RTI
JF-Expert Member
- Dec 20, 2018
- 2,423
- 7,124
Sure mkuu yaani nchi yetu ina mifumo mibovu kiasi kwamba hata aje nani kuliongoza taifa hili ataliacha kama alivyo likuta.Hapo umeongelea Point sasa! Mjadala unafungwa
Kuwaongoza WTz ina hitaji uwe na moyo mpana sana na uvumilivu wa hali ya juu sana ,tofauti na hapo unaweza kuwauwa wote kwa hasira.
Mfano JK ni mtu mwenye moyo wa kipekee sana kutokana na uvumilivu wake dhidi ya Wtz.
Lakini JPM ambaye hana
huruka ya uvumilivu alijikuta ana kuwa katili kutokana na aina ya watu anao waongoza ,alirazimika kuwa katiri ili kuwajengea hofu watumishi wa uma ili wawajibike lakini haikusaidia maana walikuwa wameshaaza kumzoea na kutoogopa vitisho vyake.
Mfano unakuta mkuu wa wilaya anapokea mshahara lakini majuku anayo takiwa kuyatimiza eti anasubili rais ndo aje kuya shughulikia.
Mfano mdogo ni hili la madawa hili si jukumu la rais kuanza kufatilia eti kwann hakuna madawa hospital, na ndio maana kuna watumishi wa idara ya afya kuanzia ngazi ya taifa mpaka kijiji hawa ndio wana takiwa kufatilia na kudhibiti wizi wa dawa za serikali lakini hawafanyi hivyo na kila mwisho wa mwezi wanaenda kuvuta mshahara hapo utamlaumu rais kwa lipi?
Nchi hii ina matatizo uki yaangalia juu juu unaweza kuona ni ya kawaida lakini ni janga.