Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
23,606
2,000
Na jaji aliemhukumu Sabaya alitumika kumsaidia nani?
Sabaya kitendo cha kutamka kuwa alitumwa na mamlaka ya uteuzi, maana yake unyang'anyi aliutenda isipokuwa tu alitumwa kuutenda! Kutumwa hakuondoi kuwa alitenda, SEMA ILITAKIWA NA ALIYEMTUMA NAYE ALE MVUA KAMA ZA SABAYA. Nyerere alishawahi sema mtoa rushwa na mla rushwa wote manji ga nyanja.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
15,202
2,000
Matumaini ya kuwa mahakamani ndiko kuliko mahali pa kukimbilia panapo dhuluma, yalizimika kikamilifu jana.

Hazipo shamra shamra, pongezi wala amsha amsha kokote kuonyesha pana haki imepatikana mahali, bali ni malalamiko na manung'uniko ya kilichotokea.

Tangu lini haki ikajificha?

Ikumbukwe shauri hili limekuwa likifuatiliwa kwa karibu na wengi japo hata kwa taabu mno.

Itoshe kusema jana ilikuwa siku mbaya sana kwa wapenda haki wote nchini.

Jana ilikuwa siku mbaya sana kwa Adamoo. Kumbe kipigo alichokipata kinyume cha utu kutoka kwa watesi wake kilikuwa ni halali yake.

Jana ilikuwa siku mbaya sana kwa Mohamed Ling'wenya, kwamba kumbe kweli duniani hakuna haki.

Matumaini ya haki yaliyochipuka upya yamezimwa ghafla.

Jana ilikuwa siku mbaya sana kwa mke wake Adamoo ajuaye sasa kuwa mahakama imebariki kuteswa kwa mumewe.

Kwani Adamoo kitu gani kulinganisha na maslahi binafsi?

Kwani haki ya Moses Lijenje ina nini kulinganisha na maslahi binafsi?

Kweli mkono mtupu haulambwi.

Mambo kama haya yanakera.

Ila haki inapokosekana mahakamani si jambo la kupuuzia.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
15,202
2,000
Hakuna mahakama hapo hilo ni shina la CCM

Kudhani ni CCM inaweza kuwa kupoteza shabaha.

Alisema Chakubanga nchi imetekwa nyara.

IMG_20210911_000004_180.jpg


Mtu nyuma ya usukani ndiyo mtu wetu anajua Moses Lijenje alipo.
 

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
6,015
2,000
Wamekubali bana yaisheee...!

Ndio bwana lepo lepo

Tuambie makosa ya wazi ya Mbowe wapi alilipua kituo cha mafuta na wapi amefanya ugaidi? makosa ya Sabaya hata dingi yako anayajua vizuri

Kesi ya SABAYA haki ilitendeka:

Sabaya: Haki Imetendeka na kuonekana ikitendeka

Kesi ya SABAYA haki haikujificha.

Kesi ya SABAYA manung'uniko yako wapi?

Kesi ya SABAYA ndiyo kihalalishi cha hukumu yoyote hata kama ni batili?

Hii ni akili? Au matope?
Hvyo hvyo Kwa Bwana Mbowe haki itatendeka na ushahidi utawekwa wazi madam kesi inaendelea kusikilizwa...!! Hata hvyo inafkrisha Sana kumfunga miaka 30 mtu aliyekuwa anapambana na Gaidi
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
15,202
2,000
Hawa watu tumalizane nao kwa nguvu za giza

Nguvu za giza hailipi hawa ni wa nguvu za nuruni.

Lazima tukubali kufa, kujeruhiwa, na kuyajaza magereza yao kwa raha zetu.

Hawa siyo CCM. Hawa ni wateka nyara tu. Wahalifu kama wengine.
 

Gerad2008

JF-Expert Member
Jun 9, 2009
580
500
Kwa Sabaya mahakama ilitenda haki?
Watu wote waliodhulumiwa na sabaya wangeitwa kutoa ushahidi angehukumiwa kunyongwa. Kesi ya sabaya na Mbowe ni vitu viwili tofauti. sabaya alishtakiwa kutokana na malalamiko ya wananchi ila mbowe kashtakiwa na serikali na mashahidi wanaosema mbowe ni gaidi ni polisi na siyo raia. Mashahidi wengi waliokuwa wnatoa against Sabaya ni wananchi waliodhulumiwa. mbowe kamdhulumu nani? hajakutwa hata na kisu wala bomu; ni gaidi gani wa namna hiyo?
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
15,202
2,000
Hvyo hvyo Kwa Bwana Mbowe haki itatendeka na ushahidi utawekwa wazi madam kesi inaendelea kusikilizwa...!! Hata hvyo inafkrisha Sana kumfunga miaka 30 mtu aliyekuwa anapambana na Gaidi

Haki huonekana ikitendeka. Haki haiji kama mvua.
 

