Msemaji wa Yanga Haji Manara aufyata, amuomba radhi Rais wa TFF Wallace Karia

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Msemaji wa Yanga Haji Manara ameufya kwa kuamua kujishusha baada ya kumuomba radhi Rais wa TFF Wallace Karia kuhusu jambo ambalo lilitokea Jijini Arusha wakati wa fainali la Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup ASFC, baina ya Yanga SC na Coastal Union.

"Jana mimi na rafiki yangu Heris Said alinisindikiza kwenda kumuona Rais wa Shirikisho la Soka Nchini Tanzania Wallace Karia, na tuliongea kwa furaha sana na kuzungumza mambo ya msingi zaidi nyumbani kwake.

"Kiukweli jambo la Arusha tukio zima halikua na matusi, hilo nataka iwe Very Clear, ambalo watu wengi wananishtumu nalo na waling'ang'ania hapo hapo.

"Ndo maana nilisema pale Airport, kuwa atakayepata tukio lile likiwa na matusi nitajiuzulu kwa kuwa nitakuwa kinyume na hata maadili ya kitanzania na wala si football peke yake.

"Kwa namna yoyote ile naomba msamaha, nilikosea kujibizana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Tanzania Wallace Karia, naomba radhi, na haimaanishi mimi nisichukuliwe hatua.

Kama itaonekana nastahili kuchukuliwa hatua nipo tayari kupokea adhabu hiyo, lakini lazima niombe msamaha bila kujali kamati itaamua nini.

Kingine sina matatizo na Karia, ni Mzee wangu na namheshimu, na nimekuwa mstari wa mbele mara kadhaa kutetea hoja zake.

Naomba radhi, mimi ni mwanadamu na binadamu yoyote yule hukosea, ila kwa kuwa Rais amenizidi kwa vitu vingi sana, sina budi kuheshimu na kuomba radhi kubwa kwake, amenizidi umri na mambo mengi ambayo itakuwa si uungwana kuliacha jambo hili."

Amezungumza Haji Manara kwenye mkutano wake na waandishi wa vyombo vya habari, kufuatia kadhia yake na Rais wa TFF Wallace Karia.
 
Binafsi kama shabiki wa Yanga SC ninashikuru kuwa ameomba msamaha ili aendelee kuwapo kwa lengo la KUKINUKISHA ZAIDI.
 
Kuomba msamaha ni Jambo la hekima

Viongozi wa Yanga SC wana akili sana.

Wameshaufahamu uongozi wa Msomali Karie unachotaka. Si kingine bali ninkuidhoofisha Yanga SC wakidhani wanaikomoa.

Wakamshauri akaombe msamaha wakijua wazi msamaha utaondoa adhani ya kufungiwa na kubakisha adhabu ya faini.

Ambayo hata iyo faini inaweza kusamehewa pia.
 
Wameshaufahamu uongozi wa Msomali Karie unachotaka. Si kingine bali ninkuidhoofisha Yanga SC wakidhani wanaikomoa.
Wangelitaka hilo Safari yenu ya kutwaa ubingwa ingewashinda mapema.
 
Manara kamuomba msamaha Karia personally, sio kamati ya maadili, ndio maana mbele amesema yupo tayari kwa adhabu yoyote, coz anajua Karia sio kamati ya maadili.

Naona ameshtuliwa mapema ndio bahati yake, Karia akiwa sawa na mzazi wake hakutakiwa kujibizana nae kwa namna ile.

Sasa kinachobaki ni kushushwa wenge la usemaji alilonalo, wenge linalomfanya asijue kutofautisha kati ya mzazi, kiongozi, na shabiki, wenge hilo anaenda kushushwa na kamati ya maadili.

Miaka kama mitatu hivi asijihusishe na football naamini itamtosha kujifunza adabu.
 
Haji mjanja sana, uyu atazidi kusumbua sana anajua kucheza na akili za watu.

Kawapamba wahandishi wa habari.

Kampamba Karia alafu anaskilizia.
 
Msaka tonge mwingine. Njia ya chooni ni hatare kuota magugu.
Chezea nzara (lingala)
 
Video haikuwa na sound lakini body language ya manara ilionesha hatoi mameno politely

Kujinasibu mbele ya camera kuwa hakutoa maneno ya kashfa kwa Karia na kwa watu waliokuwepo karibu na tukio siku hiyo ni rudeness.

Msamaha umeombwa kisela au tunaweza kusema msamha umeombwa kwa namna isiyo ya kibusara, ameonesha sio mkosaji na anasingiziwa ila kwa kua ametaka kuwaamisha watu yeye ni muungwana kakubali unyonge kafunika kombe mwanaharamu apite.

Thisi is wrong move, huwezi ukaomba msamaha ukiwa na dhana ya kinyonge kuonesha unaonewa na umekubali kukiri kosa kwasababu ya kuogopa nguvu ya mamlaka.
 
Kuomba msamaha kwa Haji Manara sio taarifa njema kwa WANAO MCHUKIA
Wanaomchukia kama nani?

Halafu msamaha wenyewe umeombwa kwa shinikizo, inaonekana uongozi wa Yanga ndio umemshauri aje aombe radhi

So busara yake hapo iko wapi?

Huyu mtu bado anasimamia msimamo wake, huo msamaha ni takwa la club kulinda maslahi yake lakini mimi na wewe wote tunajua Manara asingeweza kuthubutu kwa willing yake kuomba radhi
 
ROPO ROPO.
alipokuwa Simba alikuwa hivyo hivyo leo yupo utopolo yupo hivyo hivyo.ndo kusema ana uchungu Sana na timu
 
Adhabu yake iko pale pale hata afanyeje.

Unajua ndo maana wanaume huwa tunakufa mapema kutokana na kuwa wabishi ili uonekane kwa watu kuwa wewe ni mbabe lakin kama siku hyo angeamua kuondoka kimya tu kusingekuwa na shida yoyote lakin alisubiri mpaka watu wenye akili waje wamuondoe hapo na kumtuliza
 
Back
Top Bottom