All about Tanzania life
Member
- Jul 6, 2023
- 23
- 28
Katika mpango wangu wa kuwahamasisha watanzania kutembelea vivutio mbalimbali ndani ya nchi yetu, kutembelea mikoa na maeneo ya kihistoria niliamua pia kujaribu kufikia sehemu hizo kama mfano kwa watu wachache wanaofikiwa na ujumbe huu.
Habari!! Mwishoni mwa mwezi wa nane tarehe 28 nilianza rasmi safari ya wiki moja kutembelea jiji la Mwanza a.k.a The Rock City. Hii ilikuwa ni mara yangu ya pili kutembelea jiji hilo, ambapo takribani miaka miwili nyuma niliwahi kufika hapo na kukaa kwa siku mbili pekee, siku ambazo hazikuzaa matunda kwangu kwa kuwa sikuweza kufikia sehemu nyingi nilizotamani kutembelea wakati huo. Basi niliahidi kurudi tena Mwanza na sasa nimetimiza ndoto na ahadi yangu ya kutembelea kwa mapana jiji hilo.
Safari inaanzi Dar es salaam, jiji kubwa zaidi kiuchumi Tanzania na nitaishia Mwanza jiji la pili kwa ukubwa na kiuchumi Tanzania. Kama kawaida yangu ni muhimu zaidi kwangu kujua ghalama zote nitakazo tumia njiani, malazi nitakapofika, nauli, tips, pesa za kulipia viingilio, dharura na kuchukua tahadhali zote muhimu ikiwa ni pamoja na kuandika mpango wangu wa safari na sehemu zote nitakazofikia ama kutembelea zikiwa tayari kwa njia ya maandishi katika diary yangu.
Nipo ndani ya standi kuu ya mabasi yanayoelekea mikoani na nchi jirani, bila shaka ni muhimu sana kuwahi kufika kituoni ili kuepusha presha za kuogopa kuachwa na gari uliyoabiri. Ni saa kumi na moja alfajiri na baadhi ya magari yanaanza kutoka hapa na gari yetu itaanza safari saa kumi na mbili kamili asubuhi, nikiwa abiria wa mwanzo kabisa kuingia katika gari (jina kapuni) nilipata wasaa kuzungumza na dereva na kutaka kujua mambo machache njiani na hususa kujua ni kiasi gani cha mafuta atatumia njiani kwa safari ya kwenda na kurudi Dar es salaam na ghalama yake pia. Bila shida alinipa ufafanuzi mzuri na kwa bahati nzuri kabisa gari yake haikupata kujaza mafuta usiku huo kwa sababu maarumu hivyo aliponiambia kuhusu ghalama na alinipa nafasi ya kushuhudia na kupiga picha screen ya pump wakati wakiweka mafuta njiani umbali kidogo tu kutoka Mbezi.
(Picha ya idadi ya lita 310 na kiasi cha pesa laki tisa elfu hamsini na sita na miatatu hamsini 956350)
Na hiyo atapaswa kuongeza tena wakati akiwa anarudi Dar es salaam.
Safari iliendelea vizuri sana kwa mwendo mzuri na furaha kwa abiria wote. Tuliipita Morogoro, Dodoma mji mkuu wa Tanzania na binafsi nilipata changamoto kidogo pindi tu tulipoanza kuingia mkoa wa Singida na kusababisha kuamua kushukia njiani katika mkoa wa Shinyanga. Haikuwa changamoto ya kiafya , hapana!! Maana najua wengi wangeweza kuhisi hivyo😁 lakini kutokana na kutaka kuingiliana kwa majukumu yangu ilinisababisha kushukia njiani kwanza baada ya mawasiliano ya muda mrefu kugonga mwamba na mpango ukawa kushuka hapo na kutafuta usafiri kurejea Dar es salaam muda huo huo. Mungu sio Athumani, ombi langu la kupatiwa muda kidogo likapita na tayari nimeshashuka njiani🥶🥵 hii ni asala sasa!! Na sikuwa nimepanga kulala Shinyanga au eneo lingine lolote njiani.
