Licha ya kuambiwa chuo kuna watoto wakali. Lakini kuna Watu walimaliza chuo bila kupata demu yeyote

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Kwema Wakuu!

Wakati tunakua moja ya mambo yaliyotupa hamasa ya kusoma mpaka kufika chuo ni stori za kuwa chuo kuna watoto wazuri alafu kuna Uhuru.

Ni kweli. Tuliofika chuo kikuu hasa vyuo vyenye wanafunzi wengi tulijionea maua ya Dunia. Kulikuwa na warembo wa kila namna.

Mimi ndoto yangu kubwa ilikuwa nitafute kidemu cha kimataifa, basa kichina maana huko ndio sikuwahi kúpita. Mpango wangu ungekamilika kwa kujiunga na darasa la kusoma lugha ya kichina huko ndiko nilijua ningepata connection na vitoto vya kichina. Utoto na ujana unamambo sana. Ngoja niachie hapa. Hii stori nitaileta siku nyingine.

Wakati wengine tukijivinjari na kufaidi fahari na maua ya Dunia. Kuna wenzetu walikuwa wakiteseka, na kuteswa na mapenzi. Mpaka wanamaliza mwaka wa mwisho wakiwa hawaamini nini kinaendelea kwenye maisha yao ya chuo. Walikuwa bilabila. Hawakupata Mwanamke yeyote.

Hujui maumivu ya kurusha jiwe kwenye kundi la Ndege wengi kama nyuki alafu usiambulie chochote. Hujui hayo maumivu.

Mbaya zaidi GPA nazo hazisomi, licha ya kutokuwa na demu lakini bado walishindwa kufikisha GPA ya 3.5 ambayo ni ya kawaida kabisa.

(Kunawatu watasema Taikon unasifa😄😄).

Najua kuna ile kujidanganya kimoyomoyo kuwa wakipata kazi sijui pesa watalipiza kisasi au watafikia. My Friend, Haya maisha sivyo hivyo yalivyo. Wapo wenye pesa na wanakazi na bado mademu wanawakataa😀.

Tatizo lenu vijana mnapenda kuwa serious sana na Maisha. Mnajifanya mnamalengo ya millenium. Saikolojia ya warembo haihitaji sampuli ya Watu hiyo.

Mademu wanapenda Sanaa na burudani. Ukiweza hayo hata uwe na mia mfukoni utawafaidi. Alafu yule mwenye milioni akabaki anapiga miayo huku akilaani.

Nimemaliza. Mwenye hasira aje tupigane.
 
KWERI TUPU, Nilishuhudia wanangu chuo wakimiliki pisi mbovu mbovu tena zinawaendesha, mimi nikiwa Shule bado nilishangaaa ila nilipofika Chuo niliyaona ya kawaida sikuwah date demu wa chuo kwangu ila vyuo jirani niliwekeza sanaaaaaaa🤣
 
KWERI TUPU, Nilishuhudia wanangu chuo wakimiliki pisi mbovu mbovu tena zinawaendesha, mimi nikiwa Shule bado nilishangaaa ila nilipofika Chuo niliyaona ya kawaida sikuwah date demu wa chuo kwangu ila vyuo jirani niliwekeza sanaaaaaaa🤣
Uliposema pisi mbovu umenikumbusha mbali sana maana hata mimi niliwahi kumiliki peugot moja ili kutoa wenge la upwiru. Ila nilipopata uzoefu wa kazi nilianza kulamba zile hotcake tu 😂 ni mapito Mungu anisamehe
 
Ukweli ni kwamba chuoni tulistuka wanafunzi wa kike wanatembea na walimu, watumishi wa serikali, wafanyakazi wa mabenki hasa wale teller, wafanya biashara, swagga boys wa mitaani, n.k. Yaani ikitokea mwanafunzi wa kiume kaamua kuwa na girlfriend wa hapo chuoni inabidi amvute geto waishi pamoja zile ndoa za chuoni maana ushindani ni mkubwa, tena wanafunzi tulikuwa hatuheshimiani, wakijua umepata wa chuoni ni kama umepuliza filimbi ya mashindano, watafanya jitihada wakuchapie.

Hii ikafanya na sisi tutafute wanyonge wetu wa nje ya chuo kuanzia mabinti wanaouza maduka, mabinti vya mama ntilie, mabinti wanaoshinda majumbani, mabeki tatu, n.k. hawa walikuwa hawana gharama sana na wengi walituheshimu kwa ile hadhi / status ya kuwa mwanachuo.

dem wangu wa kwanza chuoni alikuwaga wa mtaani ila mabroo waliotutangulia wakanisanua huyo cha wote nikamuacha, nikaja kuwa na mtoto wa mama ntilie, nikahamia kwa anaefua nguo, nikahamia kwa Anaeuza duka la simu, nikaja kwa beki Tatu alieletwa tupo nyumba moja namvusha geto la nje kikomandoo.

Nadhani mada ilibidi iwe kwa wanaume wanaomaliza chuo bila kuwa na dem kabisa.
 
2010-2014 kuna wimbi kubwa la *WATOTO WA SALMA walijiunga chuo fulani.

Kwa udadisi wangu na uoga nikahisi kila ninayekutana naye ni miongoni mwa hao mabinti.

Kingine masomo yangu yalikuwa magumu sana.

By the way mapenzi ya chuo hutegemea boom ambapo mkimaliza masomo mwanaume anakuwa na hali ngumu huku binti akiwa huru kufanya mahusiano mapya na kumuacha yule wa chuo.

Kwa hiyo sikutaka kuwa na mahusiano ya aina hii.

So miaka minne yote sikupata demu chuo.

Na bado ninadhani nilifanya uamuzi sahihi sana.
 
Back
Top Bottom