Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 576
- 1,626
Lissu ameyasema hayo baada ya kuulizwa swali kwenye kipindi cha Clouds 360 ambapo mtangazaji alimuuliza Lissu yupo upande gani sababu mahasimu wake wa kisiasa wamekuwa wakimtuhumu kuwa supporter wa mapenzi ya jinsia moja kwakuwa anakaa ulaya.
Lissu amesema hizo ni siasa za maji taka na kwamba hajawahi kusema popote kuwa anaunga mkono mapenzi ya jinsia moja.
Anasema jambo hili liliibuliwa alipojibu swali kwenye kipindi cha Hard Talk BBC ambapo alisema mambo ya faragha serikali haitakiwi kuingilia na kwamba nchi ina katiba inayosema serikali hairuhusiwi chumbani.
Akielezea msimamo wake juu ya jambo hili Lissu amesema, "Watu wenye utamaduni huo waendelee na utamaduni wao, sisi wenye utamaduni tofauti tuendelee na utamaduni wetu, sheria na tamaduni zetu haziruhusu ushoga hivyo tuendelee na utamaduni wetu, siungi mkono ushoga."