Licha ya vikwazo kadhaa, hatimaye nimefanikiwa kuianza ile safari. Asanteni kwa sala zenu zimesaidia ila bado zinahitajika sana! Mungu nisaidie

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,494
113,590
Wanabodi,

Ukiwa na jambo lako, ukaomba msaada wa usaidizi kwa public ili usaidiwe, the public ulioomba msaada ika respond positive, ukasaidiwa kwa michango ya hali na mali, baadhi yetu ni huwa wanyenyekevu wakati wa kuomba tuu, lakini tukisha fanikiwa, tunatabia ya kujisahau. Haturejei kushukuru na wala hatukumbuki fadhila na kuwa na shukrani, naomba mimi nionyeshe tofauti kwa kurejea humu kushukuru.

Mimi nilikuja kwenu humbly kuomba msaada wenu, Wana JF, niko mbele yenu kwa unyenyekevu kuomba baraka zenu & moral support yenu jambo langu hili liwe! Mniombee Mungu asaidie, awezeshe liwe!
na kweli nimesaidiwa, nimefanikiwa na sasa narejea kwenu kwa unyenyekevu tena kushukuru kuhusu lile "jambo langu jambo letu".

Licha ya vikwazo kadhaa vidogo vidogo vya hapa na pale, hatimaye nimefanikiwa kuianza ile safari. Asanteni sana kwa sala zenu na michango yenu. Sala zenu na michango yenu vimewezesha, nimefanikiwa kwa asilimia 100% kutimiza lengo kusudiwa la kuianza safari. Ila sala na moral support bado vinahitajika sana katika muendelezo hadi jambo letu litimie, Mungu nisaidie!

Mwanzo siku zote ndio huwa mgumu, sala zenu na support zimesaidia sana katika hatua hii ya mwanzo ila huko mbele tunakokwenda, kama tumeanza vizuri, then mbele ni msesereko tuu! Tumeanza na Mungu, tunaenenda na Mungu na tutamaliza na Mungu.

Juzi ndio juzi, yaani juzi was the day ya kuanza ile safari ya lile Jambo letu! Japo nimeianza safari kwa vikwazo vidogo vya hapa na pale, lakini nimekamilisha hatua ya kwanza japo kwa mbinde! Tulikotoka ni kurahisi, tunakwenda ni mbali na kugumu zaidi, hivyo nakuomba keep praying for me. Ungana nami morally, to offer me your unconditional support kwa kujitolea will power yako, tuunganishe nguvu, join forces za will powers za wengine wenye mapenzi mema na taifa hili to produce a gigantic power of forces of will, that will make things happen! Mungu nisaidie!

JF ilipoanzishwa, na mkuu Max Ile 2006, was meant to be a home of great minds, lakini kwa vile watu hatulingani kuna simple minds, kuna ordinary minds na kuna great minds. Vivyo hivyo, humu JF tuko watu wa aina zote, simple minds wanao discuss people, ordinary minds wanao discuss events na great minds hawa wana discuss ideas, wote tuko humu na tumekuwa accommodated.

Bado silitaji hili jambo langu, na all ma GT wameisha lielewa na hawalisemi. Wale wenzangu na mimi ma ordinary minds wao watalizungumzia as an event! Nawaomba hata kama wewe ni mmoja wa ordinary minds, kama unajihisi unalijua, hilo jambo langu, nakuomba jifanye GT kwa kutolisema! Na wale simple minds ambao kazi yao is to discuss people, I beg you, don't discuss people, hapa usimjadili mtoa mada, muombee tuu afanikiwe katika jambo letu.

Japo siamini katika uwepo wa nguvu za giza ila kiukweli nguvu za giza zipo, they exist in reality and to those who believes them, they can act on you and destroy your dreams! Even if you don't believe them, kwa vile hizi nguvu zipo, they can act on you, zikakukumba na kukutandika, na kukukwamisha kwa kukuchelewesha tuu lakini haziwezi kuzuia! Kama jambo letu limepangwa na yeye, then ni limepangwa na litatimia!

Kwa vile mimi ni mtu wa ma story, kama wewe sio mtu wa mastory mastory then ishia hapa! Kama wewe ni mtu wa mastory, endelea...

