Dada Regia, mimi mwanachama wa chadema. Lakini naanza kupata mashaka na agenda mliyonayo viongozi wetu hii ya kuandamana. Siogopi maandamano ila sidhani kama ni muda muafaka. Tumieni njia mbadala kuimarisha chama na sio hii inaleta mtazamo hasi na kukitenga chama na kundi flani kubwa la watu ambao kwa kiasi kikubwa kwa kutokuamini upinzani unaweza kufanya kile unachoahidi, waliipa kura ccm mwaka jana na kuirudisha madarakani japo wameshaichoka sana. Lazima tukubali ukweli, ccm bado inakubalika sana. Unaweza kuona Bungeni walivyofunika, ok hata ukisema walituibia viti 20 vya ubunge bado upinzani hauna nguvu. Maandamano na migomo haiwezi kuwang'oa kwa sababu ni wachache ndio wataunga mkono. Tena leo CCM wakiamka wakafunga mjadala wa Dowans, wakawafikisha mafisadi kadhaa kizimbani(kama ilivyofanya kwa kina Mramba), upinzani wote utanyong'onye. Hebu tutafute sera za kudumu tuachane na vivuli vya matukio ya mpito. Kwa hiyo staili yenu, mnapunguza kasi ya ukombozi wa Taifa hili. Muda wa maandamano sio sasa, msirubuniwe na wachache wanaowazunguka ambao ni waelewa, wasomi na walio karibu na vyombo vya habari. Watanzania wengi hawako pamoja na nyie hata kidogo. Na siku CCM ikiamua kutusambaratisha litakua ni pigo takatifu na hatutasimama tena. Mwambie Dk Slaa, ths will never work out!!