Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Mwamba wa Senegal ukiacha mapenzi yangu binafsi kwa sadio mane kwa kile alichokuwa anakifanya uwanjani...NAPATA SHIDA SANA KUAMINI JUU YA USAJILI WA NUNEZ KAMA UTALIPA KAMA AMBAVYO INATAZAMIWA BADO NAONA SALAH ATAENDELEA KUTUBEBA MBELE LABDA NA JOTA ILA SIJUI KWANINI ROHO YANGU BADO INAKATAA KUAMINI KUWA DIAZ NA NUNEZ NI WACHEZAJI AMBAO WATAZIBA PENGO LA HUU UTATU TULIOKUWA NAO MIAKA YA KARIBUNI....NIMEPENDA WALIVYOSAJILIWA SABABU NI WACHEZAJI WENYE VITU FLANI VIZUR UWANJANI ILA KUWABEBESHA HII MIZIGO YA KURITHI MIKOBA YA FLANI NA FLANI KWA HII LIGI PENDWA YA EPL NADHANI TUACHE MUDA UONGEE ...DIAZ NAONA AMEFIT KWENYE TIMU SABABU YA AINA YA MSIMU TULIOKUWA NAO PLUS WACHEZAJI ALIOWAKUTA HAPO MBELE NGOJA TUONE KIPIND TUKIWA NA WAKAT MBOVU ATATUPA NINI KAMA AMBAVYO TUTATEGEMEA.....SIWEZI KUBADILISHA ILA NATAMANI IFIKE KIPINDI CLUB YANGU PENDWA YA LIVERPOOL IACHANE NA POLICY ZA KIJINGA,MPIRA NI PESA DUNIA YA SASA TUSIJIAMINI SANA KWAMBA KILA WAKAT KLOOP ATATULETEA MAAJABU AU BAHATI ITAKUWA KWETU TU....NO WAY HAWA WACHEZAJI NI BINADAMU NA WANAHITAJI WALIPWE VIZURI KULINGANA NA KAZI ZAO SIO KUENDEKEZA POLICY ZA UNYONYAJI WAKATI WANAONA WENZAO WANAVYOFAIDI MATUNDA YA KAZI ZAO....NILITAMANI KUONA SALAH,MANE AND FIRMINO WAKIENDELEA KUWA PAMOJA ILI KUWAONGOZA HAWA WAGENI HADI WATAKAPOIVA ILA SIO KUWATWISHA HII MIZIGO SIJUI YA KUCHUKUA NAMBA YA FLANI...TIMU YA MISIMU MIWILI MITATU ILIYOPITA IMETUFANYIA MAKUBWA SANA WANA LIVERPOOL WA KIPINDI HIKI HATUTAKIWI KUIBEZA HATA KIDOGO.
Duuuh nimekwelewa sana fellow Red yaaani....

Tuwe na subira.

YNWA
 
Mmekwisha tayari ,huyo Darwin anaenda kuflop ,Diaz nae ni nguvu ya soda tu ,next season mtamkataaa kabisa
 
Asijekuwa kama carol tu
Hapana Carrol alikua one season wonder na Dalglish nii muumini wa kujenga kikosi kwa kutumia Great Britain au UK players hivyo alifeli kocha ndio maana FSG hawakua na namna zaidi ya kupumzisha...

Darwin Nunez ni generation talent yaaani next big thing from Uruguay..

Darwin =Surez+Cavani.

YNWA
 
Hii partnership ya Nunez na Salah haitashine kwa sababu Salah ni selfish na Nunez anapenda kufunga.
Unselfish Mane ndo aliekuwa anaweza kucheza na Salah
Hapo ndo tutajua Mane alimsaidia vp Salah kutamba

Otherwise time will tell!!

Kama uelewa wako wa Mpira ndiyo huu bora tu ukashabikie Rede na Netball.
Football haikufai kabisa unaibisha Kijiwe chako munachoongelea mpira.
 
Carvalho hua ana operate vyema upande wa kushoto na Elliott hua ni upande wa kulia.
Ngoja tusubiri maana kwa mara ya kwanza Klopp kawekeza pesa ya maana kwa real 9 hivyo pengine hata mfumo atakuja kivingine.

