KadaMpinzani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2007
- 3,715
- 93
Taarifa sahihi ni kuwa wa break wanarudi muda mfupi ujao kuchagua wajumbe wa NEC viti 20 (kundi la kifo) sasa hizo habari za katibu mkuu mpya ni mazingaombwe tu...
masatu,
mie nimo ndani..
Are U sure?... ama ndio katika kutufunga kamba sisi tusojua/ona yanayojiri CCM Dodoma.Hizi habari za Makamba nje sio sahihi. Katibu mkuu anapendezwa na Mwenyekiti na CC inamthibitisha. Kikao cha leo ni cha Mkutano mkuu ambao unachagua wajumbe wa NEC.
Masatu,
Are U sure?... ama ndio katika kutufunga kamba sisi tusojua/ona yanayojiri CCM Dodoma.
Kwa nini mhangaike hivi wakati habari zote tutazipata tu kupitia vyombo halali, au Invisible anawalipa kwa kuleta mabreaking news?
Masatu,
Uko right, habari ya katibu mkuu haiwezi kupatikana leo.
Katibu wa CCM anachaguliwa kwenye NEC mpya, yaani baada ya NEC kuchaguliwa, watakaa na ndio watamchagua katibu mkuu baada ya kupendekezwa na JK.
Sasa hata NEC haijaundwa, tayari waganga wa mvua wanasema Makamba kaondolewa?
Labda kama huo ni utabiri lakini sio habari ya kweli.
Kazi,
Mjadala mzuri. Katika ilani kumi za Chama alizotaja. Ameongela moja baada ya nyingine na kuelezea zilivyotekelezwa so far.
Ukiangalia kwa makini ameongelea kuanzia walivyodhibiti Ujambazi mpaka tatizo la Umeme.
Kwa ufupi ni kuwa katoa mifano hai katika kila kipengele.
Yaani ilikuwa hotuba safi sana kaka, itafute uisome.
Mimi nimeleta to hints, ila kaka mimi huwa natazama pande zote za shillingi ndio maana utaona kuwa nimesema, HAKUONGELEA KWANINI MIKATABA NI SIRI. Ila kaongela kuundwa kwa tume huru, nyinyi wapinzani na viongozi wa dini mtakuwemo!
Maneno yako mazito sana,hata mimi nayaona yamejikita katika matokeo yatakayojiri ambayo ndio yatakayo isambaratisha CCM,wenyewe kwa wenyewe,Ukichukulia kauli ya Muungwana akisema Wengine hata wakishindwa kwa kura moja halali, wanalalamika ,hapa pana ashiria matatizo ambayo amekwisha tonywa na alizidi pale alipo wapiga jembe wengine kwa kuchimba mkwala alisema Wale wanaotumia fedha zao zitapotea bure.Hapo kunaonyesha kuna watu ambao wanatumia fedha nyingi kusaka nafasi za NEC,aidha alikuwa akionyesha dalili za wazi watakaopita hawatakuwa na faida ndani ya chama zaidi ya kutafuta njia za kurudisha fedha zao,na hivyo chama kitapambana naohilo kundi la watu 20 hapo ndio watu watakapochoka na hao watakaotajwa ! subirini mtasikia mtandao umerudi ??
FD!Kazi,
Kuhusu kuchukua hatua amesema kesi ya Mahalu (hakumtaja) ipo mahakamani. Na tutegemee kesi 38. Kuna viongozi 38 wa serikali wanahojiwa sasa hivi...
Is it not a good move?, amesema kwa sasa even ukituma SMS wanaifanyia kazi, yaani hata majungu wanayafanyia kazi, kikieleweka ni mahakamani.
Alichotakiwa azungumze mambo ya Chama chake na si mambo ya Serikali,maana ameonekana akilihutubia Taifa na wanachama waliokuwepo ndani ya ukumbi sijui amewapiga chenga,au alijisahau na kuona Tanzania nzima ni ya wana CCM kumbe yupo ndani ya ukumbi na wenzetu,ila mfahamuni Muungwana anachosema sicho anachokitenda,ndipo hapo amezungumza mengine kumbe ana yake mengine ,tusubiri matokeo.Kazi,
Mjadala mzuri. Katika ilani kumi za Chama alizotaja. Ameongela moja baada ya nyingine na kuelezea zilivyotekelezwa so far.
Ukiangalia kwa makini ameongelea kuanzia walivyodhibiti Ujambazi mpaka tatizo la Umeme.
Kwa ufupi ni kuwa katoa mifano hai katika kila kipengele.
Yaani ilikuwa hotuba safi sana kaka, itafute uisome.
Mimi nimeleta to hints, ila kaka mimi huwa natazama pande zote za shillingi ndio maana utaona kuwa nimesema, HAKUONGELEA KWANINI MIKATABA NI SIRI. Ila kaongela kuundwa kwa tume huru, nyinyi wapinzani na viongozi wa dini mtakuwemo!.
kada stay tuned,HIVI RUSHWA ITAISHA LINI?
Naomba niseme kidogo. Nimekuwa mfuatiliaji wa karibu wa JF kwa karibia mwaka. Nimegundua kwamba jamboforums kuna rangi nyingi sana when it comes to politics in Tanzania. Muhimu zaidi, wengi wa Jamboforums wanaonyesha bado wana imani na chama chao cha mapinduzi kwani wakati wa chaguzi hizi huwa wanakuwa wana base hoja zao zaidi on nini kitaimarisha au kuvunja chama. Ukweli huu huwa unazidi kujiidhirsha nyakati hizi za chaguzi ambapo wengi huwa wanakuwa na preferences za on nani awe au asiwe kiongozi ndani cha chama cha mapinduzi na kusahau kabisa how hizi development can or should shape upinzani. Mbali zaidi, kama kawaida, siasa za kusengenyana na kuanikana na vilevile kutafutiana kashfa humu jamboforums huwa hazikawii kujitokeza baada ya chaguzi. Hakika nyakazi za chaguzi za ccm ni muda mzuri sana wa kuchambua msimamo wa wana jamboforums wengi sana. wengi hawapo consisent na misimamo yao ya kisiasa. Hili ni bayana kama ukitumia muda wako kidogo kuangalia historia ya postings za watu kadhaa humu over time. In other words, wengi humu hawana dira. tusubiri matokeo ya NEC yapite na tutaona haya kwa mara nyingine tena.
Yeah. Kusuhu mambo ya mafisadi kashamaliza. Makofi leo amna. Hata JK akisema CCM Oyee. Lakini wanaorespond ni kidogo. angalia nyuso za makada!