Dawa ya mgomo wa hospitali binafsi

WAZO2010

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
1,610
3,738
Nimefuatilia kwa karibu tokea JPM afariki tabia ya watu, au taasisi, au takaba la kada flani kugoma, imeanza kushamili na kuzoeleka kama utaratibu halali, na kuwa sugu sasa katika awamu ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

Baadhi ya maeneo ni Bei ya Mafuta, bei ya Sukari, na sasa Hospitali binafsi kugomea Bima za NHIF.
Nime fuatilia kiini cha huu mgomo siyo madai halali ya hizi hospitali, bali lengo lao kubwa ni kuibia wananchi kwa kudai bei kubwa kuliko bei elekezi za Wizara ya Afya.

Mfano tu; Dozi ya Panaldo ktk Duka la Dawa (Pharmacy) ni TShs 2000. Hizi Hospitali binafsi kwa mtu wa BIMA wata andika Panaldo 5,000. Hivyo hivyo ktk vipimo mbalimbali, ni mwendo wa kuzidisha mara 2 au 3 ya bei halali! Hii ina ongeza mzigo kwa wananchi, serikali na NHIF, na kujikuta NHIF inashindwa kuhudumia wateja wake vizuri na kupunguza baadhi ya huduma mhimu kwa wanufaika wa BIMA ili mradi tu kukidhi matakwa na kulipa madeni yasiyo halali ya hizi hospitali binafsi.

Hii tabia ikiendekezwa hata gharama za matibabu kwa raia wa kawaida wasiyo na BIMA zita panda maradufu na kuongeza gharama za maisha pamoja na ugumu wa maisha kwa Wananchi.

Izingatiwe, roho na uhai wa binadamu siyo sehemu ya majaribio au maigizo. Uhai hauna spare!
Hii ni nchi halali na Huru ni lazima sheria, miongozo na taratibu zake zifuatwe! Na ni lazima Rais wa Nchi ya Tanzania aheshimiwe kwa 100%.

Naomba kuishauri serikali yangu na vyombo vya usalama vifanye yafuatayo kutatua mgogoro wa Hospitali binafsi.

1. Rais afute msamaha wa kodi kwa vifaa vyote na Madawa kwa Hospitali binafsi. Import duty itozwe na kodi ya mapato iwe 30% kama ilivyo kwa makampuni binafsi. Waziri wa fedha wasilisha Bungeni mswada mpya wa dharura. Ina onesha hospitali binafsi zinataka kufanya biashara na siyo kutoa huduma.

2. Ipigwe Marufuku kwa Madaktari wote wa serikali kufanya part time Hospitali binafsi kwa muda wa miaka 3. Asiye taka kutii agizo hili aache kazi.

3. Mafunzo kwa Vitendo kwa Wanafunzi wa Udaktari , Pharmacia, Macho, nk na wataalamu adimu wasipangwe Hospitali Binafsi.

4. Serikali ifute vibali na leseni kwa Hospitali Binafsi zenye asili ya Kigeni na zenye uchochezi. Hii lengo lake ni kuzuia hujuma na mauaji kwa raia wasio na hatia.

5. Serikali iboreshe hospitali zake kuanzia ngazi za kituo cha Afya hadi Rufaa. Mfano: kuboresha vifaa tiba, upatikanaji wa dawa, idadi ya wataalamu, miundombinu, na kupunguza urasimu na usumbufu wa matibabu (foleni ndefu, mizunguko mingi ya faili, madaktari kukwepa zamu zao na kwenda Private, nk).

6. NHIF acheni mzaha na pesa za Wateja wenu, kwa kuondoa huduma na dawa mhimu ktk vifurushi. Wigo wa matibabu na dawa upanuliwe.

7. NHIF dhibitini matumizi ya hovyo ya fedha za Wachangiaji. Hizo ni pesa za wanachama wenu siyo pesa zenu. Kusanyeni madeni. Toeni huduma bora za kiushindani na BIMA zingine.

Mungu ibariki Tz.
 
Back
Top Bottom