Maduka ya Dawa yaliyo nje ya mageti ya Hospitali za Serikali huwa na dawa muda wote lakini ndani ya Hospitali husika hamna dawa

MoseKing

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
2,614
2,000
Sio rahisi kama unavo fikiri, huwezi endesha hospitali kwa cost sharing kwa sababu sera ya misamaa ina sababisha nusu ya mapato ya hospitali kua misamaa tu. Cha msingi ni kuhakikisha kila mtu ana kua na bima. Nchi yetu bado sana hatuna uwezo wa kutoa matibabu bure hata kwa hayo makundi maalamu
Sasa hivi hii sera ya misamaha ni kama imekufa ila kwasababu za kisiasa wanaogopa kuweka wazi kama ilivyotokea kwenye umeme wa Tshn27,000.

Sera inataka wazee, watoto underfives na wajawazito kutibiwa bure ila ukiangalia sasa hivi ni kama serikali inapush hawa watu wote wakate Bima angalau hata za CHF.

Na sasa hivi vituoni ukifika, wanakusoma kwanza, hata kama ni Mzee au umepeleka Mtoto underfive wanaweza kukukazia na ukalipa vile vile.
 
Kelvin X

JF-Expert Member
Jun 28, 2011
1,623

Ndio hivo, hata wakati wa magu. Maana wanasiasa ukiwafata huta endesha kituo. Wana panda majukwaani wana wadanganya kua wazee bure sijui nini... ila ukweli huwezi pata huduma bure
 
Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
7,965
2,000
Maduka ya dawa nje ya hospitali hayajawahi zuiliwa, labda huko kwenu.
Kuna kipindi Magufuli alipiga marufuku ya maduka hayo kuwa ndio chanzo cha dawa Kukosekana Hospitalini kwani ilionekana kuwa madawa hospitalini yanchukuliwa kinyemela na kwenda kuuzwa hayo maduka ya nje
 
Kelvin X

JF-Expert Member
Jun 28, 2011
1,623
2,000
Kuna kipindi Magufuli alipiga marufuku ya maduka hayo kuwa ndio chanzo cha dawa Kukosekana Hospitalini kwani ilionekana kuwa madawa hospitalini yanchukuliwa kinyemela na kwenda kuuzwa hayo maduka ya nje
Zile ni siasa huwezi chukua dawa hospitali kuholela hivo. Labda kilichokua kina fanyika ni madaktari kuwaandikia watu cheti wakachukue nje
 
Diazepam

JF-Expert Member
Dec 3, 2020
231
500
Kuna watu wao huwa ni kulaumu tu hata akienda hospital tayari anakuwa na mentality ya kulaumu mfano wake ni mtoa mada.

Hivi kwa mikwara ya kipindi kile ya awamu ile ni nani alikuwa na ubavu wa kuweka dawa yenye nembo ya MSD dukani kwake?halafu hiyo ya kusema madawa sijui yalikwepo kipindi kile ni uongo mtupu acha kupotosha watu.

Kipindi kile kwanza kulikuwa na ujinga wa matibabu bure kwa special groups halafu hakuna fungu la kutoka huko juu. Halafu kuna vile vibima flani hivi vya elfu 30 yaani ukifungua file na kulipia ultrasound kishaisha na wategemezi nafikiri ni sita kwa hiyo 30k. Na asilimia kubwa hospital zilitakiwa kujiendesha kwa mapato ya ndani unategemea nini?

Yaani kuhusu dawa kutopatikana hospital ni sera mbovu tu za uongozi wa juu hakuna daktari wala nesi anayepanga hayo mambo ya madawa hospital ni issue ya policy maker na mnawajua.
Kwa hiyo mtoa mada unashauri maduka nje ya hospital yafungwe ndo dawa hospitalini zipatikane? Nchi inavijana wa hovyo sana.
 
Diazepam

JF-Expert Member
Dec 3, 2020
231
500
Yani inashangaza na hao madaktari wanaoandika hizo dawa wao kwanini wasimshauri mtu wa bohari kwamba alete varieties za dawa! Yani kwanini iwe Paracetamol tu na sio Aspirin, Diclopar,Ibuprofen?

