Timu Ambazo ndiyo Pekee Katika Historia Ya [HASHTAG]#UCL[/HASHTAG] zilizobeba Kombe Hilo na Kukabidhiwa Kombe Original na sio Replica Ni:-
√ Real Madrid.
√ Ajax after their third consecutive title in 1973 .
√ Bayern Munich after their third consecutive title in 1976 .
√ Milan after their fifth title in
1994 .
√ Liverpool after their fifth title in
2005 .
Hao Walikabidhiwa Kombe Original Kabisa Kulingana Na Sheria Ya Zamani Ya UEFA Kuwa Timu inaposhinda Kombe hilo MARA 3 MFULULIZO kama alivyofanya Real, Bayern na Ajax au Timu iliyotimiza idadi Ya Kushinda MARA 5 Kombe Hilo Kama Walivyofanya AC Milan na Liverpool Basi Anakabidhiwa Kombe Hilo Original Na Kuwa Mali Yake.
Lakini Sheria Hii Kwa Sasa Haitumiki tena na Ndiyo Mana Barcelona aliposhinda Kwa Mara Ya 5 Mwaka 2015 hakupewa Kombe Hilo Original Kuwa La Kwake.
Kwahiyo Kama Hupewi Kombe Original timu inaposhindwa inapewa Nini?
Ni Kwamba Timu inaposhinda #CL Basi inakabidhiwa Kombe Original na Kukaa nalo Kwa Miezi 10 tu. Baadae Wanalirudisha na Kukabidhiwa Kombe ambalo Ni Replica/Copy mfano Wa Hilo Original ndiyo Timu inakwenda Kulihifadhi Klabuni Kwake, Kwani Hairuhusiwi tena Kwa Timu Yoyote Kubeba Kombe hilo na Kuwa Mali Yake Hata Kama itabeba Mara 10 mfululizo.
Pia Timu inaruhusiwa Kutengeneza Wenyewe Hiyo Replica ya Kombe lakini Ni Lazima ikidhi Masharti Ya UEFA ambayo Ni Lazima liwe na Muundo hulehule Wa Kombe Original, Pia lisifikie au Kuzidi Ukubwa Wa Kombe Original (Lifikie asilimia 80% tu ya Ukubwa Wa Kombe Original).
FINALY, LIVERPOOL ITABAKIA KUWA NI TIMU YA MWISHO KATIKA SAYARI HII KUBEBA KOMBE ORIGINAL LA [HASHTAG]#UCL[/HASHTAG] NA KUWA MALI YAKE