Luhanjo atoa ripoti, Jairo arudishwa kazini

Luhanjo atoa ripoti, Jairo arudishwa kazini

Niliposikia tu Jairo kawekwa likizo ya malipo nikajua mchezo umeanza kusukwa. Hakukuwa na uchunguzi makini. Kilichofanyika ni kile wazungu wanaita "white wash," kuwanusuru Jairo na Kikwete.

Jairo ni msiri mkubwa sana wa mkweree kwahiyo hata huo mchango inawezekana kabisa ulipata blessings za Ikulu. Siamini hata siku moja kuwa wanyama pori wanaweza kutoroshwa toka mbugani kwa ndege ya kijeshi na kupelekwa mpaka Qatar bila vyombo vya dola kufahamu, na kama hivyo ndivyo basi IKULU yetu ilikuwa na taarifa kamili juu ya wizi wa wanyama hawa. Kama hivyo ni sahihi basi kusimamishwa kwa mkurugenzi wa wanyama pori ni dongo lingine la macho tunalaopigwa wadanganyika lakini siku ya siku jamaa atarudishwa kazini kuwa hakuwa na hatia!! Hiyo ndio serikali ya kishikaji, lakini iko siku mtakuja juta kwa haya mnayofanya.

Huu ndio Mwanzo Wining chess.jpg

Hivi kizazi cha wakati huu hapa TZ hamna watu wenye kusubutu kama Uncle Tom na Hashimu Macghee. Kama wapo basi usubutu wao unahitajika sasa kuliko wakati mwingine wowote wa historia ya nchi hii.

CAG ameota mapembe baada ya kuona amebaki yeye anayeaminiwa na wananchi na wanasiasa leo bila aibu ameonyesha kwamba yuko kisiasa alikwenda IKULU kufanya nini kama sio mchoro aliochora Luhanjo kumuita ili wamsafishe JAIRO wote kwa pamoja natahadharisha tukimuachia CAG kutumika kisiasa kama TAKUKURU,POLICE wanavyotumika Lazima kwa nguvu zetu zote tusiruhusu kabisa Jakaya KIkwete kuharibu nchi hii,mambo anayoendelea kuyafanya ni ya maudhi mno ameamua kutumia taasisi za kiserikali kuwa mwizi na kupindisha sheria,anaiweka nchi yetu kwenye rehani anataka tuingie kwenye mchafuko

niamini waliosema tutajuta kuwa na Jakaya Mrisho kwa miaka mitano ni mtu hatari sana aliyewahi kutawala nchi amejionyesha alivyonakiburi na anavyodharau wananchi,hajali kwa sababu anajua watanzania tupo kama misukule tu anatutoboa macho kwa vidole na sisi tumekuwa vipofu hatuoni uovu wake

As long CCM is in power haya madudu hayataisha hata siku 1.
CAG naye anajidhalilisha tu..because this is not the first time anatoa report zenya utata baada ya ukaguzi wake.
Mnakumbuka issue ya UDOM? Wafanyakazi wanapata mishahara tofauti na ile inayotoka hazina kapewa mpaka salary slips zinaonyesha kila kitu, in the end anasema hakuona ubadhirifu wowote UDOM.
Msubiri report yake ya UDA mtashangaa. Anyway, tunajua anafanya kwa maagizo ya mamlaka iliyomteua, but amepoteza kabisa credibility mbele ya jamii ya watu makini.
Mm binafsi siewezi amini any crap coming out of the so called CAG. Magamba tu naye.

hapa kuna siri kubwa badala ya kutueleza findings tunaelezwa errors kwenye accusations! tusubiri labda CAG atatoa report au ndo amemaliza?

kuanzia mwamzoni nlipata doubt, ni vigumu kumhukumu jairo mwenyewe. Chain ni ndefu sana. pengne hadi kwa wakubwa.
Nani wa kumtetea mtanzania???????

Pinda je? Alikurupuka?
Ningekuwa karbu na mtoto wa mkulima (Pinda) ningemuomba ajiuzulu!!!!!
Amepingwa!!!!
Nani msafi wa kumfukuza JAIRO????.
Wasafi ni sisi Wananchi.

Mbaya zaidi nimemsikia Luhanjo anasema kuwa Jairo, anaweza kwenda mahakamani kufungua kesi ya kuchafuliwa jina lake.
Pia wanafanya uchunguzi kujua ni nani alimpa mbunge ile barua, na hakijulika lazima wamchukulie hatua kali za kinidhamu

Nipo tayaaaaaaaaaaaaaaaaaari for any thing enough is enough its time for change

Chekundu cheusi? chekundu cheusi, chekundu cheusi? tukawaambia watu hapa toka mwanzo ni mazingaombwe haya msicheze; hawakutaka. Wakang'ang'ania "tumekiona tumekiona' jamaa akawaambia "kama mmekiona wekeni pesa zenu" watu wakihamasishana wakaweka pesa yao. Jamaa anafunua "cheusi"!! wameliwa.. wanalalamika.. "ooh tulikiona kabisa, tulikiona kabisa".. waliliwa kwa Ngeleja hawakuamini, wameliwa kwa jairo hawataki!!