Msimu ujao sasa tunaanza na DNS.. Diaz Nunez Salah.

YNWA

DNS kwa drip hii lazima Mgonjwa apige chafya tu
 
Labda Origi alikua hatoshi ila kwa usajili huu natumai mfumo utabadilika sasa .
4 2 3 1 Boby hapa hatakosekama uwepo wake utawaongezea ubora hawa wageni

Fab na Cantara kati halafu Diaz Boby Salah hafu mbele ndo Nunezi.

Baada ya ushindi asiache kuwaingiza hawa watoto Cavlnho na Eliot kuwajenge

Haka katoto kengine Ramsey bonge la mchezaji sijui itakuje na Kloop muoga wa ku roteti
 
Screenshot_20220618_055022.jpg
 
View attachment 2262725

Julian Ward ni balaaaa tupu.. Tazameni 👇 👇
The deal in numbers..
*bei ya dogo ni £64m,adds on ni kama £26m ili kutimiza £85m... hii itatimia endapo dogo atatimiza majukumu fulani fulani uwanjani...

*mshahara wa Darwin ni £140k kwa wiki 🙆🏿🙆🏿🙆🏿🙆🏿.....

*Benfica get £46.7m upfront only.

*Adds on Benfica will get £4.3m if he plays 10 times

*Adds on Benfica will get £8.6m when he plays 60 games.

*Adds on Benfica will get £8.6m on performance based payment.

*Penarol where he started playing in Uruguay will get £1.9m, hawa ndio walimuuza kwenda Almeria wakaweka future sell clause.

*Almeria club from Spain will get £8.95m hawa ndio walimuuza kwenda Benfica wakiweka future sell clause.

*Intermediation services(wakala au mwanasheria) ni £6.24m

*Amesaini miaka 6. Tunae mpaka msimu wa 2028.

* ina maana simple solution Mane £41m upfront na Darwin £46.7m upfront ni dili bora kabisa kwa bajeti ya klabu kuweza kuingia tena sokoni hata kabla ya kuuza mchezaji mwingine... Kweli kwa Julian tutulie tu mambo ni motooo 🔥 🔥 🔥

YNWA
Duu kweli sisi tunasindikiza wanao kula maisha yani Mwanasheria/Wakala anapata karibu tshs.19 billion.
 
Saido Mane the Legend...

Ndio alikua mchezaji wa kwanza ghali na wa kimkakati kusajiliwa na Klopp Liverpool.
Alisajiliwa Liverpool mwaka 2016 akicheza gemu yake ya kwanza 14/8/16.

Mane alisajiliwa kutoka Southampton kwa ada ya £31m na adds on ya £2.5m.
Ni mchezaji pekee Liverpool aliekua anacheza pale mbele kushoto, kulia na kati kwa mafanikio makubwa . Ifahamike wakati anasajiliwa Salah upande wa kulia alikua anacheza Mane lakini Klopp akampanga ahamie upande wa kushoto na akawa na matokeo safi kabisa, lakini pia alivyosajiliwa Diaz January 2022 Mane akahamishwe tena kutoka upande wa kushoto na kuhamia kucheza kati kwa mafanikio makubwa kabisa.

Rekodi yake Liverpool..
Win ratio ni 66.54%
Amesshinda gemu 179
Ametoa sare game 52
Amepoteza gemu 38.
Amecheza Mechi 196 za Ligi Kuu akifunga magoli 90 na kutoa assist 29 Liverpool.

Magoli na assist kwa kila msimu tangu ajiunge nasi ni..
EPL rekodi tangu atue Liverpool
2016/17... mechi 27 goli 13 assist 5
2017/18...mechi 29 goli 10 assist 7
2018/19...mechi 36 goli 22 assist 1
2019 /20...mechi 35 goli 18 assist 7
2020/21...mechi 35 goli 11 assist 7
2021/22...mechi 34 goli 16 assist 2.