Sikiliza, hiki ni kisa cha kweli kilichotokea juzi na jana kuhusiana na jambo letu hili!​
    1. Juzi Tarehe 1/08/2022 ndio dirisha la jambo letu limefunguliwa. Kila tarehe 1 August mimi hutakiwa kuwapo kwenye ufunguzi wa 88 kitaifa, kampuni yangu ya PPR, ina tender ya matangazo , hivyo I was faced with hard choices in between the two devils!. Ama Kuchukua fomu ya jambo letu na kupoteza tenda ya Nane Nene!. Ama kuachana na jambo letu, nikauvute mkwanja wa Nane Nane!
    2. Hivyo nikaamua kushika yote mawili!. Niendelee na jambo, kisha Nane Nane niwahi!. Hivyo nikajipanga niwe mtu wa kwanza kuchukua fomu, nijaze nirudishe asubuhi hiyo hiyo hivyo mchana nikwee mwewe nimuwahi Makamo kwenye opening ya Nane Nane Mbeya!. (mshika mawili moja humponyoka).
    3. Mimi ndiye mtu wa kwanza kufika fomu zinapotolewa na jina langu ndilo jina la kwanza lilopaswa kupewa fomu. Nikapewa Control number na kutakiwa kwenda kulipia bank.. Nikafurahi sana, maana pesa ziko kwenye simu, sihitaji hata kwenda bank!, maana kulipia kwa control number ni simple sana!
    4. Jamaa wa chama akanieleza hizi fumu hazilipiwi kwa mobile money!, lazima uende bank, ulipe, ulete bank slip!. Mambo gani haya?!. Chama digital, payment analogy?
    5. Maadam bank ni hapo next, haisumbui!, mimi huyo mbio Bank!. Kufika dirishani bank, teller ananiambia there is no way bank unaweza kupokea mobile money from the mobile phone. Lazima kwanza u deposits kwenye account, kisha bank wafanye transfer from my account into hiyo control number!
    6. Nikahamisha pesa kutoka M-PESA yangu, into my account. Pesa zikaondoka kwenye simu yangu na kuingia kwenye account yangu, nikakabidhi transfer form kwa tellar ahamishe na kuiongiza kwenye hiyo control number kulipia fomu.
    7. Tell akaniambia sorry account yako haina hiyo pesa!, Nikamgomea, kuwa nime transfer just now, na sms ya tranfer ninayo!. Kumbe fedha kwangu zimehama, lakini kwenye bank
    8. Nikauliza Voda wakakiri, pesa wanaziona ziliondoka, ila kwao pia zimeondoka, lakini benki nako kwenye account yangu fedha hizo hazipo, jee zitakuwa ziko wapi?

