Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Adjustments.jpg
 
Huu ndio ukweli. Maldini ni mzoefu na mshindi ni proper professional mpaka anayasema haya hajabahatisha. Uzuri hata sisi tunafahamu Manchester City are the team to beat ili kunyanyua kwapa you got to beat the best.

Thanks Maldini ni washidani wachache sana wataelewa hili. Kuingia uwajani ndani ya siku 7 mechi 3 na kutoka na ushindi huku uwaja ukiwa umesheheni mashabiki aidha uwe nyumbani na ugenini na tukashinda inahitaji ukomavu na uvumilivu . Mfano mzuri ni gemu ya Wolverhampton ule ushindi sio kawaida.

Tupo tayari tunakwenda mdogo mdogo mpaka mwisho wa msimu tuna imani na vijana wetu watatupa heshima kubwa.

YNWA
 
Joel Matip.

Huyu mwamba amezaliwa Bochum Ujeremani.

Alizaliwa 18/8/1991 na kupewa majina Job Joel Andre Matip.

Wazazi ni Baba Jean Matip raia wa Cameron na Mamake Eva Maria Matip raia wa Ujeremani.

Amezaliwa na ndugu zake wawili ambao ni Rebecca Matip na Martin Matip.

Binamu wake Joseph Desire aliechezea Cameron.

Upande wa familia ya Mamake ni wasomi upande wa medical na upande wa Baba ni wapenzi wa mpira.

Alianza kusoma Gesamtshulle Berger Field School na baadae SC Weitmar 45 1995 mpaka 1997 kisa VFL Bochum 1997 mpaka 2000.

Akiwa na miaka 9 alijiunga na Schalke 04 baada ya kufanikiwa majaribio mwaka 2000.

Alicheza mechi yake ya kwanza kwa senior team ya Schalke O4 vs Bayern Munich mwaka 2009 na akapata tuzo ya MOTM.

Alikaa Schalke 04 misimu 7 akicheza mechi 258 na akifunga goli 23.

Klopp kwa mara ya kwanza aliona umwamba wa huyu jamaa mwaka 2012 walivyokutana Schalke 04 vs Dortmund fainali ya DFL Super Cup na Schalke 04 wakashinda.

Baada ya kucheza Schalke 04 kutoongeza mkataba na kutafuta new challenge. Saini yake ilikua adimu sana lakini simu moja tu ya Klopp alimshawishi ajiunge na majogoo wa Liverpool mwaka 2016 pindi mkataba wake ulivyoisha Schalke 04.

Key Poins Matip
*ni Mcameroon wa pili kuchezea Liverpool baaya ya Rigobert Song.

* Anacheza beki wa kati kulia.

* Aliwakilisha Cameron kombe la Dunia 2010 na 2014. Alicheza mechi 27 za Kimataifa akifunga goli 1.

* Alistaafu mechi za Kimataifa mwaka 2015.

* Assist yake ya dakika 87 kwa Origi alitupa ubingwa wa Ulaya fainali dhidi ya Tottenham pale Wanda Metropolitano.

* Akiwa Liverpool ameshinda
-UCL 2019.
-Super Cup 2019.
-Epl Trophy 2020.

* Ni jamaa asiependa makuu wala haishi maisha ya ki supa staa. Anaedesha gari ya kawaida tu Mercedes Benz sio special edition.

* Mwaka 2020 alimuoa mchumba wake wa miaka mingi Larissa Stollenwerk na mwaka huu 2021 wakapata mtoto wa kwanza June, a boy.

* Japo majeruhi hayachezi mbali na huyu mwamba Klopp bado anamwamini na ndio maana mkataba ni mrefu tu mpaka 2024 Juni. Alisaini upya 2019 huo mkataba.

* Rumoured Salary ni £100,000 kwa wiki.

* strength ni accuracy in passes, monster in aerial duels, fearless to put his body in danger.

* Ana miaka 30. Uzito ana kilo 90. Mara nyingi anatumia mguu wa kulia.

* Amecheza mechi 138 Liverpool akifunga magoli 6.

* Mwaka 2019, a Twitter account, "No Context Joel Matip" was created, which took clips of Matip's on-field antics and turned them into GIFs, memes and short videos. As of 2021, the account has over 68,000 followers, including Matip's team-mates Virgil Van Dijk and Alisson nk. Hii itaanza kumpa ela za matangazo huyu mwamba.


* Amecheza mechi 106 EPL akishinda 69 kupoteza 9 na kutoa sare 28. Akifunga magoli 5.

Huyo ndio Mwamba Joel aka Jimmy Matip in brief.

YNWA
Cc Saint Anne.

YNWA
 
Wanamtimua sasahivi
Shinda iliyopo pale sio Benitez tu ni kubwa kuliko Benitez mwenyewe kayakuta aisee hata wakimtimua watakua wamemtoa kafara tu.

Ishu kuu inaanza kwenye recruitment ya wachezaji kabla ya Benitez kutua. Ina maana director wa mpira Marcel Brands amewajibika na kuachia ngazi. Huo endapo wakituliza akili kupata mtu sahihu itakua mwanzo mwema kwao kutoka walipo.

YNWA
 
Hello Family.

As we approach X - Mass, I would like to take this opportunity to thank you guys for keeping this forum (family) active, in one or more ways this thread has been all to me, you guys are awesome.

There are times I almost lost it, but the theme You Will Never Walk Alone made the meaning, you all supported me in one or more ways to get to this, thank you guys.

NOTE: Nitatoa jezi tatu kwa members tofauti Xmass hii (jezi kwa bei za Kariakoo 25,000/- to 35,000/-), first come first serve basis. Unachotakiwa ni ku-quote hii post kwamba unahitaji jezi hiyo, watu wa tatu wa mwanzo ndo watakao pata. Tutajadili size na wahusika na
namna ya kufikiana.

Again, thank you guys.

YNWA
Nadhani sitakosa kuwepo kwenye hili la jezi hata kwa upendeleo boss..ha ha ha ha.
 
Baada ya kubondwa na westham nasikia ulikimbilia uzi wa battle kati ya Nairobi na Dar es salam huku hukuonekana kabisa labda MMU kwahyo saiv umerudi tena? Na mpo nafasi ya ngapi?
Mkuu suala la nafasi lisikupe tabu ..maana arse8 Kila msimu anaanza wa Kwanza Ila mwishowe anapoteana. Kwa hii desemba imeisha? Sisi ni mabingwa tayari hapa tunakamilisha ratiba tu.

Sasa chagueni moja, msuke ama mynyoe ..Yani asa nyie livakuku tukikutana Tena wanabamiza bao za kutosha.

Wewe huyiogopi Chelsea,??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom