Duuhh Mane anapokea £100000? Ni ndogo sana ukilinganisha kazi anayoifanya
Mane moyo wangu mweupeeee aodoke tu kwa kweli. Hawa wachezaji ni professional lazima walipwe value for money.
Dogo Mane anajituma haumii hovyo hua hana makuu akiambiwa acheze kulia, kushoto au kati huyoo anasema powa twende kazi ila sasa mshahara wake anazidiwa mpaka na Antony Martial, Patey na wengi tu na huku akiwa fire tangu atoke Afcon hakamatiki lakini FSG wanakomaa na Salah tuu usije shangaa hata Diaz usajili wake ni kwa ajili ya kumuuza Mane. Yaaani tuna wamiliki wa ajabu sanaaa hawafahamu kwamba Arsenal, Manchester United, Chelsea ipo siku watakaa sawa na ushindani utakua mkali sana hivyo hii chance ya kushindana na Kipara pekee ilikua ya kuichukulia serious sokoni mwalimu apewe mpunga wa maaana. Kuna wachezaji wengi wa bei powa Uholanzi, Ufaransa nk ni suala la Klopp awezeshwe bila masharti ya sell to buy.
Tazama umri wa kikosi wachezaji ambao washavuka miaka 30 VVD, Firmino, Mane, Thiago, Henderson, Matip
Tazama umri hawa wanakaribia 30
Fabinho, Allison, Salah, Robbo, Keita, Ox
Mpaka hapo utaona hii cycle lazima mwalimu asaidiwe ili ku maintain ushindani klabuni na kwenye ligi.
Kwa Mane namtakia mema sana hakika amekaa miaka 6 kwetu kubwa zaidi alikuja mwenyewe bila kulazimishwa kwani alikua na ofa safi sana kutoka Manchester United lakini akawatosa na kutua Liverpool sasa tumpe heshima yake akapata changamoto mpya.
YNWA