Dkt. Slaa athibitisha kushiriki maandamano ya CHADEMA jijini Mwanza

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Maandalizi ya maandamano ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoani Mwanza yamefikia asilimia 90 huku miongoni mwa waliothibitisha kushiriki ni mwanasiasa mkongwe, Dk Wilbrod Slaa.

Taarifa hiyo imetolewa jana Jumanne Februari 13, 2024 na Katibu wa Chadema Kanda ya Victoria, Zacharia Obad, wakati viongozi wa kamati ya maandalizi ya maandamano hayo walipotembelea na kukagua uwanja wa Furahisha wilayani Ilemela jijini hapa, yanapotarajiwa kuhitimishwa.

Dk Slaa alipozungumza na Mwananchi Digital lililotaka kujua kama kweli atashiriki maandamano hayo amesema, “ni kweli nitashiriki na nitakuwepo.”

Katibu wa Chadema Kanda ya Victoria, Zacharia Obad amesema “Tutatumia maandamano hayo kuomboleza kifo cha (Edward) Lowassa kwa sababu aliwahi kuwa mwanachama na kiongozi ndani ya chama chetu, pia alikuwa kiongozi wa umma alipokuwa Waziri Mkuu nchini,” amesema Obad.

Amewataka wafuasi wa Chadema na wasiokuwa wafuasi kujitokeza kwa wingi kushinikiza matakwa hayo mawili ambayo ni ugumu wa maisha na Serikali kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu miswada mitatu ya Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani pamoja na ya vyama vya siasa iliyokwisha pitishwa na Bunge.

Source - Mwananchi
 
Mambo yamekaa sawa, ngoja mtu wetu aingie kwemye mfumo wao, halafu ukikaribia uchaguzi aanze kuwavuruga na kuwatukana
 
“Tutatumia maandamano hayo kuomboleza kifo cha (Edward) Lowassa kwa sababu aliwahi kuwa mwanachama na kiongozi ndani ya chama chetu, pia alikuwa kiongozi wa umma alipokuwa Waziri Mkuu nchini,” amesema Obad.

Source - Mwananchi
Nilifikiri Dr. Slaa hana chama cha siasa
 
Maandamano haya si ya kichama, ni yawatu wote wanaoumizwa na ugumu wa maisha

Usiposhiriki kwa sababu ya chama chako, maana yake wewe na chama chako ni wanufaikaji wakubwa wa ugumu wa maisha kwa watanzania

Kataa maisha magumu kwa kushiriki maandamano

Kataa mgao wa umeme kwa kushiriki maandamano!

Ingawa pia hata Chadema wanazingua kwa mengi tu!
 
Maandalizi ya maandamano ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoani Mwanza yamefikia asilimia 90 huku miongoni mwa waliothibitisha kushiriki ni mwanasiasa mkongwe, Dk Wilbrod Slaa.
Ni vema , huu ni ukobozi hata kwa johnthebaptist ingawa si rahisi yeye kuona ilo. hajui kuwa ana mtoto wa shangazi ambaye ananyanyaswa na CCM, andhani ataishi milele.......
 
Mimi nilifikiri watumiaji wa Jf wote wana akili timamu.
Kama unanisema mimi basi umejisema wewe kuwa huna akili timamu. Maana mtu kutojua kama Dr. Slaa ni mwananchama wa Chadema sio jambo la ajabu, ukizingatia mambo yaliyotokea tangu alipojiondoa ukatibu Mkuu wa Chadema. Dr. Sla sio baba yangu kiasi nijue mambo yake yote na yuko wapi kisiasa
 
Huyu mzee na umri alionao huwezi kufikiri kabisa kama anaweza kushiriki mambo yasiyoendana na umri wake. Nimeamini madaraka ni kama madawa ya kulevya ,ukiyatumia huwezi kuacha.
 
Maandalizi ya maandamano ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoani Mwanza yamefikia asilimia 90 huku miongoni mwa waliothibitisha kushiriki ni mwanasiasa mkongwe, Dk Wilbrod Slaa.

Taarifa hiyo imetolewa jana Jumanne Februari 13, 2024 na Katibu wa Chadema Kanda ya Victoria, Zacharia Obad, wakati viongozi wa kamati ya maandalizi ya maandamano hayo walipotembelea na kukagua uwanja wa Furahisha wilayani Ilemela jijini hapa, yanapotarajiwa kuhitimishwa.

Dk Slaa alipozungumza na Mwananchi Digital lililotaka kujua kama kweli atashiriki maandamano hayo amesema, “ni kweli nitashiriki na nitakuwepo.”

Katibu wa Chadema Kanda ya Victoria, Zacharia Obad amesema “Tutatumia maandamano hayo kuomboleza kifo cha (Edward) Lowassa kwa sababu aliwahi kuwa mwanachama na kiongozi ndani ya chama chetu, pia alikuwa kiongozi wa umma alipokuwa Waziri Mkuu nchini,” amesema Obad.

Amewataka wafuasi wa Chadema na wasiokuwa wafuasi kujitokeza kwa wingi kushinikiza matakwa hayo mawili ambayo ni ugumu wa maisha na Serikali kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu miswada mitatu ya Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani pamoja na ya vyama vya siasa iliyokwisha pitishwa na Bunge.

Source - Mwananchi
sawa,
wengine wacha wamalize matanga kwanza ikiwa kwa wengine ni fursa fursa muhimu sana maadamu ameumaliza mwendo 🐒

kwenye kuchukua fomu ya urais 2015 tume ya uchaguzi iliamriwa inchi isimame....
Amelala bas amelala 🐒

R I P Laigwanan comrade ENL
 
download (10).jpeg

Mwamba huyu hapaaaa huyu ndio sio mnafiki na ndie anae jua maandamano
 
Maandalizi ya maandamano ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoani Mwanza yamefikia asilimia 90 huku miongoni mwa waliothibitisha kushiriki ni mwanasiasa mkongwe, Dk Wilbrod Slaa.

Taarifa hiyo imetolewa jana Jumanne Februari 13, 2024 na Katibu wa Chadema Kanda ya Victoria, Zacharia Obad, wakati viongozi wa kamati ya maandalizi ya maandamano hayo walipotembelea na kukagua uwanja wa Furahisha wilayani Ilemela jijini hapa, yanapotarajiwa kuhitimishwa.

Dk Slaa alipozungumza na Mwananchi Digital lililotaka kujua kama kweli atashiriki maandamano hayo amesema, “ni kweli nitashiriki na nitakuwepo.”

Katibu wa Chadema Kanda ya Victoria, Zacharia Obad amesema “Tutatumia maandamano hayo kuomboleza kifo cha (Edward) Lowassa kwa sababu aliwahi kuwa mwanachama na kiongozi ndani ya chama chetu, pia alikuwa kiongozi wa umma alipokuwa Waziri Mkuu nchini,” amesema Obad.

Amewataka wafuasi wa Chadema na wasiokuwa wafuasi kujitokeza kwa wingi kushinikiza matakwa hayo mawili ambayo ni ugumu wa maisha na Serikali kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu miswada mitatu ya Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani pamoja na ya vyama vya siasa iliyokwisha pitishwa na Bunge.

Source - Mwananchi
Kilichomtoa Lowasa Chadema JPM alipobana shughuli za kisiasa vyama vya upinzani na wengi kufuatwafuatwa akaona maisha magumu kisiasa na hivyo EDL akachomoka kurudi kwake kwa zamani. Hali ya kisiasa ilikiwa ngumu mno upande wa upinzani la sivyo asingerejea huko. haikuwa kwa kupenda yeye na Sumaye.
 
Back
Top Bottom