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
9,261
2,000
Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, leo Jumatano Oktoba 20, 2021 inatarajiwa kutoa uamuzi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Uamuzi huo ambao utatolewa na Jaji Mustapha Siyani (Jaji Kiongozi kwa sasa) unaweza kuwa picha ya mwelekeo wa kesi nyingine ndogo ndani ya hiyo kesi.

Kesi hiyo ndogo inahusiana na uhalali wa maelezo ya mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Adamu Hassan Kasekwa, ambayo mawakili wa utetezi waliyapinga yasipokewe kama kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka.

Upande wa utetezi uliyapinga ukidai kuwa yametolewa nje ya muda wa kisheria na kwamba mshtakiwa huyo hakuyatoa kwa ridhaa yake bali kabla na wakati wa kuchukuliwa maelezo hayo alitishiwa na kuteswa.

Ikiwa mahakama itakubaliana na hoja za upande wa mashtaka, basi itayapokea maelezo hayo na kuwa kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka.

Kupokewa kwa maelezo kutamaanisha kwamba mshtakiwa huyo amekiri makosa na hivyo mahakama itaweza kuyatumia maelezo yake hayo kumtia hatiani na kwa kuzingatia ushahidi mwingine wa upande wa mashtaka.

Lakini kama mahakama itakubaliana na hoja zote za utetezi au mojawapo kati ya hizo mbili, kuwa maelezo yalichukuliwa nje ya muda au kwamba mshtakiwa aliteswa kabla na wakati wa kutoa maelezo, basi itayatupilia mbali maelezo hayo.


=========

UPDATES;

=========

Tayari baadhi ya wanachama na viongozi mbalimbali wa Chadema pamoja na Wawakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa wamewasili .

Ukumbi wa mahamama umejaa wengine wamekaa kusubiri hatma ya uamuzi mdogo wa kesi ya msingi namba 16/2021.
Wananchi wakiwaombea watuhumiwa akiwepo Freeman Mbowe walipowalisi katika viunga vya mahakama asubuhi hii.

Mawakili wa pande zote mbili wameshaingia mahakamanu na kukaa kwenye sehemu zao.

Mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani na Mwakilishi wa Ubalozi wa Sweden wakiwa katika ukumbi wa mahakama kusubiri uamuzi wa kesi ndogo ya kesi ya msingi namba 16/2021 inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Muda huu washitakiwa wameingia katika ukumbi wa mahakama tayari kusikiliza uamuzi wa mahakama katika shauri dogo la kesi ya msingi namba 16/2021.

Jaji anaingia

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 inatajwa

Robert Kidando anawatambulisha mawakili upande wa serikali.

1. Robert Kidando
2. Nassoro Katuga
3. Ignas Mwanuka
4. Esther Martin
5. Tulumanywa Majigo

Peter Kibatala anawatambulisha pia wenzie

Gaston Garubindi
Seleman Matauka
Idd Msawanga
Michael Mwangasa
Dickson Matata
Maria Mushi
Evaresta Kisanga
Allex Massaba
Jonathan Mndeme
Fredrick Kiwhero
John Malya

Jaji: Wakili wa Serikali

Robert Kidando: Shauri limekuja kwa ajili ya uamuzi tupo tayari Mheshimiwa jaji.

Jaji: Utetezi

Peter Kibatala: tupo tayari Mheshimiwa Jaji Kiongozi.

Kimya kidogo

Bado Kimya kidogo

Jaji anachana Bahasha

Jaji: Sasa nitajaribu kusoma kadri nitakavyoweza ufupisho wa yale yaliyosemwa hapa Mahakamani kwa upande wangu ambayo ni umuhimu kama ufupisho. Na utakuwa ndiyo uamuzi wangu.