Yani kwanini dawa iwe aina moja tu!
Mkuu extrovert, uagizaji wa dawa katika hospital huwa unafanyika kwa kuzingatia umuhimu wa dawa, gharama zake, idadi ya wagonjwa waliotokea kuhitaji aina fulani ya dawa pamoja na fungu la pesa iliyoletwa kutoka serikalini n.k.

Labda mfano hapo kwenye hiyo paracetamol, aspirin, ibuprofen etc... Inabidi paracatamol ziwe nyingi sababu wengi san watatumia paracetamol ila aspirin na ibuprofen zitakwepo kiasi kwaa sababu sio kila mmoja atatumia aspirin au ibuprofen kutokana na adverse effect zake. Pia kuna zile dawa kama opioids etc zina gharama kubwa san hivyo ile kamati haiwezi nunua dawa zenye gharama kubwa na zinafanya kazi kwa baadhi ya wagonjwa ikaacha zile zinazotumiwa na wengi.
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
51,310

Sawa sawa mkuu nimekupata
 
Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
39,531
2,000
Kipindi cha awamu ya tano Mheshimiwa Raisi Magufuli alipiga marufuku sana ya maduka yaliyo nje ya hospitali za serikali,
.

Lakini hayajawahi kutoweka/kuondolewa nje ya Hospitali za umma wakati wote wa awamu ya mwendazake.
 
Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
7,965
2,000
Mkuu extrovert, uagizaji wa dawa katika hospital huwa unafanyika kwa kuzingatia umuhimu wa dawa, gharama zake, idadi ya wagonjwa waliotokea kuhitaji aina fulani ya dawa pamoja na fungu la pesa iliyoletwa kutoka serikalini n.k...
Kwenye nchi yoyote ile huduma bora za afya ndio kipaumbele kwani afya ndo kila kitu kwenye maisha ya binadamu.

Hizi hizi huduma mbovu pamoja na Ukosefu wa madawa hospitalini ndio chanzo cha vifo vingi ambavyo vingeweza kuepukika, serikali iweke sera nzuri kupitia wizara ya afya ili kuondoa hili tatizo.

Mbona swala la tozo limewezakana nchi nzima
 
Diazepam

JF-Expert Member
Dec 3, 2020
231
500
Kwenye nchi yoyote ile huduma bora za afya ndio kipaumbele kwani afya ndo kila kitu kwenye maisha ya binadamu. Hizi hizi huduma mbovu pamoja na Ukosefu wa madawa hospitalini ndio chanzo cha vifo vingi ambavyo vingeweza kuepukika...
Hii ni nzuri sana mkuu. Ahsante
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
12,492
2,000
Huyu waziri amekuwa akitoa matamko yenye ukakasi kila wizara anayopewa.

Siku si nyingi zilizopita akiwa TAMISEMI alikataza wanafunzi kusoma masomo ya ziada wakati wa likizo. Wadau mbalimbali walipiga kelele kulamikia tamko hili wakiwemo viongozi.

Hivi leo kuna tamko linatembea mitandaoni likimnukuu Ummy (kama waziri wa afya) akiwataka wenye maduka ya madawa baridi ndani ya mita 500 ktk hospitali zote nchini kuyaondoa mara moja.

Kuna maswali mengi kuhusu tamko hili. Kwann? Kwasabb gani? Lina faida gani? Au ni wivu tu?
 
Ngariba1

JF-Expert Member
Jan 12, 2017
1,319
2,000
Huyu waziri amekuwa alitoa matamko yenye ukakasi kila wizara anayopewa.

Siku si nyingi zilizopita akiwa TAMISEMI alikataza wanafunzi kusoma masomo ya ziada wakati wa likizo. Wadau mbalimbali walipiga kelele kulamikia tamko hili wakiwemo viongozi...
Lakini ndivyo sheria inavyotaka. Anasimamia sheria.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom