Waziri Aweso aigaza DAWASA kuboresha miundombinu ya uzalishaji maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Waziri wa Maji Jumaa Aweso (Mb) ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuhakikisha inafanya maboresho kwenye mitambo ya uzalishaji maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu hususani pampu za kusukuma maji ili kuwezesha huduma ya maji iweze kupatikana kwa ufasaha na kwa wananchi wote.

Mhe. Waziri ametoa maagizo hayo wakati alipotembelea na kukagua hali ya uzalishaji wa maji na upatikanaji wa maji Dar es Salaam na Pwani na kujiridhisha juu ya upatikanaji wa maji ya kutosha kwenye chanzo cha maji ya Mto Ruvu.

Ameongeza kwa kusema ameridhishwa na hali ya upatikanaji wa maji kutoka Mto Ruvu kwa kuwa vyanzo vyote vya Ruvu Juu na Ruvu Chini maji yapo ya kutosha, hivyo kazi kubwa inayohitaji kufanyika ni maboresho ya pampu za kusukuma maji kwenye Mitambo ili huduma iweze kupatikana kama kawaida.
 
AWESO ATOA UHAKIKA WA HUDUMA DAR NA PWANI
IMG-20240307-WA0024.jpg

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuhakikisha inafanya maboresho kwenye mitambo ya uzalishaji maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu hususani pampu za kusukuma maji ili kuwezesha huduma ya maji iweze kupatikana kwa ufasaha na kwa wananchi wote.

Mhe. Waziri ametoa maagizo hayo wakati alipotembelea na kukagua hali ya uzalishaji na upatikanaji huduma ya maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani na kujiridhisha juu ya upatikanaji wa maji ya kutosha kwenye chanzo cha maji Mto Ruvu.
IMG-20240307-WA0030.jpg

Ameongeza kwa kusema ameridhishwa na hali ya upatikanaji wa maji kutoka Mto Ruvu na kuwa mitambo ya maji Ruvu Juu na Ruvu Chini maji yapo ya kutosha, hivyo kazi kubwa inayohitaji kufanyika ni maboresho ya pampu za kusukuma maji kwenye ili huduma iweze kupatikana.
IMG-20240307-WA0026.jpg

"Nipende kuwajulisha wananchi kuwa hakuna shida ya maji kwenye vyanzo vya maji Ruvu Chini na Ruvu Juu, kazi inayofanyika ni kuboresha uzalishaji wa maji hususani mitambo ya kusukuma maji pamoja na kuboresha ufuatiliaji wa maji kwa wananchi," ameeleza Mhe. Waziri.

Wizara ya Maji itaendelea kuwa kipaumbele katika kufuatilia na kuhakikisha huduma inaimarika kwenye maeneo yote Dar es Salaam na Pwani.
IMG-20240307-WA0032.jpg

Amewasihi wananchi kulinda vyanzo vya maji vilivyopo ili kuokoa gharama kubwa inayotumika katika kusafisha na kutibu maji kwenye mitambo ya kuzalisha maji.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Ndugu Kiula Kingu amesema kuwa kazi ya maboresho kwenye mitambo ya kuzalisha maji imekamilika na sasa huduma imeimarika katika eneo la kihuduma kuanzia tangu siku ya jana.
IMG-20240307-WA0025.jpg

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Adam Ngalawa amesema kuwa viongozi wamejionea kazi inayofanyika na wameridhika kwa kuona fedha zinazotolewa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan zimetumika kuboresha huduma ya maji kwa wananchi.

"Tumeona pia uwepo wa maji kwenye vyanzo vya maji na kazi kubwa inayofanywa na DAWASA kuboresha miundombinu ya uzalishaji maji ili huduma ifike kwa wananchi ipasavyo," amesema Mhe. Ngalawa.

Naye Meya wa Kinondoni Mhe. Sengoro Mnyonge ameipongeza DAWASA kwa kazi kubwa inayofanyika ya kupambania upatikanaji wa maji kwa wananchi wote wa Dar es Salaam na maeneo mengine.

Amesema kuwa kupitia ziara hii wamebaini sababu zilizosababisha upungufu wa maji mjini ikiwemo mvua kubwa zilizosababisha uharibifu wa miundombinu ya maji. Hivyo kwa sasa tunaweza kufikisha ujumbe sahihi kwa wananchi kupitia madiwani na wenyeviti wa mitaa kuhusu hali ya upatikanaji wa maji mjini.
 
Karibu DUWASA ujionee mambo yanavyokwenda mrama. Visima tulivyoahidiwa na kuambiwa ukosefu wa maji hapa Jijini itakuwa Historia haijulikani vipo wapi. Mgao wa maji haufuatwi na watu hawapati maji karibu wiki nzima. Kwa hili la maji hakika hakuna cha kujivunia.
 
DAWASA acheni janja janja. Mmechimba visima Kigamboni vinaweza kuzalisha maji mengi sana na kuinywesha nusu ya population ya Dar na Pwani, kwanini mnaangaika na kutoa maji kilometa kadhaa na bado mnatumia gharama kubwa kwenye treatment na non revenue water kibao inapotea kwann msiwekeze nguvu kwenye Kigamboni?

Kwa study zilizofanyika, zaidi ya 54% ya maji ambayo Wami Ruvu wanamuuzia DAWASA yanapotea njiani kama unaccounted for, either kuibiwa, vandalism au leakages. Imagine izo asilimia zinazopotea.

Kwanini issue ya Kigamboni inakua ngumu mnaikumbuka mvua zikigoma tu. Mnakera.
 
Nimekuja kugundua watendaji wanaleta mchezo sana na maisha ya watanzania.

Yaani pampu mpya kununuliwa ni shida..??

Mpaka watu wanakosa huduma???

Jamani kuna huduma nyingine ni za msingi kama maji sio za kuleta siasa.
 
Kati ya mawaziri wanaopiga kazi jumma awesso ni no moja 💪💪💪💪Kuna wengine wanafki tu ,maji ni uhai na papu kununua serikali inashindwa wp shinda ni watu janjajanja nyingi
 
Back
Top Bottom