BARDIZBAH
JF-Expert Member
- Jan 11, 2017
- 5,935
- 11,778
Jamaa wapo kibiashara sana, ila kumuachia Salah au mane haitopendeza.Mkuu tuna wamiliki wachumi balaa. Amini usiamini huu ununuzi wa Diaz unamengi sana nyuma ya pazia aisee. Usije shangaa Salah, Mane wakanyimwa nyongeza ya mikataba yao ama ukaona Mane amepewa mkataba mpya na pengine wamlipe £180 au £200 kwa wiki na waongeze miaka miwili ina maana mpaka 2025.
Kwa Salah FSG wanatega hivi, Mbappe atasaini mkataba mpya PSG kama ndio FSG wanaweza kumuuza Salah Real Madrid, ama je Barcelona kuna pesa wanategemea je wanaweza kumshawishi Salah atue kwao.. FSG wanamtega Salah kwa kuangalia movement za wachezaji wengine ambao ni Mbappe na Haaland. Timu zenye uwezo wa madai ya Salah ni PSG, Real Madrid, Manchester City na Juventus labda kwa baadae akiona vipi Chelsea na Barcelona wakipata hela.
Hili sakata la Salah ndio kwanza asubuhi labda watonywe mapema movement za Mbappe na Halaand zipo hivi na hivi.
Firmino naona ni rahisi kupata kama akihitaji kwa vile dogo hua hana makuu hata ya dakika uwajani hanuni asipopangwa wala sub na pia hata mshahara wake sio ishu kubwa kwa £180k,wakimpa miaka 2 inamtosha.
YNWA



