Saido Mane the Legend...
Ndio alikua mchezaji wa kwanza ghali na wa kimkakati kusajiliwa na Klopp Liverpool.
Alisajiliwa Liverpool mwaka 2016 akicheza gemu yake ya kwanza 14/8/16.
Mane alisajiliwa kutoka Southampton kwa ada ya £31m na adds on ya £2.5m.
Ni mchezaji pekee Liverpool aliekua anacheza pale mbele kushoto, kulia na kati kwa mafanikio makubwa . Ifahamike wakati anasajiliwa Salah upande wa kulia alikua anacheza Mane lakini Klopp akampanga ahamie upande wa kushoto na akawa na matokeo safi kabisa, lakini pia alivyosajiliwa Diaz January 2022 Mane akahamishwe tena kutoka upande wa kushoto na kuhamia kucheza kati kwa mafanikio makubwa kabisa.
Rekodi yake Liverpool..
Win ratio ni 66.54%
Amesshinda gemu 179
Ametoa sare game 52
Amepoteza gemu 38.
Amecheza Mechi 196 za Ligi Kuu akifunga magoli 90 na kutoa assist 29 Liverpool.
Magoli na assist kwa kila msimu tangu ajiunge nasi ni..
EPL rekodi tangu atue Liverpool
2016/17... mechi 27 goli 13 assist 5
2017/18...mechi 29 goli 10 assist 7
2018/19...mechi 36 goli 22 assist 1
2019 /20...mechi 35 goli 18 assist 7
2020/21...mechi 35 goli 11 assist 7
2021/22...mechi 34 goli 16 assist 2.
UCL rekodi tangu atue Liverpool
2017/18 mechi 13 goli 10
2018/2019 mechi 13 goli 4
2019/2020 mechi 8 goli 2
2020/2021 mechi 10 goli 3
2021/2022 mechi 13 goli 5.
Katika UCL kwa Liverpool ana rekodi ya kipekee kabisa akiwa amezidiwa tu na CR7, Benzema na Lewandowski kufunga magoli mengi ya mtoano tangu 2016. Katika kipindi hicho amefunga asilimia 63 ya magoli ya mtoano Liverpool.
Akiwa Liverpool ameshinda yafuatayo
2017 August EPL player of the month
2019 March EPL player of the Month
2019 November EPL player of the month
2019 Champions League winner
2019 Super Cup winner
2019 Fifa World Club Cup winner
2019 EPL Golden Boot winner.
2019 /20 EPL Premier League winner
2022 Afcon trophy winner
2022 African player of the Year winner
2022 mchezaji bora wa mashindano ya Afcon.
2022 League Cup winner .
2022 FA Cup winner.
Alicheza mechi yake ya mwisho Liverpool tarehe 28/5/22.
Ameuzwa kwa heshima kubwa sana kwenda Bayern Munich kwa ada ya £35m ikiwa ni zaidi ya bei waliyomnunua Liverpool kutoka Southampton.
Bayern watalipa cash £27.5m,adds ni £7.5m.
Kila la heri mwamba wa Senegal

hakika umetuwakilisha vyema sana Liverpool.
YNWA