Pesa ya Mwanamke ilivyotamu lazima niilambe! Huo ndio msimamo wangu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
PESA YA MWANAMKE ILIVYOTAMU LAZIMA NIILAMBE; HUO NDIO MSIMAMO WANGU!

Anaandika, Robert Heriel

Ujumbe huu ni Kwa Hustlers wote. Vijana wote mliotokea kwenye Familia Masikini! Usiogope Kula au kutumia pesa ya Mkeo.

Ati nisiitegemee pesa ya mwanamke, Nani kasema?
Pesa ya mwanamke lazima Taikon ailambe! Kama ni Mama yangu lazima niile, Kama ni pesa ya Mke wangu lazima niile. Hao watu wawili lazima pesa Yao niilambe kivyovyote. Nao wanauhalali wa Kula pesa yangu kivyovyote.
Hakuna Raha Kama pesa ya Mwanaume ikiliwa na Mkewe au Mamaye. Raha tuu.

Tabia za ubinafsi ndio zinafanya watu washindwe Kula Bata Duniani. Kama unaogopa Kula pesa ya mwanamke na umetoka familia Masikini. Nakupa pole Sana.

Sijali ninyi Walimwengu mtasemaje, mtajijua wenyewe na unafiki wenu. Hata hivyo kila mtu anakanuni zake.

Kwanza pesa ya mwanamke ni tamu licha ya. Kuwa inamasimango😀.

Hakuna pesa tamu Kama pesa upewayo na Mama yako, na Ile upewayo na Mke wako.

Kwanza ukipewa pesa na Mkeo au mchumba wako unakuwa unachekacheka Kwa aibu😂😂 nafsini ukijisemea hii pesa nitairudisha,lakini ukikiri kuwa huyu Mwanamke ni kweli ananipenda.

Kumbuka kuwa mwanamke kama hakupendi lazima awe mgumu na ajisikie vibaya kukupa pesa yake.

Lakini kama mwanamke anakupenda pesa zake utazila Sana. Zingatia, wanawake kiasili ni wachoyo na wachumi wa pesa. Yaani ili akupe pesa yake basi lazima akupende Sana, alafu mbili uwe mtoto wake wa kuzaa.

Mwanamke akikupa pesa yake wivu wake unaongezeka maradufu, na anataka uwe wake pekeake, yaani ni kusema achilia mbali kutaka kumiliki moyo wako lakini pia anataka na roho yako. Doooh! Lakini tavumilia Mimi!

Mario! Sijui umarioo! