Sasa hivi mambo yamebadilika sana ili kuchungua ubingwa wa EPL au UCL inabidi timu iwe na mentality ya kushinda kila mechi inabidi tiwe iwe na mentality ya Ugiant kama ilivyo Bayern Munich kupiga vitimu vyote nyumbani na ugenini. Na hili linawezekekama EPL, Guardiola ameproove hili kwa kutupilia mbali mambo ya kusema sijui EPL ni ngumu,sijui kushinda mechi karibia zote ni ngumu yeye hakujali hilo kwahiyo amejitengenezea Ugiant England. Liverpool inabidi muepukane na utamaduni wa kugawana na point na hizi timu mnazoziita top six ndo mchukue ubingwa, msimu huu mlikuwa vizuri sana lakini mkashindwa kuchukua point angalau tatu kwa City, Tottenham na Chelsea. Hamuwezi kuchukua ubingwa kwa kutegemea timu nyingine zimsimamishe mshindani wenu ili nyie mtwae ubingwa.