DAWASA: Matengenezo ya Mtambo wa Ruvu Chini yanakamilika leo, Tatizo la Maji litakwisha

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Kiula Kingu amesema matengenezo ya moja ya chujio la kuhifadhia maji katika mtambo wa kuzalisha maji Ruvu chini yatakamilika leo ambapo tatizo la maji lililodumu kwa saa 36 katika baadhi ya maeneo ya Dar es salaam na Pwani litakwisha na Watu watapata maji safi yasiyo na tope.

Akiongea na Waandishi wa Habari, Bagamoyo Mkoani Pwani katika mtambo huo, Kingu amesema ——— > “Hapa tupo kwenye moja ya mitambo mikubwa ya uzalishaji maji Afrika Mashariki ambaol kwa siku unahudumia Watu zaidi ya 75% katika Jiji la Dar es salaam eneo tulipo kuna choteo la maji ambapo yanachukuliwa na kwenda kuchakatwa kwa ajili ya Watumiaji”

“Hali ya Mto kwa sasa maji ni mengi ya kutosha yanatosheleza na mengine yanakwenda baharini lakini maji haya yana rangi kama ya udongo kutokana na uharibifu wa mazingira Mto Ruvu unapoanzia hii inapelekea kujaa kwa matope kwenye sehemu yetu ya kuchujia, tuliomba saa 36 ili kuondoa matope katika machujio yetu ya maji ili yakija mjini yawe ya kujitosheleza na yenye ubora”

Kingu amewataka Wananchi kusafisha matanki yao ya kuhifadhia maji ili waweze kupata maji yaliyo safi na salama kwa afya.
 
Wasirudishe bn waendelee kuyakata hivo hivo naenjoy Sana kukutana na wanachuo kwenye maji ya chumvi
 
saa thelathini na sita zilikua nyingi sana kukosekana kwa maji, hata kama ukubwa wa tatizo ulikuwa wa namna gani lakini waliacha adha kubwa sana.
 
Back
Top Bottom