white wizard
JF-Expert Member
- May 18, 2011
- 8,316
- 13,282
Sasa mkuu mbona unakuwa kama huelewi hata unachokitetea?!!Michezo ni suala la Muungano?
Kwanini Zanzibar wana chama chao na ni wanachama wa CAF?
Kuna mtu wa bara anaweza kwenda kugombea ZFA?
Kwanini wasipiganie kupata uanachama wa FIFA?
Zbr ina timu ambayo inashiriki kombe la mataifa ya Afrika?, je ina timu ambayo inashiriki michezo ya kombe la dunia?kwanini inapofikia hapo huwa ni timu ya Tz, ndio inawajumuisha wao?kwanini pesa zinazotoka CAF/FIFA, zbr wana mgao wao kutoka TFF?
Ina maana hadi hapo hujaona kuwa mzanzibar ana haki ya kulalamika juu ya TFF, lakini Mtanganyika hana haki juu ya ZFA?!!sasa watapigania vipi kupata uanachama wa FIFA, wakati sifa hiyo hawana kutokana na muundo wa muungano huu, wa kuwa zbr sio nchi?!!