Jaji: Wakati anatoa Ushahidi Upande wa Simu Shahidi Kingai, alitoa Ushahidi kuwa Adam Kasekwa alikamatwa tarehe 05 Mwezi wa 08 Mwaka 2020.

Jaji: Kwa mujibu wa Ushahidi wake baada ya kuwakamata aliwachukua kwenda kuwasaidia kumtafuta Moses Lijenje.

Jaji: Na baada ya hapo all msafisha Kuja Central Dar es Salaam

jaji: Kwa maelezo hayo ACP kingai aliomba Maelezo ya onyo yapokelewe kama Sehemu ya Ushahidi.

Jji: Ombi lake lilipingwa na Upande wa Utetezi.

Jaji: Sababu ya Pingamizi

Jjai: Maelezo hayo yamechukukiwa kinyume na Muda wa Sheria know nyume na Sheria inayoongoza Mwenendo wa a Makosa ya Jinai kifungu namba 5 na 52.

Jaji: Na Sababu ya pili kwamba Adam aliteswa wakati anatoa Maelezo hayo.

Jaji: Mawakili wa pande zote mbili waliona kuna umuhimu wa Kisheria fanya shauri dogo

Jaji: Mawakili wa pande zote mbili waliona kuna umuhimu wa Kisheria fanya shauri dogo

Jjai: Kusikiliza shauri hili dogo

jaji: Mimi nakubaliana nao

jaji: Know kila Upande ulikuwa na Mashahidi Watatu

Jaji: Sikusudii Kurudia Kusema kila kitu ambacho Mashahidi walisema.

jaji: Isipokuwa nitapitia yale ambayo nitarejea wakati wa uamuzi.

jaji: Upande wa Jamhuri kwamba Adam Kasekwa ni kweli hakuweza kuhojiwa ndani ya masaa Manne kwa sababu Upelelezi wao ulikuwa haujakamilika.

jaji: ACP kingai na Mahita wakati wamepewa taarifa mpango wao ulikuwa kuwa ni kuwakamata watu watatu.

jaji: Licha ya hivyo hawakumkamata Moses Lijenje

Jaji: Kwa Mujibu wa Kingai ni kwamba Adam akijitolea kwenda kumtafuta Moses Lijenje sehemu mbalimbali kama Majengo, Boma Ng'ombe na Sehemu zingine bila Mafanikio. Wakarudi Central Moshi.

jaji: Kwa Mujibu huo Siku ya tarehe 06 pia Juhudi za kumtafuta Moses Lijenje zilindeleaa. Wakaenda Mpaka Arusha Maeneo ya Sakina kwa Dada yake Moses Lijenje.

jaji: Ambao tarehe 06 amri ikatolewa kuwasafirisha kwenda Dar es Salaam.

Jaji: KINGAI NA MAHITA wote wanakubali kuwa walisafiri kuja Dar es Salaam Na wakakabidhiwa kwa Msemwa.

jaji: Kingai anasema baada ya kufahamishwa haki zake Kisheria aliojiwa Siku hiyo hiyo.

jaji: Adam Kasekwa alikamatwa na kukanusha kuwaongoza Polisi wale waliomkamata kwenda maeneo kadhaa Mji wa Moshi na Arusha.

jaji: Alikanusha pia hakupelekwa Central Dar es Salaam Bali Kituo cha polisi Tazara.

jaji: Ushahidi wa Adam Kasekwa unaonyesha alipofika Dar es Salaam Siku ya Tarehe 07 Mwezi wa O8 alipelekwa Tazara na Mbweni na Siku ya tarehe 09 alitishwa ili kuweka sahihi.

jaji: Ilishabihishwa pia kupitia Shahidi wa Pili Mohamed Ling'wenya.

jaji: Kwa Mujibu wa Moses Ling'wenya alisikia walipokuwa Moshi akilia kwa Sauti ya zege.

jaji: Lilian pia kama Shahidi wa tatu ambaye ni Mke wa Adam Kasekwa alithibitisha kuwa alimuona Adam Kasekwa kuwa kateswa na kwa kuthibisha kwa makovu. ...Na alivyokuwa anatembea

jaji: Hivyo baada ya kupitia pia mawasilisho yao ya pande zote, nawashukuru sana.

