Jana baada ya game niliingia website ya BBC, Match of The Day.
Kuna polls nadhani ilifanywa na BBC wenyewe kwa mashabiki wa Liverpool kuhusu Jota kuwa starter nafasi ya Bobby.
Around 5,000 wanataka Jota aanze, na ni 1,000 pekee wanaotaka aendelee kuanzia benchi.
Ninachokiona hapa kelele za mashabiki zinaweza kulipa, Klopp akafanya mabadiliko.
Pia interview ya Klopp (post match) alisema, "He's much better than I thought he would be and that's really impressive,"
"He's an exceptional talent. He has the speed, physicality, technique, and he's both-footed."
Hii ni indicator ya Klopp kuanza kumwelewa Jota na ikibidi afanye jambo nafasi ya Bobby.
La sivyo ni mpaka tupoteze poteze mechi kadhaa ndo mabadiliko yafanyike kama ilovyokuwa kwa Fabinho na Hendo (kumchezesha Hendo namba 6 kulitucost ubingwa msimu ule).