Liverpool FC (The Reds) | Special Thread


1.Sio jana tu siku zote Liverpool wanacheza vizuri first half second half wanakuwa wabovu

2.Real Madrid huwa hawachezi vizuri first half second half wanakuwa hatari

So ukicheza na Liverpool hakikisha wasikufunge first ikifika second half washambulie lazima utawafunga.First half Marcelo huwa anacheza kama beki but second half anakuwa winga
 


Hapa Kwa Ederson Nakuunga Mkono 100% Huyu Jamaa Hamna Kitu Ni Sawa na Karius.

Siku Beki Akikosea Ederson Huumbuka! Na Siku Ya Kuumbuka Ederson ipo Njiani Kama Ulivyosema..
 
Kwa Nilichokiona Katika Msimu Uliomalizika Wa 2017/18

√ Timu inahitaji Usajili Wa Minimum ya Wachezaji 5 Kwa Two Windows (Summer & Winter)

√ Nafasi Zinazohitajika Kusajiliwa Ni:
β€’ Goal Keeper
β€’ Centre Back (Partner Wa VVD)
β€’ Defensive Midfielder
β€’ Attacking Midfielder
β€’ Striker

* Formation inatulazimu iwe:

New GK
TAA - (New CB) - VVD - ROBBO

Keita - (New DM) - BOBBY

SALAH - (New STRIKER) - MANE


Kwenye Hili Eneo La Midfield Ndiyo Linatakiwa Lifanyiwe Mabadiliko Kwa 100%. Tuweni Wakweli Huwezi Shinda Taji Kwa Mido ya 'GINI - HENDO - MILNER'. Hawa Wote Watatu Wanahitaji Kufanyiwa Mabadiliko.

√ Kuna Wachezaji Ni Lazima Waruhusiwe Kuondoka:
β€’ Lallana
β€’ Mignolet
β€’ Clyne
β€’ Klavan
β€’ Ings
β€’ Origi
β€’ Sturridge

Hapo tutakuwa Angalau Tunaweza Kuonesha Ushindani Wa Kuwa Tuko Tayari Kubeba Silverware.

Lakini Kwa Kikosi Hichi Cha Kuwa Atoke Salah Aingie Lallana,
Atoke Mane Aingie Solanke! Basi Tusidanganyane Hatuwezi Beba Kombe Hata La Ndondo Cup.

√ Pia Hatuwezi Shinda Kombe Kwakumtegemea Salah Pekee.

MY TAKE: NI JAMBO LA AIBU KWA MSHABIKI WA LIVERPOOL KULALAMIKA TUMEFUNGWA KISA KAUMIA SALA! Ridiculous!!!!!

Hili Jukumu letu Kuwa na Back up Ya Kila Mchezaji! Backup Ya Salah Mara Nyingi Huwa Ni Solanke au Ings ambao Hawa Wote Ni Shitholes.

Kwahiyo Tusilete Excuse Yoyote Tunapopoteza Mchezo Bali Tukubali Kuwa Hatupati Mafanikio Kwa Sababu Ya UFINYU WA KIKOSI CHETU (Depth).

Naamini Klopp Atajifunza Na Kufanya Mageuzi.
 
Wengine chuki tu zimewajaa achana nao mkuu. Timu imefika hadi fainali then wanaibeza wana akili sawasawa kweli hao,
Kwani Madrid dakika 20 za mwanzo kuna mchezo gani kacheza dhidi ya kuja kusaidia kulinda.

Mpira ni dkk90 (normal time). Kwa hiyo kama mchezaji unatakiwa kuwa mchezoni kwa DKK zote mara baada ya kipenga cha kwanza kupulizwa. Usijifiche nyuma ya dkk20 kuamua sura ya mchezo wa Jana. Liverpool wamekuwa na msimu mzuri lakini bado wana safari ndefu kidogo kujenga kikosi bora na imara. Poleni sana.
 
Ngwaba umepanic sana. Relax kwanza Kaka
Madrid hii Pamoja na kuwa na Top players wengi lakini akikosekana Key player mmoja tu kama Ramos timu ina teteleka tumeona game na Juve timu ilivyo struggle
Barcelona wana quality player wengi lakini mechi ya Roma Messi kapotezwa timu nzima ikapotea
Sallah ndio key player wa timu kwa sasa mipango yote ya ushindi wa timu .Movement za timu kwenye upande wa attack inaanzia kwake
 
Ndo ulisema firminho aanze Brazil? Nadhani Usha pata jibu
 
Goli la Mane ni la dakika ya ngapi?
 
Ni kwa sababu Mo anacheza kama front 3 ina maana muda wote anakuwa mbele akisubiri mipira katika mfumo wa 4.3.3 kutoka kwake kuingia Lalana ikabidi warudi 4.4.2 hii inampa nafasi Marcelo nafasi ya kupanda maana beki za kati Madrid wanakaa na Firminho tu na midfield wana cover gape la Marcelo. kucheza na team 4.3.3 inakuwa ngumu kwa fullback kupanda kila mara ila 4.4.2 ukiwa na midfield wazuri utajikuta kila dakika uko mbele. ile game ni wazi kutoka kwa Salah tu ndio wakaanza kufika mbele. dakika zote alozikuwepo Mo Real walikuwa hawatoki nyuma wakihofia kuacha mianya sababu ya speed. ila 4.4.2 wakaweza kucheza highline inampa Marcelo chance hata yule Nacho akawa anaenda mbele.
 
Ndo ulisema firminho aanze Brazil? Nadhani Usha pata jibu
Firminho sio number 9 ana fit zaidi katika mfumo wa 4.3.3 sababu wakiwa watatu wanakuwa wanazunguka wote wa tatu kilichotokea jana baada ya kuingia Lalana ikabidi waende 4.4.2 ina maana ikabidi awe kati ikawa ngumu kwake kufanya kitu hakuna movement. unakumbuka siku Conte alipomweka Hazard kama number 9? Hazard akapotea maana sio style yake ni lazima atokee pembeni lakini haina maana Hazard akawa mchezaji mbaya kwa siku moja. Firminho wakati anakuja Liv hakuwa typical #9 alikuwa kama winger hivi sio kama kina Drogba au Costa. ndio maana kabla hajatoka Mo firminho alikuwa anapenyeza mipira.
 
Kitu kimoja ni lazima Live tuwe na 16 players wote viwango na zaidi kipa ni lazima na lazima tupate centre forward#9 ili tuwe na system 2 tunaweza kwenda 4.3.3 au 4.5.1 Firminho akacheza deep kama midfield Salah na Mane wings halafu tuwe na mtu striker number 9 type za kina Costa na Drogba. tukiwa home tunaenda 4.3.3
 
Ni watu wawili tofauti.
Kwahiyo Jombaa huyo aliyeingia alikua anasimama kama mti, hakabi, hashambulii, hashambulii.
Hata akipata mpira basi Madrid hawamkabi?????
Acheni mambo ya kiboya. Ladecima Halla Madrid
Wewe ndo boya,Salaah ana magoli mangapi,assist ngapi na alikuwa threat kiasi gani hadi umlinganishe na Lalana.Salah ni world class player halingani siyo na lalana tuu bali kikosi chote cha Liverpool anayemkaribia ni Mane na Firmino.Siyo lazima ukubaliane na mimi kama hutak unaacha.Mwenye akili hawezi kupinga.
 
Mkuu hilo jamaa achana nalo ,kule kwetu mijitu kama hayo huwa tunayaita Entabani.Linakomalia ujinga.
 

Fainali ya sita akifeli, soma takwimu vizuri. Labda kwa Liverpool pekee
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…