jaji: Kwa Upande wa Jamhuri wao walisisitiza kuwa Maelezo yalichukuliwa kwa Mujibu wa sheria kwamba Kifungu cha 50(2) unaondoa Muda huo katika Hesabu za Masaa Manne toka awekwe Chini ya Ulinzi

jaji: Hivyo kwa Mujibu Wa Robert Kidando Muda uliotumika KusafiriSha watuhumiwa haupaswi kuwa sehemu ya Masaa Manne.

jaji: Kuhusiana na Shauri hili sasa Upande wa Jamhuri wanakiri kuwa walikuwa na Adam kasekwa.

jaji: Upande wa Jamhuri sasa wameniletea Kesi Mbalimbali kwa ajili kufanya Rejea

jaji: Kuhusiana na Uamuzi sasa kwanini Adam Kasekwa amekamatiwa Moshi na Kuja kuhojiwa Dar es Salaam.

jaji: Kwa Mujibu wa Robert Kidando sasa anasema ni sababu ya Uzito wa tuhuma, kuzingatia pia Makosa yalitakiwa kufanyika sehemu mbali mbali

jaji: Kuhusu Pingamizi la pili kuhusiana Adamoo kulalamika kwamba Ameteswa

jaji: Wakili wa Serikali amesema Maelezo hayo yaliandikwa Siku ya tarehe 07 Mwezi wa 08? Na Kwamba Upande wa Utetezi wameshindwa Kuibua shaka.

jaji: Upande wa Utetezi umeshindwa Kuwahoji Mashahidi wa Jamhuri

jaji: Maelezo ya Adam Kasekwa ni kwamba Japo alitoa Maelezo lakini hakutoa kwa ridhaa yake.

jaji: Kuhusiana na Ushahidi wake hauonyeshi kuwa alitoa Maelezo au Kuteswa akiwa Central Police Dar es Salaam.

jaji: Kwa hiyo kwa Upande wa Serikali ni kwamba Ushahidi uliachana na Pingamizi
Badala yake ukawa ni wakufikirika

jaji: wakanirejesha kwenye kesi ya Rugemalila VS Jamuhuri

jaji: Kwamba Kingai hakuhojiwa kwa Mateso aliyopewa Adamu Kasekwa akiwa Moshi.

jaji: hakuhojiwa pia kuhusiana na Maelezo aliyoyachukua Dar es Salaam

jaji: Kwa Mujibu wa Robert Kidando akaeleza athari za kutokuhoji Mambo ya msingi.

jaji: Pia amezungumzia kukinzana kwa Maelezo ya Ushahidi kati ya Adam Kasekwa na Mohammed Ling'wenya

Kuhusiana na Upande wa Utetezi Mawasilisho yaliandikwa na John Malya

jaji: Kwamba Maelezo yalichukuliwa Siku ya tarehe 07 ambapo Masaa Manne yalikuwa yameshapita

Kuhusiana na Mazingira yaliyowekwa na Sheria kifungu cha 50 kwamba Mahakama inapaswa kingatia Masaa Manne na kuyaondoa yale ya kusafirisha Watuhumiwa

jaji: Moshi palikuwa na Nyenzo zote ambazo zingeweza kuwezeha Maelezo kuchukuliwa

Kuhusiana na Mateso, Wakili Malya anasema Mateso siyo lazima yawe ya kimwili, Bali Fikra na utu.

Au Mateso yanayotweza Utu wa Mtu

jaji: wakili mallya akaturejesha Kwenye katiba pia

Na Pia akaturejesha Kwenye Tamko la Umoja wa Mataifa linalozingatia Mateso na Utu wa Mwanadamu.

Wakili Malya ametutaka Mahakama tuzingatie Nyaraka hizo.

jaji: wakili mallya ametupa kesi za Marejesho

jaji: Kutokana Nyaraka hizo alizowasilisha Wakili Malya, Amesema ingawa hapakuwa na Ushahidi wa kitabibu Lakini ametutaka tuzingatie Ushahidi wa kimazingira.

jaji: ametutaka tuzingatie Ushahidi wa kimazingira

1. kuchelewa kuandika Maelezo yake
2. kuchelewa kumsafirisha
3. kuchelewa mfikisha Mahakamani
4. Ushahidi wa Lilian Kibonqla Mke wa Adam Kasekwa Kushindwa Kumuona Mme wake pamoja na Juhudi zote alizozifanya.