UCL rekodi tangu atue Liverpool
2017/18 mechi 13 goli 10
2018/2019 mechi 13 goli 4
2019/2020 mechi 8 goli 2
2020/2021 mechi 10 goli 3
2021/2022 mechi 13 goli 5.

Katika UCL kwa Liverpool ana rekodi ya kipekee kabisa akiwa amezidiwa tu na CR7, Benzema na Lewandowski kufunga magoli mengi ya mtoano tangu 2016. Katika kipindi hicho amefunga asilimia 63 ya magoli ya mtoano Liverpool.

Akiwa Liverpool ameshinda yafuatayo
2017 August EPL player of the month
2019 March EPL player of the Month
2019 November EPL player of the month
2019 Champions League winner
2019 Super Cup winner
2019 Fifa World Club Cup winner
2019 EPL Golden Boot winner.
2019 /20 EPL Premier League winner
2022 Afcon trophy winner
2022 African player of the Year winner
2022 mchezaji bora wa mashindano ya Afcon.
2022 League Cup winner .
2022 FA Cup winner.

Alicheza mechi yake ya mwisho Liverpool tarehe 28/5/22.

Ameuzwa kwa heshima kubwa sana kwenda Bayern Munich kwa ada ya £35m ikiwa ni zaidi ya bei waliyomnunua Liverpool kutoka Southampton.

Bayern watalipa cash £27.5m,adds ni £7.5m.

Kila la heri mwamba wa Senegal 🇸🇳 hakika umetuwakilisha vyema sana Liverpool.

YNWA
Binafsi toka nianze kuwa fan wa Liverpool Sadio Mane& Daniel Agger ndio wachezaji niliowapenda.
 
Duu kweli sisi tunasindikiza wanao kula maisha yani Mwanasheria/Wakala anapata karibu tshs.19 billion.
😂😂😂😂😂Ngoja jamaa yetu MosDef azame kwa big boys table na sisi tuambulie vumbi ya hizo dolali aiseee yaaani mchezaji mmoja wanapata hivyo sasa huyo wakala Jorge Mendes ana wachezaji lukuki Ronaldo, Mourinho, Silva, Fabinho, Fabio nk jamaa kazi yake moja tu kusaka the highest bidder wa wachezaji wake ndio maana amekua moja ya wakala anaeaakwa na wachezaji wengi...

YNWA
 
Binafsi toka nianze kuwa fan wa Liverpool Sadio Mane& Daniel Agger ndio wachezaji niliowapenda.
Agger nakumbuka tulichomfanyia iliniuma sana yaaani hatukufanya fair hata kidogo maana nakumbuka Manchester City walileta ofa kwetu ya maana lakini Agger akasema mchana kweupe hana mpango wa kuhama timu atabakia Liverpool duuh msimu mmoja akanyimwa mkataba na kuambiwa atafute timu asepe zake yaaani iliniuma sana kiasi nikasema bora angewakumbalia Manchester City kuliko yaliyomtokea.

Mane duuh huyu hakuna cha kuongeza kuanzia kukumbali kuachilia jezi namba hali inavyotaka na kukumbali kuhama namba kutokana na mipango ya mwalimu yaaani alikua flexible kuanzia siku ya kwanza mpaka anasepa ni full professional...

Tetesi ni kwamba Bayern walikua tayari kuikacha hii dili na Mane moyo wake ulikua ni Bayern tu sasa Liverpool kwa kuheshimu mchango wa Mane na alivyoomba asepe akasake changamoto mpya Liverpool wakaona wasilete drama kumng'ang'ania Mane wakakumbali washushe bei kwa tofauti ya £7m ili Mane atimize ndoto yake.....

Ameodoka kwa heshima kubwa ndio maana mashabiki kidakidaki hawana hard feelings nae zaidi ya kum wish mema huko Bavarian.

YNWA
 
Labda Origi alikua hatoshi ila kwa usajili huu natumai mfumo utabadilika sasa .
4 2 3 1 Boby hapa hatakosekama uwepo wake utawaongezea ubora hawa wageni

Fab na Cantara kati halafu Diaz Boby Salah hafu mbele ndo Nunezi.