      Shetani anapoamua kukukwamisha!, kumbe anaweza kuingilia hadi mitandao!.
    9. Voda wakatuma ujumbe, within 24 hours, zitarushwa!, sasa naenda 48 hours, hakuna kilicho rudi!, jee fedha hizi ziko wapi?.
    10. Nikatoka next to CCM Ofisi Ndogo Lumumba, kuna M-PESA kubwa, huyo wakala ni janki tuu, mkewe ndie cashier wake, nikamweleza the situation kuwa natakiwa kulipia just I.M aniazime nilipe, kwake nikaweka dhamana zifuatazo, 1. Passport yangu, 2. Kitamulisho cha Taifa. 3, Laptop ya MacBook Pro ya 2022 (16M), nikamuonyesha tiketi ya ndege yenye reporting time ya saa 6:00 mchana, hivyo kumhakikishia kabla ya muda huo nitakuwa nimerudisha 1.M yake.
    11. Jamaa hakuniamini, akamuita ofisa mmoja wa CCM ili athibitishe hiyo 1.M inatakuwa kweli CCM. Jamaa CCM akathibitisha. Ni kweli. Jamaa wa fedha akaongea na Mkewe, wife wake akamwambia, unataka kupigwa!.
    12. Kiukweli shetani huwa wanawatumia sana wanawake, hata kwa Adamu, shetani alimuingia Adam kupitia kwa mkewe Eva!. Jamaa akaniambia, nakuamini and IO share your concern, ila mimi namsikiliza sana mke wangu!. Wife amenogomea!. Haya ya wanaume kuwasiliza sana wake zao, na hata kushindwa kumsaidia mwanaume mwenzio aliyekwama!, haijakaa poa!.
    13. By that time, ni saa 4:00 Asubuhi, nikaenda Mtaa wa Samora kwa mdogo fulani, ndio akaokoa jahazi, akanipa nikaenda mbio CRDB ya karibu ili nilipe nikimbie kuchukua fomu. Kufika nikawaonyesha ile control number, kule bank haionekani. Kumbe hiyo control number, ni lazima kudepositia tawi moja tuu specific. Hivyo nikaanza safari kuelekea tawi husika!.
    14. Nikafika, nikalipa, nikatoka benki na kuwahi kuchukua fomu. Nikawasilisha ile bank slip, nikaandikwa jina, mimi ni mtu wa pili kukabidhiwa fomu. Nikaondoka, by that time ndege yangu ya Mbeya nimeisha chelewa!.
    15. Basi nikaamua acha niendelee kujaza fomu na kukamilisha. Fomu hiyo inajazwa Shina lako, Tawi lako, Kata yako, Wilaya, Mkoa na ndipo unairejesha.
    16. Kumbe maofisa wa CCM, Shina, na Tawi, ni watu wenye shughuli zao nyingine, kuwapata bila appointment ni issue!. CCM Kata, Wilaya, na Mkoa mambo safi.
    17. Nimemaliza mizunguko yote saa 9:45, nikachomoka mbio kuwahisha kurejesha. Nimefika pale, saa 10:01!. Nikaelezwa dirisha la kurejesha fomu linafungwa saa 10:00!. Njoo kesho!.
    18. Kesho yake nikadamkia CCM kurejesha fomu, nimefika kurejesha, wanacheki, majina ya waliochukua fomu jana, jina langu halipo!. Hivyo unaambia huwezi kurejesha fomu huku jina halipo kwenye list ya waliochukua fomu!. Nikajieleza, mimi ndio mtu wa kwanza kufika kuchukua fomu na mtu wa pili kupewa fomu!, how come jina halipo?. This is strange!.
    19. Jamaa akapekuwa kule kwenye zile bank slips, slip yangu ikaonekana, ndio nikaandikishwa upya kuchukua fomu na kurejesha. Fomu ikapokelewa. Nikatoka mbio kuwahi Airpot kubahatisha flight.
    20. Nauli ya jana yake imepotea, ndege imejaa!, nikaambiwa kusubiri kama kutatokea no show!. Ikabidi watu waingie mzigoni kunoshowisha abiria mmoja!, ili nafasi ipatikane, na kweli ikatokea no show moja, ndio nikakwea pipa hivyo hivyo na nguo zangu za Chama nikatua Songwe sasa ndio Niko uwanja wa John Mwakanhale, napiga mzigo wa Nane Nane
Kitendo cha kusafiri huku nimetinga sare za chama mwanzo kulinipa taabu, maana zamani kuvaa sare za chama ilikuwa aibu hivyo nikawa naona soo. Kumbe kusafiri na sare za chama sasa ni opposite, badala ya aibu ni advantage. Kwanza kufika airport nikapokelewa kama Mheshimiwa, walidhani mimi ni Mheshimiwa Mbunge, hivyo ule ukaguzi wa vua mkanda, vua viatu huo uliniepuka.

Kufika boarding area nikapelekwa Tanzanite lounge, na baada ya ku-board yule flight attendant hakubodha kuangalia boarding pass yangu, tiketi yangu ni economy, ila kufuatia sare niliovaa nikawa upgraded to Business Class, makamuzi yakaanzia kwenye ndege!

Kufika Songwe napokelewa na kupelekwa VIP, kule nikakutana na Mawaziri, RC na wakubwa, hivyo nami kuonekana kama mkubwa fulani huku nikiitwa Mheshimiwa. Hivyo ndugu zangu, pamoja na ule mwanzo mgumu wa safari hii, hizi sasa ni dalili nzuri za kufunguka kwa njia, sasa mwendo ni msesereko tuu wa praaaaa mpaka Maka!​

Paskali - 0754 270403
 
Pole Sana na Pascal. Unaona kuwa fitina ni mbaya. Angalia walivyokuzungusha na vikwazo kibao!

Mimi sikupendi kwa vile wewe Ni adui nambari ONE wa CHADEMA.

All in all, nakuombea kwa hili ufanikiwe. Dirisha lililofunguliwa CCM Ni la Bunge la Afrika Ya Mashariki kuomba kuteuliwa na chama Kama mgombea ubunge huo. Nimelitaja like Jambo letu, I am a simple mind man as you have put it in your narration.

All the Best. What is the next step in that bid after this?
 
Back
Top Bottom