jaji: Zoezi Zima la ukamataji halikuzingatia Utaratibu wa kisheria kama PGO

Na Kwamba Ushahidi au Maelezo ambayo hayajazingatia Sheria hayapaswi Kuchukuliwa Mahakamani

jaji: Kwamba kwa Mujibu wa Jamuhuri wameshindwa kuthibitisha kwamba Adam Kasekwa alihojiwa kwa kuzingatia sheria

Kwa hiyo nimejaribu kwa ufupi kupitia yale yaliyosemwa mahakamani.

jaji: baada ya Mimi kupitia Ushaidi uliowasilishwa Mhakamani na Mawasilisho

Nitaanza na hoja ya kwanza kwamba Maelezo yaliandikwa nje ya Muda wa Kisheria.

jaji: Miye na kubaliana kuwa Muda ambao Mtu anapaswa kuanza Kuchukuliwa ni Masaa Manne

jaji: EXCEPTION pekee ipo Maeneo Mawili kifungu 51 pale ambao Muda wa Masaa umeongezwa.

jaji: Unawakumbuka kuongezwa na Askari polisi Mkuu wa Upelelezi au Kwa kuleta Maombi Mahakamani.

MASAA MANNE lazima yazingatiwe isipokuwa yale yaliyoelezwa yamezingatiwa, Ukishindwa hivyo Ushahidi huo Haupaswi kupokelewa.

jaji: mimi Narejea kesi ya a Mahakama ya Rufaa kuwa kutokuzingatia Sheria ya kifungu namba 51 katika Kuchukua Maelezo inaathiri Ushahidi huo.

pia Kesi Nyingine katika Mahakama ya Rufani palikuwa na Ucheleweshaji wa kumsafirisha Mtuhumiwa kwa Siku 02.

Kwamba Mahakama ya Rufani ktk Shauri hili walikutana tena na Mazingira kama haya Ya Ucheleweshaji wa Kuchukua Maelezo.

jaji: Sasa Adam Kasekwa alikamatwa tarehe 05 Mwezi 08, 2020 na Maelezo aliandika tarehe 07, 08, 2020 bila shaka hapa kuwa na uthibitisho wowote kwa Upande wa Mashitaka kuwa Masaa Manne yalishapita.

jaji: Hivyo Jambo pekee limebakia kama kuna Exception Ni kweli Wakati Adam Kasekwa anakamatwa palikuwa na Mtu anaitwa Moses Lijenje.

Kwa Mujibu wa Ushahidi Upande wa Jamhuri Mpango ulikuwa ni Kuwakamata watu watatu

Lipo pia kwenye Kumbukumbu za Mahakama

jaji: Kwa Maoni yangu kwa kuwa Adam Kasekwa alikuwa na Moses Lijenje na Mohammed Ling'wenya alikwepo Rau Madukani ni Maoni yangu kuwa Jambo la kuanza Kumtafuta linaleta MANTIKI kwamba palikuwa na Juhudi za kutaka Kujua alikuwa wapi

jaji: Ni vigumu kuondoa dhana kuwa Adam Kasekwa aliwaongoza Kumtafuta Moses Lijenje

Na Pande zote Mbili hawabishani kwamba Adama Kasekwa alisafirishwa kuja Dar Es Salaam.

jaji: Hata Lilian Kibona alitueleza kuwa Alijulishwa kuwa Mme wake alisafirishwa kuja Dar Es Salaam

kwa hiyo kwa Upande wa Jamhuri Ushahidi unaunga Mkono Jambo hili

jaji: Kwa Muda uliotumika kumtafuta Moses Lijenje na Muda uliotumika Kumsafirisha Kuja Dar es Salaam Adam Kasekwa unapaswa kuzingatiwa kuondolewa katika Masaa Manne.

Kwa Upande wangu kwamba Walipaswa Kuombwa Muda wa Nyongeza, kwa Upande wa Askari kama ameanza kumuhoji na akaona Muda wa Masaa Manne hayatotosha.

jaji: Hivyo ni Kwa Maoni yangu ni kwamba Adam Kasekwa alikuwa hajaanza kuhojiwa

Kwa Upande wangu Katika kesi ya Malya Juu ya Albert Mendez ni tofauti na Shauri hili, Kwa sababu kesi ile ilikuwa ni Madawa ya Kulevya.

jaji: Mahakama ilisema hapa kuwa na Sababu ya kusubiri Mshitakiwa atoe zile kete (pipi), katika Shauri hili hakuna Mazingira ya Kusubiri Bali walikuwa wanatembea na Mshitakiwa sehemu Moja kwenda nyingine.

jaji: Kwa Upande wangu naona kuwa Ucheleweshaji katika Shauri hili palikuwa na Sababu, Matakwa ya Sheria yalikuwa yamezingatiwa.

