WanaJF, Takwimu hazidanganyi kwa wale waliosoma takwimu za kimataifa ni dhahiri tupo uchumi wa kati.
Kampeni za CCM zimepelekea maelfu ya wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara kujaza viwanja na kufurika.
Wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania sasa wanapatiwa elimu bora kuliko wakati wowote ule tangu uhuru wa Taifa hili, wanafunzi hawa wanaajirika na kukubalika kimataifa.
Leo hii wafanyakazi wa serikali na wale wa sekta binafsi wamepunguziwa kodi kwa asilimia kubwa sana kuanzia mwezi July 2020. Punguzo la kodi limeongeza uwezo wa jamii kuuza na kununua.
Upande wa wafanyabiashara kodi zimekuwa rafiki zaidi ukilinganisha na miaka mitano kabla ya JPM, Wafanyabiashara wanaruhusiwa kulipa kodi kwa majadiliano na Mamlaka ya mapato TRA.
Aidha, Maelfu ya wanafunzi wameajiliwa serikalini kuanzia mwaka 2014. Sekta ya afya zaidi ya madaktari mia sita wameajiriwa,Karibuni zaidi ya ajira elfu kumi na tatu za walimu zimetangazwa.
Kwa upande wa wakulima mambo ni mazuri zaidi, Wakulima wa nafaka na mikunde serikali imeimarisha uhimilivu wa bei hivyo bei kutoyumbishwa na madalali wachache,Hali hii imepelekea wakulima kulima na kuuza kwa wakati,Zao la korosho limeimarika kwa kipindi cha miaka mitano baada ya serikali kuingilia kati watu waliotaka kushusha bei kwa manufaa binafsi,Serikali iliamua kununua korosho zote na kulipa kwa wakati.
Ni furaha,na Upendo kila kona ya nchi hii,Mzunguko wa pesa ni mzuri kwa wajasiriamali walio wengi na hii imepelekea kila mtu kula ,kununua na kufanya atakalo bila kuvunja katiba ya nchi.
Tutashinda kwa mbinu za kisasa zaidi kwa maendeleo ya watanzania wote.
Hoja hujibiwa kwa hoja bali si kwa matusi,Mwenye kupinga alete takwimu zake hapa JF.
Je, hatupo uchumi wa kati?
Je, wanafunzi graduate wa udaktari na ualimu hawajaajiriwa?