DAWASA: Changamoto ya Umeme Mdogo imesababisha baadhi ya maeneo ya Dar kukosa Maji, maboresho yanaendelea

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Mamlaka ya Majisafi na Uhifadhi wa Mazingira (DAWASA), imesema inaendelea kufanya maboresho katika maeneo yenye Changamoto ya kukosa Maji katika Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na maeneo ya Segerea.

Taarifa iliyotolewa na Everlasting Lyaro ambaye ni Afisa wa Mamlaka hiyo aliyezungumza na JamiiForums, imesema baada ya maboresho ya miundombinu na matengenezo ya miundombinu ya kusukuma maji kutoka Chanzo Kikuu cha Ruvu Juu pamoja na Kituo cha Kusukuma maji cha Segerea yameendelea kuimarisha huduma katika maeneo mengi ikiwemoo eneo la Kibamba na Tabata Segerea.

Afisa huyo amesema Huduma ya maji katika eneo la Segerea imekuwepo siku ya Februari 18, 2024 na Maeneo yaliyopata huduma ni Segerea Chama, Sanene, Toroka Uje, Segerea Tani Moja ,Segerea kwa Mkuu wa majeshi, Segerea seminary, Segerea Uwanja wa punda, Segerea kwa Makongoro mahanga.

=========

Kwa wiki iliyopita tulipata msukumo mdogo wa maji katika maeneo ya Kinyerezi na Bonyokwa wakati huduma ikiwa imeelekezwa huko.

Ila kuanzia siku ya Jumamosi mpaka Jumapili ya tarehe 18.2.2024 eneo la Segerea yote ilipata maji kwa 98% na tulipita katika Maeneo hayo kwa ajili ya uhakiki.

Pia eneo la Kimanga walipata maji kwa maeneo yote.

Kwa eneo la Kinyerezi ambayo wanatumia pump ya Segerea wanaendelea kupata huduma kwa migao na team zetu zinaendelea kufuatilia migao ili kuhakikisha wateja wote wanapata huduma.

kinachofanyika kwa sasa kuongeza msukumo bonyokwa:

Kwa Bonyokwa pump ya kusukuma imekwisha nunuliwa na tunaendelea na mradi mdogo wa kufunga Booster pump mpya eneo la Mavurunza ili kuongeza msukumo wa maji katika maeneo ya Bonyokwa Stand ,JKT,Macedonia ,Kisiwani Juu na chini pamoja na Mnara wa Voda ,Airtel ,Msikiti wa kijana na sehemu ya kisukuru.


Pia soma DAWASA Mitaa ya Tabata Segerea kuna shida gani, Mbona hatupati Maji wiki ya tatu sasa?
 
Back
Top Bottom