Marekani yalaumiwa kuingilia mambo ya ndani kwa kupinga sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ya Uganda

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG11460314959.JPG
Bunge la Uganda hivi karibuni lilipitisha mswada kuhusu mapenzi ya jinsia moja, ambapo kufuatia muswada huo, watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja nchini humo watakabiliwa na kifungo au faini. Mswada huo umepingwa vikali na nchi za Magharibi zinazoongozwa na Marekani, na Marekani kwa mara nyingine tena ilinyoosha mkono wake katika masuala ya ndani ya nchi za Afrika.

Mapenzi ya jinsia moja yamepigwa marufuku nchini Uganda tangu mwaka 1902. Mara hii, mswada huo ulipitishwa bungeni kwa kura 387 za ndiyo na 2 tu za hapana. Hapo awali, spika wa bunge la Uganda Anita Annet Among, alisema mswada huo unalenga kulinda “maadili ya thamani na utamaduni” wa nchi hiyo. Sasa mswada huo umekabidhiwa kwa Rais Yoweri Museveni wa Uganda, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akihimiza hatua za kupinga mapenzi ya jinsia moja, hivyo anatarajiwa kuuidhinisha haraka.

Kupitishwa kwa mswada huo dhidi ya wapenzi wa jinsia moja kumepigwa vikali na Marekani. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameitaka serikali ya Uganda “kutafakari upya kwa umakini zaidi utekelezaji wa sheria hiyo”, akisema itadhoofisha haki za binadamu za watu wa Uganda. Msemaji wa Ikulu ya Marekani Karine Jean-Pierre amesema mswada huo utatishia mapambano dhidi ya UKIMWI na kuathiri utalii na uwekezaji nchini Uganda. Msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa la Marekani John Kirby, ameitishia Uganda moja kwa moja, akisema kutekelezwa kwa sheria hiyo kunaweza kuleta athari za kiuchumi na kifedha, akimaanisha kwamba, Marekani itaiadhibu Uganda kwa kupunguza misaada, kufuta ushirikiano wa kiuchumi, na hata kuiwekea vikwazo vya kiuchumi.

Kitendo hiki cha umwamba cha Marekani kimelaaniwa na nchi za Afrika. Rais Museveni wa Uganda amesema, nchi za Magharibi zinapaswa kuacha kulazimisha nchi nyingine zifanye mambo zisizoyataka, huku Rais wa Kenya William Ruto pia akisisitiza kuwa, mapenzi ya jinsia moja hayana nafasi katika nchi yake. Baadhi ya wanaharakati wa kijamii barani Afrika pia wamejitokeza kuzishutumu nchi za Magharibi kwa “ubeberu wa kitamaduni”, na kuzitaka wajifunze kuheshimu maadili ya Kiafrika badala ya kulazimisha kuiga vitendo vyao visivyofaa.

Kwa nchi za Afrika, mapenzi ya jinsia moja ni suala nyeti na tatanishi kutokana na sababu za kidini na kiutamaduni. Wakati nchi za Magharibi zinapozidi kukubali vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, watu wengi barani Afrika bado hawawezi kuvipokea. Hadi sasa zaidi ya nchi 30 za Afrika ikiwemo Uganda zimepiga marufuku mahusiano ya watu wa jinsia moja. Bila kujali kama mapenzi ya jinsia moja ni sawa au si sahihi, Marekani inapuuza hali ya kitaifa ya nchi za Afrika, na kuzilazimisha kufuata njia yake, na hata kuingilia utungaji wa sheria za nchi nyingine kwa kutumia nguvu zake za kisiasa na kiuchumi, kamwe kitendo hicho hakipokeleki na jamii ya kimataifa.
 
Acha propaganda,

Nimesoma kichina, Mandarin,
I understand Chinese language when somebody speaks,
Nimefanya kazi na wachina,
Nina experience na wachina,

Wachina ni moja ya watu wanapenda rushwa sana na hii ni kutokana na mfumo wa kiuongozi wa CCP

Mnapita kwenye developing countries mnahonga viongozi ili mlazimishe ushawishi wenu.
Hondorus, Zambia, Philipine mmeziharibu,

Hapa nchini mkija kazi mnazofanya ni kuchezesha kamari mitaani, mnaharibu Society, hamjali watu hamuna transparency and accountability kwenye mifumo yenu,

China Kuna kesi chungu nzina za ubakwaji kwa wanawake lakini mfumo hausapoti kuzisovu. Mfano mdogo ni mcheza teness Peng shuai Alitaka kubakwa na top member wa CCP alipolalamika akanyamazishwa.

Mfumo wenu wa kiuongozi ni hatari zaidi Duniani, haufai na unaharibu jamii.
 
Serikali yetu ya Tanzania nayenyewe ioneshe rangi zake halisi kisheria kama Uganda walivyofanya.
 
Back
Top Bottom