Tovuti 334, akaunti za Facebook 361, Instagram 198 zafungiwa kwa kutangaza Mapenzi ya jinsia moja

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Fuatilia yanayojiri Bungeni kwenye Bunge cha 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 8 leo Aprili 17, 2023.

SERIKALI YACHUKUA HATUA KUFUNGIA TOVUTI NA MITANDAO YA KIJAMII
Akizungumzia hatua zilizochukuliwa kupambana na wanaotangaza mapenzi ya jinsia moja, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema tovuti 334, akaunti za Facebook 361, Instagram 198, Twitter 12 vikoa zaidi ya 2,456 vimefungiwa

Awali, Anatropia Lwehikila Theonest aliuliza swali Bungeni kuwa Sheria za Tanzania zinasemaje kuhusu mapenzi ya jinsia moja? Ambapo Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Pauline Philipo Gekul amesema “Kifungu cha 9 cha Sheria ya Ndoa kinatafsiri Ndoa ni mahusiano ya hiyari kati ya Mwanaume na Mwanamke

Ameongeza “Pia Kifungu cha 154 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 16 kinabainisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile ni kosa la jinai na adhabu yake ni kufungo cha maisha jela au kisichopungua miaka 30 jela.”

MIUNDOMBINU YA DAR HALI NI MBAYA, MVUA ZIKINYESHA KAZI HAZIFANYIKI
Mbunge wa Segerea, Bonnah Ladislaus Kamoli amesema “Mvua ikinyesha Kisarawe maji yanakuja Ilala, hasa katika majimbo ya Segerea, Ukonga na Ilala kutokana na miundombinu mibovu.”

“Mfano juzi Wananchi wa Kata ya Vingunguti na Mnyamani wameshindwa kutoka ndani hadi tulipoomba msaada wa kampuni inayotengeneza barababa kusaidia kuondoa maji.”
 
Fuatilia yanayojiri Bungeni kwenye Bunge cha 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 8 leo Aprili 17, 2023.

Akizungumzia hatua zilizochukuliwa kupambana na wanaotangaza mapenzi ya jinsia moja, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema tovuti 334, akaunti za Facebook 361, Instagram 198, Twitter 12 vikoa zaidi ya 2,456 vimefungiwa

Awali, Anatropia Lwehikila Theonest aliuliza swali Bungeni kuwa Sheria za Tanzania zinasemaje kuhusu mapenzi ya jinsia moja? Ambapo Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Pauline Philipo Gekul amesema “Kifungu cha 9 cha Sheria ya Ndoa kinatafsiri Ndoa ni mahusiano ya hiyari kati ya Mwanaume na Mwanamke

Ameongeza “Pia Kifungu cha 154 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 16 kinabainisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile ni kosa la jinai na adhabu yake ni kufungo cha maisha jela au kisichopungua miaka 30 jela.”

Good
 
"The obvious outside of curiosity" yaani ndiyo kitu pekee kwa sasa wanachoweza kujadili na ndiyo mambo watu wetu wa habari wanayoona ni habari.

Sheria zipo na watekelezaji wapo lakini kila siku linajadiliwa kama vile ni jambo jipya linalotakiwa kutungiwa sheria na kuwekewa mkakati wa kupambana nalo.
 
B
Fuatilia yanayojiri Bungeni kwenye Bunge cha 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 8 leo Aprili 17, 2023.

Akizungumzia hatua zilizochukuliwa kupambana na wanaotangaza mapenzi ya jinsia moja, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema tovuti 334, akaunti za Facebook 361, Instagram 198, Twitter 12 vikoa zaidi ya 2,456 vimefungiwa

Awali, Anatropia Lwehikila Theonest aliuliza swali Bungeni kuwa Sheria za Tanzania zinasemaje kuhusu mapenzi ya jinsia moja? Ambapo Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Pauline Philipo Gekul amesema “Kifungu cha 9 cha Sheria ya Ndoa kinatafsiri Ndoa ni mahusiano ya hiyari kati ya Mwanaume na Mwanamke

Ameongeza “Pia Kifungu cha 154 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 16 kinabainisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile ni kosa la jinai na adhabu yake ni kufungo cha maisha jela au kisichopungua miaka 30 jela.”

BIla kutaja list ya hizo tovuti na account hii habari si ya kuamini sana
 
Kwa hiyo mjadala kuhusu kutafunwa kwa rasilimali za watanzania ndio tusubiri hadi November? Halafu waliotuhumiwa kutafuna wanaendelea kukalia nafasi zao?
 
Back
Top Bottom