Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,513
- 52,155
Kwema Wakuu!
Wakati tunakua moja ya mambo yaliyotupa hamasa ya kusoma mpaka kufika chuo ni stori za kuwa chuo kuna watoto wazuri alafu kuna Uhuru.
Ni kweli. Tuliofika chuo kikuu hasa vyuo vyenye wanafunzi wengi tulijionea maua ya Dunia. Kulikuwa na warembo wa kila namna.
Mimi ndoto yangu kubwa ilikuwa nitafute kidemu cha kimataifa, basa kichina maana huko ndio sikuwahi kúpita. Mpango wangu ungekamilika kwa kujiunga na darasa la kusoma lugha ya kichina huko ndiko nilijua ningepata connection na vitoto vya kichina. Utoto na ujana unamambo sana. Ngoja niachie hapa. Hii stori nitaileta siku nyingine.
Wakati wengine tukijivinjari na kufaidi fahari na maua ya Dunia. Kuna wenzetu walikuwa wakiteseka, na kuteswa na mapenzi. Mpaka wanamaliza mwaka wa mwisho wakiwa hawaamini nini kinaendelea kwenye maisha yao ya chuo. Walikuwa bilabila. Hawakupata Mwanamke yeyote.
Hujui maumivu ya kurusha jiwe kwenye kundi la Ndege wengi kama nyuki alafu usiambulie chochote. Hujui hayo maumivu.
Mbaya zaidi GPA nazo hazisomi, licha ya kutokuwa na demu lakini bado walishindwa kufikisha GPA ya 3.5 ambayo ni ya kawaida kabisa.
(Kunawatu watasema Taikon unasifa😄😄).
Najua kuna ile kujidanganya kimoyomoyo kuwa wakipata kazi sijui pesa watalipiza kisasi au watafikia. My Friend, Haya maisha sivyo hivyo yalivyo. Wapo wenye pesa na wanakazi na bado mademu wanawakataa😀.
Tatizo lenu vijana mnapenda kuwa serious sana na Maisha. Mnajifanya mnamalengo ya millenium. Saikolojia ya warembo haihitaji sampuli ya Watu hiyo.
Mademu wanapenda Sanaa na burudani. Ukiweza hayo hata uwe na mia mfukoni utawafaidi. Alafu yule mwenye milioni akabaki anapiga miayo huku akilaani.
Nimemaliza. Mwenye hasira aje tupigane.