Maandamano ya CHADEMA Jijini Mwanza

Maandamano ya CHADEMA Jijini Mwanza

acha upashikuna wewe huaridhiki chadema ikiwa pamoja. Zitto yupo mwanza na alikuwa kushoto kwa dr slaa, sasa huu umbeya na ufirauni unautoa wapi? Umezoea kutumwa kama jini wewe -jini tena la kike. Stopppppp your stupid behaviour.
waeleze watakuwa wanasumbuliwa na YAHAYA wala sio siri maana wameshaona maji yameshawazidia
 
lakini MWanf1 umedhibitisha hayo maneno ya huyo mtoa mada?
JE ni kweli Zitto amekataa?
je ilikuwa ni lazima wabunge wote waende Mwanza?
mbona watu mnakosa reasoning ability ya vitu vidogo tu
hao wanaoleta mada ni watu wasiotaka mazuri ya Mageuzi na mabadiriko tz kwa ujumla
hivyo msipokuwa makini na watu kama hao, mtaishia kulaumiana bure

mkuu mallaba ..usihangaike na desperate patient ..atakufia mikononi mwako .... zitto alikuwapo mwanza na hata asingekuwepo maandama yamefanyika kwa mafaniko makubwa sana ...
 
240211-1444.jpg Hapa ni mabatini leo hiii hapa rocky city peopleeeeeeeeeeeeeeeees powerrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
jeykey umeishaanza tena chokochoko. humpati mtu hapa. mbona humzungumzi Mbowe na akina Mnyika? JAMANI HUYU NI YULE YULE JEIKEI WA UKWELI.
kumbe inwezekana akawa ndio yeye mwenyewe eti?
 
mkuu mallaba ..usihangaike na desperate patient ..atakufia mikononi mwako .... zitto alikuwapo mwanza na hata asingekuwepo maandama yamefanyika kwa mafaniko makubwa sana ...
Thank u LAT,
Hawa jamaa wanahaaha hwana pa kwenda na mshetani yameshawabana zaidi...
 
MMmmhh!

Mara ya mwisho niliona Hospitali ikijengwa kwa Tofari na sement kisha kuwekwa vifaa dawa na madakatari.

Kama zinajengwa kwa maandamano basi hiyo ni Techolojia mpya kwangu na pengine ya kuigwa.

Kuna Hospitali umesikia imejengwa kwa maandamano mahali popote duniani??

Ila najua kwamba Wizi na ubadhirifu wa Fedha za umma ni sababu moja kubwa ya kushindwa kujenga Hospitali nzuri.

CCM wamekumbatia Maharamia kama Rostam Azizi na Dowans yake na Edward Lowassa.

KWa mtaji wa kukumbatia mafisadi tunaweza jenga Hospitali ngapi Tanzania????

hivi Hospital zinajengwa na maandamano??[/QUOTE]
 
Bora Ukimwi kuliko Kikwete! Bora Ukimwi Kuliko Kikwete! ni nyimbo za waandamanaji Mwanza leo.
 
Wakuu yale maandamano ya CHADEMA katika Kanda ya Ziwa ndio yameshaanza.Maandamano yameanzia Buzuruga kuelekea uwanja wa Furahisha.Watu ni wammejitokeza kwa wingi wa jinsia na rika zote.Kwabahati mbaya sijakaa kwenye position nzuri ya kurusha picha lakini nikipata fursa nzuri nitazirusha.

Aluta Continua.

From kwenye Maandamano Mwanza

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

182093_1470892587284_1682707865_914231_1937388_n.jpg

Picture added by JF Admin

181960_1806066466589_1087715548_32082108_675130_n.jpg


Mambo ni yanafurahisha, umoja ni nguvu
 
Kama sio Uzembe wake Kikweteeeeeeeeeeee!kama sio uzembe wake Kikweteeeeeeeee! na mabomu yangelilipuka liniiiiiiiiiiiiiiiiii! wakuu ilikuwa niburudani cijawahi kuona.
 