Nawaangalia wachezeshewe tena mchezo wa 'chekundu cheusi chekundu cheusi".. mkitaka kujua ni mchezo angalieni wanaowaambia 'na mimi nimekiona!!""

Wakati mwingine mtusikilize...

grrrrrr!!

Mbaya zaidi nimemsikia Luhanjo anasema kuwa Jairo, anaweza kwenda mahakamani kufungua kesi ya kuchafuliwa jina lake.

Pia wanafanya uchunguzi kujua ni nani alimpa mbunge ile barua, na hakijulika lazima wamchukulie hatua kali za kinidhamu

Lohanjo apeleke mavi yake chooni, na aache mara moja kutuona watz ni mazezeta. Kuna haja gani ya kumtafuta mtu wa aliyeuza mali ya wizi badala ya kumkamata aliyekutwa na mali ili yeye ndio aeleza aliyemuuzia. Rais legelege hapo magogoni amewafanya wote hapo ikulu wazugaji. Hapa tu mwaka bado, itakuwa je kwa minne iliyobaki?

Chekundu cheusi? chekundu cheusi, chekundu cheusi? tukawaambia watu hapa toka mwanzo ni mazingaombwe haya msicheze; hawakutaka. Wakang'ang'ania ;tumekiona tumekiona' jamaa akawaambia;kama mmekiona wekeni pesa zenu; watu wakihamasishana wakaweka pesa yao. Jamaa anafunua ;cheusi;!! wameliwa.. wanalalamika.. ;ooh tulikiona kabisa, tulikiona kabisa;.. waliliwa kwa Ngeleja hawakuamini, wameliwa kwa jairo hawataki!!
Nawaangalia wachezeshewe tena mchezo wa 'chekundu cheusi chekundu cheusi;.. mkitaka kujua ni mchezo angalieni wanaowaambia 'na mimi nimekiona!!";
Wakati mwingine mtusikilize...
grrrrrr!!
Huu mchezo nakumbuka siku ya kwanza kuuona ilikuwa Mwaloni Kirumba Mwanza, uliletwa na wazaire teh teh teh!

Juzi nilikuwa nasikiliza moja ya hotuba za Baba wa Taifa Mwal. J.K.Nyerere, akielezea mkasa wa mgiriki aliyemweka ndani baada ya kusema ameiweka serikali yake mfukoni, alisema "haki na sheria ni vitu viwili tofauti". Alizungumzia kwa kirefu jinsi alivyopata shinikizo ndani la nje ya Tanzania ili apate kumwachia huru . Pia alisema mtu hawezi kusema kuwa ameiweka serikali mfukoni kama hajatoa rushwa, kumbuka JAiro aliwaita wabunge Ze Comedy.

Katika hali ya kawaida unaweza ukajiuliza ukashindwa kuelewa kabisa, kama hata hili jambo hakuna mwenye tuhuma tutegemee kuwa kuna afisa yeyote atakuja kupatikana na rushwa? je bado tunaamini serikali hii ni makini? inawezekana Jairo hana hatia lakini hiki ni kielelezo cha siasa uchwara za chama tawala. Serikali hii haiwezi kupambana na maovu kwani wote wako kwenye boti moja. Ikiitobolewa wote watazama na hakuna mwenye uwezo wa kumtosa mwingine. Nchi imekwisha hii.

kuanzia mwamzoni nlipata doubt, ni vigumu kumhukumu jairo mwenyewe. Chain ni ndefu sana. pengne hadi kwa wakubwa.

Nani wa kumtetea mtanzania???????

Tz itatetewa na mtu yeyote ambae hana ushirikiano na magamba aka ccm

Umoja na mshikamano kama misri ndiyo itakayotukomboa Tanzania kwani kukubaliana na hali kama hii ni sawa na kunoa panga na kujaribia makali yake shingoni TZ wakeup

Hii serikali inatupeleka wapi sasa. Mtu ambaye ametuhumiwa kwa uwazi kabisa anarudishwaje tena kazini. It beats me!

Kama ni kweli basi itadhihirisha serikali yetu inavyoendeshwa, tutasikitika mno kwa jairo, malima na ngeleja kwa kutowajibika kwa hili!
Wana CCM wanatazama kwa makini mwisho wake kabla ya kutoa maamuzi yao!

Back
Top Bottom