Live: Kizota Dodoma

Live: Kizota Dodoma

  • Thread starter Thread starter MegaPyne
  • Start date Start date
Komba, Kopa na Asha Baraka ni wapiga porojo na propaganda...!! NEC ikichoka na mikakati wao kazi yao nikuwaburudisha...
 
Mtanzania na Dua na Yeboyebo,

Sikuwa nikigombea, nilikuwa mpambe wa wagombea watatu, lengo langu kuu ilikuwa ni kuwapigia debe na kuangalia mwenendo wa kampeni kwa ujumla. Nasikitika mmoja wapo amekosa ni kijana.

Wawili wamepeta, mmoja toka kundi la wanaume bara na mmoja kijana.

Ushindi ni ushindi tu, ila sikufurahia baadhi ya mambo.
Nipo Dar kwa sasa, yaani toka jana jioni.

Asanteni waliokuwa wananiombea mema!
 
Mtanzania,

Yes, huyohuyo unayemfikiria kadondoka. Ila wawili wamepeta. Mmoja kutoka kundi la UVCCM.

Bado tutasherekea tu wikiendi hii!
 
Lakini naomba kuwatetea wapiga ngoma[Kopa, Asha baraka,,, maana bwana ndio composition ya jamii!!! ] sio kila mahali tunaoakina Kitila!!!

On another note, Natamani kumwona Katibu Mkuu, mmama!!!
 
YES.ndio mkuu


Basi bana. Nichukue nafasi kuwapongeza sana wapiga kura wa CCM kwa kukubali ombi letu sisi wapinzani la kuwakataa Tambwe na Ngawaiya. Hii liwe fundisho kwa wanasiasa wengine wa upinzani wanaotaka kutumia upinzani kama malisho ya kukuza soko lao huko CCM. Safi sana. Mmefanya kazi nzuri. Kariubuni sasa tuendelee kupambana kifikra katika uwanja wa siasa. Mjue tu kuwa siasa za Tanzania nje ya CCM zimebadilika, zinahitaji akili na sio ujanjaujanja na porojo kama ilivyo huko kwenu katika CCM. Hakuna njia ya mkato, lazima kujiandaa na tena kujisomea hasa, hakuna longolongo. Kila la heri.
 
FD ilikuwaje mgombea wako akadondoka? au hukumpigia kampeni za kutosha?
 
Jamani kwenye kundi la bara hakuna mwanamama hata mmoja...heri ya kundi la Zanzibar walau kuna wadada wachache...

Wanataka usawa wakati waoga!
Hata kugombea, mwanamke alikuwa Shyrose tu.
 
Huyu ana uhusiano wowote na Wilbroad Slaa?



Na John Daniel, Dodoma


Mgombea mwingine Diwani wa Ukonga, Dar es Salaam Bw. Jerry Slaa aliomba asihukumiwe kwa dhambi isiyo yake kutokana na jina lake la mwisho kufanana na mwanasiasa machahari wa kambi ya upinzani ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbrod Slaa

Alijitetea kwamba hana uhusiano wowote na mwanasiasa hivyo anaomba achague ili atoe mchango wake kwa CCM.

MAJIRA-05/11/2007
 
Shukran kwa habari za Dodoma, tunaomba mtumalizie na kiporo cha Katibu Mkuu sasa maana tuliambiwa "kapatikana" toka jana
 
Sasa naona tupate list ya walioshindwa na kielelezo cha watu hao kushindwa kuwa wajumbe wa NEC etc
 
Back
Top Bottom