LIVERPOOL LIVERPOOL LIVERPOOL
Nlichogundua kuhusu LIVERPOOL ni kwamba wachezaji wetu na benchi zima wapo kwenye ARI KUBWA msimu huu
Alafu pia kuna AMANI na FURAHA Pia kuna UMOJA tukiendelea hivi msimu huu kuna legend atafungwa tena 5 zingine nadhani hakuna timu yoyote ile Barani ULAYA ambayo inaweza kutukaribia UCL Wapinzani wetu ni Real Madrid na Hawa Mabaharia Wakijerumani Bayen Munich Hamna timu nyingine narudia tena kusema HAMNA TIMU Nyingine tena ambayo ina uwezo wa kutusimamisha labda sisi wenyewe tuwe wazembe ila kama mambo yatakwenda hivi tutegemee mazuri LIVERPOOL
Mkuu mbona hujayesema hayo yote weekend iliyopita Baada ya mechi dhidi ya Brighton?
Mkuu tatizo la timu yetu kwa sasa ni kiungo pale kati,pale kati wakiwa Henderson na Fabinho ,mtu wa tatu hapo weka mtu yoyote yule hata wewe ingia hapo lazima tupate ushindi tu ushindi goli tunaanza 2 ,ikiwa hivyo hapo huwezi kulaumu beki wala kulaumu kipa,ndio kilichotokea kwa jana.
Mechi na Brighton tulicheza hovyo sana mido walikuwa ox,Jones na Henderson sasa kwa mido hiyo hapo mkabaji ni Henderson tu hao wengine ni mabingwa wa kupoteza mipira.
Kwa namna tulivyocheza jana kwa yule ambae hajaangalia mpira kwa sasa hakuna timu ya kuifunga
LIVERPOOL, ligi ambazo watakuwa wanapangwa hao watu Henderson na Fabinho natangaza rasmi liverpool tunabeba Epl na ucl msimu wa 2021/2022
Me nimeanza rasmi jana kuanza maandalizi ya kushangilia ubingwa wa ucl na Epl msimu huu wa 2021/2022.
Kwa namna timu zingine navyoziangaliaga zinavyocheza hakuna timu ya kumsumbua Liverpool kwa sasa,na ndio maana mpaka saizi hakuna timu uliyoweza kuchukua point tatu kwa Liverpool.
Mkuu sio legend mmoja wengi watakula hizo goli 5.
Mkuu nashukuru kwakuliona hilo Jana kama mimi .kama na wewe uliliona hilo inaonesha pia kuna ukweli ndani yake,hakuna timu ya kumsumbua Liverpool kwa sasa.
kuna muda nikawa nawaza timu nyingine ya kutusumbua ni ipi ? sijaona kwa sasa ulaya kwa huwezo ule na tuko siriaz sana Na ubingwa msimu huu.
Kwa sasa ucl hapo nani sijui atataka kukutana na sisi? Maana sasa hivi dozi yetu ya magoli tunaanza kuesabia goli 2 nakuendelea kila mechi mashindano yote.