Kuendeleza! kukuza! wapi na wapi?
Salah katengenezwa Chelsea kakulia Roma, Sadio Mane Southampton kaja Liverpool kashekomaa, Oxlade-Chamberlain kaibukia Southampton na kukulia Arsenal, Roberto Firmino katengenezwa na Hoffenheim ya bundesliga kabla ya kuja Liverpool. Timu inayosifika kwa kuwatengeneza wachezaji ni Arsenal tu na hizi timu ndogo ndogo, hizi timu kubwa ni buyers wa ready-made players tu wacha kumuonea Jose bure.
Pep kawanunua wengi ready made ndio maana mwaka huu mambo imemnyookea, Conte kanyimwa mshiko wa kuingia dukani na kidogo alichopewa kashindwa kununua waliokomaa ona matokeo ovyo kabisa, Wenga na kubana kwake matumizi kwa kutengeneza vipaji kila mwaka kombe analisikia redioni.
Barca na RM timu zinazoongoza kwa kununua wachezaji waliotengenezwa ona matokeo yao yalivyo mazuri.
Siku Liverpool ikijikita kutenegenza na kuendeleza internal youngster itakuwa kama Arsenal au hizo timu ndogondogo kama akina Sounhamtom na everton an wengineo ambao wao wakishatengeneza wanaume wenye mshiko wanachukua na kuwatumia kubeba makombe