Maeneo 38 kukosa huduma ya Maji kwa zaidi ya Saa 36 jijini Dar, kutokana na maboresho ya kuondoa tope kwenye Mtambo wa kuzalisha maji

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetangaza upungufu wa Huduma ya Maji kwa Wateja wanaohudumiwa na mtambo Ruvu Chini, kuanzia Machi 5 hadi Machi 7, 2024

Kwa mujibu wa taarifa ya DAWASA upungufu huo unatokana na maboresho ya msingi yanayofanywa katika mtambo huo

Maeneo yatakayoathirika ni Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Kunduchi, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Madale, Goba, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo Kikuu UDSM, Mwenge, Chuo Kikuu Ardhi na Kijitonyama

Maeneo mengine ni Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang'ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti, Ilala na Katikati ya Jiji.

=====

UPDATES; 06.03.2024

======

MABORESHO RUVU CHINI MBIONI KUKAMILIKA
IMG-20240306-WA0029.jpg

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imesema kuwa kazi ya maboresho ya kuondoa tope kwenye Mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini uliosababisha kupungua uzalishaji kwa asilimia 20 iko mbioni kukamilika.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Ndugu Kiula Kingu ameeleza kupitia vyombo vya habari kuwa uchafu kwenye maji umesababisha tope kwenye machujio ya maji na hivyo kuathiri ubora na usafi wa maji yanayozalishwa kwenda kwa watumiaji.
IMG-20240306-WA0030.jpg

"Tuliona ni vyema kutenga muda wa saa 36 kusafisha machujio ya maji ili kuwezesha kupatikana kwa maji yaliyo masafi na yenye ubora kwa watumiaji, amesema na kuongeza kuwa kazi ya kuondoa tope kwenye chujio kubwa ilianza tangu siku ya Jumanne na inafanyika usiku na mchana," amesema Ndugu Kingu.

"Mpaka sasa kazi imefikia hatua nzuri na leo jumatano zoezi la kuondoa tope itakamilika na kuruhusu baadhi ya pampu kuwashwa na huduma kurejea kwenye hali yake," ameeleza.
IMG-20240306-WA0027.jpg

Ndugu Kingu ameeleza kuwa baada ya kukamilika kwa kazi hii huduma ya maji itaimarika na maji yaliyopungua kwa asilimia yanapatikana kwa usafi.

Ametoa wito kwa wananchi wote wanaoharibu miundombinu ya maji hasa kipindi hiki cha mvua kuacha mara moja kwa kuwa uharibifu unasababisha gharama kubwa kwa Mamlaka ya kusafisha mtambo kila mwezi tofauti na awali ambapo mtambo ulikuwa ukisafishwa kila baada ya miezi sita.
 
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imetoa taarifa kwa Wateja wake na Wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini kuwa, kutakuwa na upungufu wa huduma ya maji kwa baadhi ya maeneo ili kuruhusu maboresho ya msingi katika mtambo leo Jumanne March 5,2024 kuanzia saa 12 jioni hadi Alhamisi March 7,2024.

Maeneo yatakayoathirika na upungufu huu wa huduma ya maji ni Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Kunduchi, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Madale, Goba, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo Kikuu UDSM, Mwenge, Chuo Kikuu Ardhi, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang’ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti, Ilala na Katikati ya Jiji.

“DAWASA inawashauri Wananchi kuhifadhi maji ya kutosha katika kipindi cha matengenezo” ——— imeeleza taarifa ya DAWASA.
 
Hivi huko Dawasco Kuna wafanyakazi wenye ubinadamu kweli? Haya maji ya tope Kama like la udongo mwekundu wa mfinyanzi mliyoyaachia huku Tegeta mkipewa ninyi myatumie mtaweza?

Au ninyi ni mawakala wa magonjwa yatokanayo na maji so, mmasaka wateja?

Kumbukeni kuwa wananchi wamelipia bili za maji safi na salama na siyo matope!

Au nanyi mmejiunga kwenye kundi la kuifelisha serikali ya CCM na Rais wake?

Wizara ya maji na ile ya afya hebu yazuieni hayo maji kabla hayajaleta madhara ya magonjwa ya kuharisha. Mitaa yote ya Tegeta na Kunduchi maji hayafai kabisa kwa matumizi ya viumbehai kwani ni matope Tena Yale mazito Kama yale yaliyotokea kule Hanang! Mtatuua.
 
Back
Top Bottom