani hii sasa kangaroo court kule the Hague kina Charles Taylor na Slobodan milesevic mashahidi dhidi yao hawakufichwa sura
 
Back
Top Bottom