Basi kwa kuwa muda ulikuwa umeshasogea sana niliamua kulala hapo Shy town na sikuwa na mambo mengi jioni hiyo zaidi ya kuchukua chumba na kujipumzisha mapema kwaajiri ya kuendelea na safari kesho yake asubuhi. Na ukumbuke kuwa mpango wangu wa kutembelea Mwanza kwa wiki moja ulikuwa tayari umeshaanza kuhesabu siku na kuongeza ghalama zaidi kwa kuwa siku nitakayo amkia Shinyanga ndio ilipaswa kuwa siku ya kwanza jijini Mwanza, hivyo ni kama timu iliyofungwa nyumbani sikuwa na cha kupoteza tena zaidi ya kuabiri Tata asubuhi na mapema kuitafuta ilipo Rock city🙂 safari wakati huu haikuwa ndefu sana tuliingia Mwanza katika standi kuu ya Nyegezi mapema tu. Nilianza kushangaa ukubwa na uzuri wa stendi hiyo kama kawaida yangu, na nilishukuru Mungu kwa kunifikisha salama na kunirudisha tena katika jiji hili la ndoto zangu nililohaidi kurudi tena miaka zaidi ya miwili iliyopita. Unajua ni jambo linaloleta hisia fulani hivi za ajabu kufika sehemu unayotamani sana kutembelea!! Hasa ukiwa peke yako na kutaka kugundua vitu ambavyo jamaa yako imeshindwa kugundua na kufikia!!? Ni hali nzuri na unatengeneza kumbukumbu za ajabu sana maishani mwako, ndio maana napenda kukuonyesha hapa kuwa unaweza kufikia jambo lolote unalolitamani ikiwa tu utachukua hatua na kuamini inawezekana.
Mfano mdogo kuna mwaka mmoja hivi siukumbuki vizuri nilibahatika kutazama filamu moja tena kwa bahati mbaya tu.
Filamu hiyo inaitwa A MILLION MAILS AWAY
filamu inayozungumzia historia ya kweli kabisa ya kijana mhamiaji akiwa na wazazi wake nchini Marekani. Akiwa anatokea katika familia maskini, wakiamia Marekani kama wafanyakazi na vibarua katika mashamba mbalimbali huku wakitumia muda mwingi kuhamahama kutafuta vibarua mashambani huko. Siku moja akiwa shambani anaonekana kushika mhindi mbichi, kisha ukiwa na maganda yake anauzungusha hewani na kutamani sana kufika nje ya uso wa Dunia siku moja. Kiukweli ni filamu nzuri sana na inayotia moyo na kutuonyesha kuwa hakuna jambo gumu duniani kama utaamua kuchukua HATUA.
Nisiwachoshe kuhusu filamu hii, namalizia kidogo sehemu ambayo ilinigusa sana na kama utaitazama najua itakugusa na kukuonyesha maajabu makuu ya Mungu.
Unajua ubaguzi wa Marekani kwa watu kutoka nje ya Marekani? Basi siku moja mwalimu wa shule aliyokuwa akisoma kijana yule alitembelea nyumbani kwa wazazi wa yule kijana na lengo kuu likiwa kujua ni kwanini watoto wa familia ile hawaendi shule mara nyingi!?
Baba wa kijana akiwa hajui kuzungumza kiingereza anamwambia mwalimu huyo kuwa " wao ni maskini na ili kuweza kuishi marrkani inawapasa wao na watoto wao wafanye kazi mashambani ili wamudu ghalama za maisha" mtoto anamtafsiria mwalimu na mwalimu anachoka na kuamua kuondoka, kisha anaonekana yule kijana wa miaka kama mitano hivi akimfuata mwalimu huyo na kumpatia karatasi yenye picha ya mhindi na nyota nyingi mfano wa nje ya Dunia (space) kisha mtoto anasema ndoto yake ni kuwa mwana anga mkubwa na kutembelea nje ya Dunia. Kwa sura ya huzuni mwalimu anapokea ile karatasai na kumwambia hivi yule kijana.
"YOU ARE FORCING NATURE, NOTHING WILL STOP YOU. REMEMBER THAT!!"
"UNALAZIMISHA ASILI, HAKUNA KITAKACHOKUZUIA, KUMBUKA HILO!!"
Kisha mwalimu anaondoka zake na anarudi na karatasi ile miaka arobaini baadae jamaa akiwa engineer mkubwa wa NASA na mwana anga anaejiandaa kwenda angani.
.......Basi nikaomba kupata picha ya kumbukumbu kwenye stendi hiyo na kwa msaada wa mkatisha tiketi nikafanikiwa kupiga picha hii ya kwanza jijini Mwanza
(Subili kupata mwendelezo wa safari hii hapa hapa. Ntarejea tena hapa)