Huyo mwenye jina la kikwerekwere naona kaumbuka, naona macho yake yalikuwa kwa zitto na shibuda; nani kakwambia hao ndio mtaji wa CDM? Poleni sana, watanzania wengi sasa hawako na ninyi; kwa ufupi mnafulia siku zinavyosonga mbele, maana uongo na uozo wa hicho chama chenu na serikali yenu dhalimu unazidi kujianika wenyewe kila kukicha! Poleni sana. :wink2:
 
There are currently 664 users browsing this thread. (186 members and 478 guests)
 
katika hali isiyo tarajiwa wabunge wawili wameendelea kupingana na uongozi wa chadema kwa kukataa maandamano ya mwanza

Mpaka sasa leo(24.02.2011) sio chibuda sio zitto aliyeko kwenye maandamano ya mwanza


Nawapa big up zitto na shibuda


Ona ukweli huu!

181960_1806066466589_1087715548_32082108_675130_n.jpg


Asante kwa uchonganishi, lakini wananchi wanaelewa sasa maana ya umoja wa watanzania ktk kupigania haki yao-na si utengano unaotaka kuukuza wewe mkuu
 
Andamaneni halafu kesho asubuhi au wiki ijayo mtuambie hayo maandamano yameleta mabadiriko gani?
Sio mnaandamana kila siku na hakuna kinachobadiria lakini bado mnaandamana tena na tena na tena.
Kuwa insane maana yake ni " to do the same thing again and again and then somehow expect different results". Mkiandamana kila siku na hakuna kinachobadirika mjue mko insane.

Mkuu, kauli zako zinafanana na OCD wa Arusha ambaye ana bifu na Mbunge wetu Lema. Ndio wewe?
 
Wimbo mwingine wa leo Mwanza ni, kama sio Uzembe wake Kikweteeeeeeeeeeee!Mafisadi wangetoka wapiii!
 
wasikusumbue hao, watu wenyewe wanahesabika, we unadhani watamtisha nani, naona padri ka prove failure leo maana naona watu kama wanamshangaa vile!!!!!!!!!!!!!!!!
ila hawa jamaa kwa kujipa moyo tu, wanaweza

Hata idadi ya Watanzania wote inahesabika Mkuu, Pole hata Mubarak Mke aliumia sana
 
thanx sana wanamwanza. Jamaa hapa amepiga picha vizuri nendeni mkajionee linki hapo chini nguvu ya uma. kweli siku za sisihemu zinahesabika

g sengo
 
katika hali isiyo tarajiwa wabunge wawili wameendelea kupingana na uongozi wa chadema kwa kukataa maandamano ya mwanza

Mpaka sasa leo(24.02.2011) sio chibuda sio zitto aliyeko kwenye maandamano ya mwanza


Nawapa big up zitto na shibuda

Polisi waridhia maandamano ya Chadema

Wednesday, 23 February 2011

dk%20slaa%2021.jpg

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa

Frederick Katulanda, Mwanza

Polisi mkoani Mwanza wameridhia maandamano yaliyoandaliwa na Chadema, kupinga malipo ya fidia kwa Kampuni ya Dowans, kuongezeka kwa gharama za maisha na kupanda kwa gharama za umeme.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Mwanza, Wilson Mushumbusi alisema tayari wamekwishakamilisha maandalizi ya maandamano hayo, yatakayofanyika leo kuanzia saa 8: 00 mchana na kufuatiwa na mkutano wa hadhara.


Maandamano ya Mwanza yanafanyika takriban miezi miwili tangu kutokee mauaji ya raia waliopigwa risasi na polisi mkoani Arusha, wakati walipokuwa wakizuia maandamano ya Chadema mkoani humo.


Katika tukio hilo la Januari 6, mwaka huu watu kadhaa walijeruhiwa, polisi wa Arusha walimwaga damu za watu kadhaa, walioshiriki na wasioshiriki maandamano yaliyoandaliwa na Chadema.