Baada ya ushindi asiache kuwaingiza hawa watoto Cavlnho na Eliot kuwajenge

Haka katoto kengine Ramsey bonge la mchezaji sijui itakuje na Kloop muoga wa ku roteti
Mkuu Fabio ndio silaha kuu ya 4 2 3 1 yaaani ili Klopp aje ki hivyo anahitaji mchezaji wa thread pass na baller mwenye mbio za kukimbia na mpira na kwa sasa best option ni Fabio..

My 4 2 3 1
Trent Konate VVD Robertson
Fabinho Thiago
Diaz Fabio Salah
Nunez...

Kwa mfumo huo kwanza ndio ulikua mfumo mkuu pale Benfica na dogo Nunez akicheza kwa mafanikio makubwa sana.... Ifahamike pale Benfica katika msimu mzima 4 3 3 walitumia mara moja au mbili hivyo dogo Nunez itabidi awe adaptable ama Klopp acheze na strength zake ili atumike vyema...

Thiago, Henderson ni over 31 hivyo hata intensity kwao itaanza kushuka sitegemei kuona Klopp akikomaa na Henderson, Thiago, Fabinho dakika 80 eti ndio anaingia Fabio au Jones. Kama hatusajili kiungo mpya basi hakuna tena wakati sahihi kama huu kuwaamini vijana wetu Elliott, Jones na Fabio... Naamini sasa wata step up vyema na kua integrated kwenye kikosi kwa kupata dakika za kutosha na ukizingatia sub zimeongezwa msimu ujao ni 5.

YNWA
 
Madrid hawakucheza tu kutaka kushinda uefa ,Kwan ukiangalia wachezaji kalibia wote walishachukua CL hivyo basi Carlo hakuwa na maneno ya kuweza kuwashawishi sana....

ila walivosikia huyo mbwa Salah analopoka mambo ya kulipa kisasi ndio kila mchezaji mishipa iliamuka na kutaka kuonesha dunia ,hapa Carlo alipata sababu ya kuwambia vijana wake kuwa " that f**king boys they want to make revenge,come on ,we can't tolerate such kind of embarrassment,we want to show the world that we own this trophy,"
 
Madrid hawakucheza tu kutaka kushinda uefa ,Kwan ukiangalia wachezaji kalibia wote walishachukua CL hivyo basi Carlo hakuwa na maneno ya kuweza kuwashawishi sana....

ila walivosikia huyo mbwa Salah analopoka mambo ya kulipa kisasi ndio kila mchezaji mishipa iliamuka na kutaka kuonesha dunia ,hapa Carlo alipata sababu ya kuwambia vijana wake kuwa " that f**king boys they want to make revenge,come on ,we can't tolerate such kind of embarrassment,we want to show the world that we own this trophy,"
😂😂😂😂 😆 😆 Rodriygo kwenye interview juzi anasema" Modric ni muuaji kipyenga cha mwisho kilivyopulizwa alimkimbilia Salah na kumwambia 'try again' kumpoza kwa maneno ya kejeli baada ya kumfariji alienda kumsindika mineno kuntu".Salah bora angekausha hata mimi mshindani wangu akianza kwa vijembe na vitisho sitomchukulia poa niaibike lazima nihakikishe maneno yake hayatimii.
 
Naomba picha ya wachezaji wakiwa wamenyanyua kombe la epl kabla hili la klopp alilowapa kipindi Cha corona mkuu
Thubutu yao hilo walilobeba wachambuzi wakubwa wa mpira duniani hawalitambui kama ni kombe la Epl bali wao wanalitambua kama ni kombe la Cpl (Corona Premier League)
IMG_20220619_080737.jpg
 
Mateo Kovavic akimuomba Bwana Gerrard ku shake hands wakati huo Mateo akowa bado ni chalii halafu ballboy

Leo Mateo ana more European Cups kumzid Bwana Steven ..

#CFC💙💙💙
 

Attachments

  • IMG_20220619_085133.jpg
    IMG_20220619_085133.jpg
    18.2 KB · Views: 17

Similar Discussions

Back
Top Bottom