Kwa mara nyingine leo hili jambo limenifanya nijisikie vibaya sana moyoni

Ivan Stepanov

JF-Expert Member
Apr 22, 2023
4,891
15,943
Ni matumaini yangu kwamba mnaendelea vyema.

kwa wale wenye changamoto, ni maombi yangu kwa Mwenyezi Mungu kwamba atufanyie wepesi hasa katika kipindi hiki tunapomalizia mfungo wa Kwaresma na tunapoendelea na Ramadhani wengine.

Ni jambo nimelishuhudia kituo cha dala dala leo asubuh katika harakati za kuwahi kutafuta mkate wangu wa siku.

Nikiwa tayari ndani ya dala dala baada ya kugombania sanaa na jasho kunitoka almanusura nivunje laptop yangu kwenye bag, sasa nikawa nime relax nimeshika bomba chuma ya muhindi, Eicher ikawa anataka kutoka kituoni, kisha nikapiga jicho nje kuwatazama watanzania wenzagu watumiaji wa usafiri wa umma. Jicho langu likatua kwa watu watano (5) ambao kwa experience yangu nikatambua hii lazima ni Familia.

Alikua mwanaume 1 kala kanzu safi na barakhashia yake, dada mmoja makamo, watoto wawil (mmoja binti na mmoja mtoto tu kama mwangu wa 3 kuzaliwa nilipomfananisha, like 5 years). Huyu mama na hawa mabinti wamekula baibui sao safii na Hijab.
Ustadh (tumwite hivyo) yeye kwa nyongeza alikua amebena mtoto mdogo wa mwaka hivi kwa makadirio.

Wako kituoni (nisitaje pande gani, msije mkatuponda sie wakaz wa Kilwa road) , kituo kimetapakaa tope zitoo kutokana na mvua zilizonyesha hapo siku mbili nyuma. Ao unatembea kwa tahadhari kubwa kuepa kuchafuka kama sio kuchafuliwa kwa kurushiwa tope na raia au madereva daladala waliokosa ustaarabu.

Hawa watu (hii family nzuri) wanaonekana wapo hapo kwa ajili ya usafirbwa daladala wawahi wanakowahi.

Kiukwel kwa wale watumiaji wa dala dala tunaelewa ilivyo mtihani kupata usafiri wa kutokea nje ya mji kwenda mjini kati kwa mida ya asubuh. Huwa ni wa kugombania sana sana. Sasa nikajikuta nawaza sana kiubinadamu na kumuonea huruma mwamba, kama mwanaume mwenzangu, na kujikuta nafika mbali na kuona kama hii ni kadhia kubwa. Unapandaje na watu wa 5 tena wanawake katika usafiri wa kugombania. Dahh nikajiskia vibaya sana na kuona huruma na nilipo imagine na kujiweka kwenye picha hakika nikaumia zaid na kujiona kama nadharirika sana.

Ukiwa alone fresh tu, ila ukishakua na family kama hiv kiukwel inakupa teso la kihisia. Kukanyagana na kugumiana humo, wife na watoto wako plus lugha za kukera kwenye daladala ,matusi kwakifupi huwapangii watu cha kuzungumza

Mfano mzuri ni daladala za feri, wale wauza samaki utasema wanajuanaga maana wakianzaga kupiga soga unaweza sema wamekaa barazani kumbe tuko na sie wengine humo ndani ambao tume staarabika kidogo.

Nikawaza kwakwel ukishajua una oiting kama hiz na whole family, ni muhimu kujiweka sawa kama baba pale inapobidi lakini (maana maisha tunatofautiana na sio kosa) , bas angalau uwe hata na kahela ka bajaji, mmefika zenu mbagala, chukua bajaji yako, shuka steshen au kariakoo unakokwenda. Au lah subir bas angalau mida kuanzia saa 5 asubuh ambapo msongamano sio mkubwa kama una safar na family yote angalau mnaweza tumia usafir wa dala dala kwa amani kidogo bila bugudha.

MImi sio mpenz wa kutumia sana gari binafsi kuja na kurudi kazini, kwakua kwa kanuni za uchumi wangu naona sio lazima sana. Pia nature ya majukum yangu muda mwingi katika week hua ni kufika na kukaa ofisin so napendelea zaid kutumia daladala kuja na kuondoka home.

Pia kwakua kijiweni kwangu ni saa 12 nimeingia, so saa 11 alfajiri huwa hakuna adha kubwa kama ya kuanzia saa 12 ikikukuta kituoni. Pia natoka late sana around saa 2 usiku, muda ambao dala dala ni usafir comfortable kabisa time hizo ukiondoa foleni ambao hata wanaotumia magar binafsi tunakua pamoja barabarani, haya yoote hunifanya kupaki tu gari.

Lakini moja ya vitu vilinifanya kuona gari kama chombo au zana muhimu ya usafiri, ni baada ya kupanuka familia. I have four kids, na kuna momemt we have to get together going some places, kwakwel kutumia usagir wa daladala ni moja kati ya vitu vilifanya kuona nanyanyasika sana na kuwanyanyasa mke na wanangu, so i had to have one.

SAsa leo hii nilipoona wale ndugu pale kituoni, rohoni kiukwel nikajisikia vibaya sana kama mwanaume na mtu mwenye familia..

Anyway, najua kwel hayanihusu ila mdio hivyo tena sio vibaya ku feel for others.Tujitahid wanaume wenzangu, japo huwa sipend sana ule msemo wa "tutafute pesa" , ila kiukwel pale inapobid tunatakiwa kufanya hivyo.

Ahsanteni
 
Halafu kuna muda nikaona umeamua kabisa kulia huku vilio vya kwikwi vikitawala na kamasi juu
 
Back
Top Bottom