Muda wa Masaa Manne hautojumuishwa kwa sababu za Usafirishaji.

jaji: Hitimisho la Hoja ya kwanza ndiyo hilo

Sasa nageukia Pingamizi la Pili, lina nahusu uhiari Kwamba Adam Kasekwa aliteswa kabla na wakati wa Kuandika Maelezo.

jaji: Kwa Uelewa Wangu, Pingamizi linaonyesha Mshitakiwa alikubali kuwa alitoa Maelezo. Kingai anasema walipofika Dar es Salaam Mshitakiwa alihojiwa Siku hiyo hiyo baada ya Kufika.

jaji: Kwa Mujibu wa Shahidi huyu ni kwamba aliomba Mahakama ipokee Maelezo yaliyochukuliwa Central Police Dar es Salaam, Ilikutibitisha kwamba Mshitakiwa alitoa Maelezo katika Central Police Dar es Salaam.

jaji: Mahita na Msemwa hawakushuhudia wakati Adam Kasekwa anatoa Maelezo Na Msemwa alitoa Detention Register kwamba Adam Kasekwa alikuwa amepokelewa Central Police Dar es Salaam Siku hiyo hiyo

jaji: Alitolewa Saa 12 Kasorobo na akarudishwa Siku hiyo hiyo saa 3 Hapa kuwa na Pingamizi kwamba Mahakama isipokee Kielelezo hicho Kutokipinga inaonyesha kwamba hupingi kilichopo ndani ya Kitabu hicho.

jaji: Maelezo ya Adam Kasekwa kwamba aliteswa na Kuchukuliwa Maelezo Mbweni Ushahidi unakinzana na madai yake ACP Kingai alidai kuwa Maelezo yalichukuliwa Central Police Dar es Salaam Upande wa Utetezi ulitarajiwa kuweka Pingamizi kuwa Adam Kasekwa hajawahi Kufika Central Police

jaji: Kwa kukubali kuwa alitoa maelezo lakini kwa Mateso anakubaliana kuwa ametoa Maelezo akiwa Central Police Dar es Salaam, Na Kama Mshitakiwa hakufikishwa katika kituo cha Polisi cha Kati cha Dar es Salaam.

jaji: Kwa hiyo kwa hitimisho langu Naona Mapingamizi yote Mawili yamekosa Mashiko Kwamba Maelezo yalichukuliwa ndani ya Masaa Manne Kwa Ushahidi, Upande wa Utetezi walioutoa Na pia Maelezo yalitolewa na Mshitakiwa wa Pili kwa ridhaa yake.

jaji Kiongozi: Wakili wa Serikali Wakili wa Serikali: Naomba utoe Amri turejee katika Shauri la Msingi Jaji Kiongozi: Upande wa Utetezi? Peter Kibatala: Hatuna Pingamizi Mheshimiwa Jaji Kiongozi

Jaji Kiongozi: Sasa Kwa kuzingatia Maelezo yaliyowekewa Pingamizi nayapokea sasa Maelezo haya Kama Ushahidi, SASA tuta Break kidogo nifanye Consultation na Mawakili wa pande zote kisha tutarejea tena JAJI KIONGOZI ananyanyuka anatoka Nje

Mahakama bado haijarejea Usishangae akajitoa kuendelea na shauri hili.

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 inatajwa

Wakili wa Serikali: Upande Jamuhuri tupo Kama Mwanzo Jaji Kiongozi: Utetezi..? Peter Kibatala: na sisi tupo sawa

Jaji Kiongozi: ni sawa tunapaswa Kunaendele na Shahidi Lakini nikaomba nishauriane na Mawakili. Sasa Nimeona kwamba Shauri hili ni Moja ya Shauri linalopaswa kuisha kwa haraka.

jaji: Kama Shauri likienda mfululizo ingechukua Miezi kama Minne jaji: Hivyo kwa Majukumu niliyonayo nimeona nijitoe aje Jaji mwingine haraka iwezekanavyo. Jaji ananyanyuka anaondoka Zake
Kwa hitimisho hili ina maana kesi inarudi lini tena mahakamani?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom