Hitilafu ya Umeme yawakosesha Maji wakazi wa Dar na Pwani

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia wananchi wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani kuwa kumekuwa na ukosefu wa huduma kutokana na hitilafu katika mfumo wa umeme wa Gridi ya Taifa.

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumamosi Februari 3,2024 na kitengo cha mawasiliano cha mamlaka hiyo.

Imetaja maeneo yanayoathirika ni kwa wanaohudumiwa na mtambo wa Maji Ruvu Juu, Mtambo wa Maji Ruvu Chini, Mtambo wa Maji Wami, Mtambo wa maji Mtoni na Visima vya Maji Kigamboni.

“Mamlaka inategemea kuendelea na uzalishaji maji pindi huduma ya umeme itakaporejea. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza,”amesema sehemu ya taarifa hiyo.

Hata hivyo, wakati mamlaka ikitangaza hilo baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam, wananchi wamelalamika kukosa huduma ya maji kwa zaidi ya siku tatu sasa.
 
Back
Top Bottom