Risasi za moto na mabomu ya machozi vilitumika katika jitihada za polisi kuzima maandamano ya Chadema, wakitekeleza amri ya Mkuu wa Jeshi hilo, Ispekta Jenerali Said Mwema ambaye awali aliyapiga marufuku baada ya kuwa yameruhisiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye.


Jana Mushumbusi alisema maandamano ya Mwanza yatahitimishwa kwa mkutano wa hadhara utakaofanyika katika Viwanja vya Furahisha, Kirumba jijini hapa kuanzia saa10:00 jioni.


Tayari Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amewasili jijini hapa kwa lengo la kushiriki maandamano hayo ya kwanza kufanyika Mwanza tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani, Oktoba 31 mwaka jana.


Dk Slaa aliwasili jijini Mwanza jana mchana. Viongozi wengine wa Chadema wanaotarajiwa kushiriki maandamano na baadaye mkutano ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe.


Mushumbusi alisema mbali na viongozi wa taifa wa Chadema, wabunge wote wa chama hicho wanatarajiwa kuhudhuria maandamano hayo.


Aliwataka wapenzi, wanachama na Watanzania wote kwa ujumla wanaochukia ufisadi kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Mwanza kushiriki.


"Sisi maandalizi yetu yamekamilika na viongozi wote wa kitaifa wa chama na wabunge wote wa Chadema wamethibitisha kuhudhuria maandamano yetu ambayo yataanzia Kituo cha Mabasi cha Buzuruga, Nyakato na kupita Barabara ya Mwanza-Musoma, Nyerere, Kenyatta na kuingia Barabara ya Uwanja wa Ndege kwenda hadi katika Viwanja vya Furahisha," alifafanua katibu huyo wa Chadema.


Mushumbusi alisema kutokana na wao kufanya maandamano ya amani, chama chake kimeandika barua ya taarifa kwa Jeshi la Polisi na kuzingatia sheria ya kutoa taarifa kwa jeshi hilo saa 48 kabla ya kuandamana na wala siyo kuomba kibali.


"Barua ya kuwataarifu Jeshi la Polisi kuhusiana na maandamano tuliwakabidhi tangu Februari 20, mwaka huu na Jeshi la Polisi limekubaliana na maandamano yetu na njia ambazo tutapitia, hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi, tutaendelea na maandamano yetu kama yalivyopangwa," alieleza Mshumbisi.


Katibu huyo alisema lengo la maandamano yao ni kupinga vitendo vya ufisadi, malipo ya Sh94 bilioni ya tozo kwa ajili ya kampuni ya Dowans, kupinga kupanda na kuongezeka kwa bei ya umeme nchini na kuongezeka kwa gharama za maisha.


Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Simon Sirro alipoulizwa kuhusu maandamano hayo, alisema jeshi lake limejipanga na kusema hawana tatizo na maandamano hayo na kwamba watahakikisha wanatoa ulinzi mkali kulinda watu wasio na nia njema kutumia mwanya huo kuzusha vurugu.


"Hatuna tatizo na maandamano, haya tumeridhia na kukubaliana ni wapi watapita, tumejipanga kwa ulinzi ili kuhakikisha maandamano hayo yanakuwa ya amani na salama kwa watu wengine na mali zao," alieleza Kamanda Sirro.


Wachunguzi wa mambo waliozungumzia maandamano hayo walisema huenda yakapata ushiriki wa watu wengi kutoka na mada ziliyopangwa kuzungumzwa, kuwagusa watu wengi.
 
Duh! Huyu nae mkabila kwelikweli. Aweza sema sisiem si lolote imejaa waswahili au Waislam simply kwa sababu viongozi wake wamezaliwa huko. We are all Tanzanians kila moja na karama yake. Anayeweza kutuhamasisha tuwe makini kuthibiti viongozi wasifuje rasilimali zetu haya. Anayeweza kutuhamasisha kuwa tumchague kuunda serikali sawa pia.
 
Back
Top Bottom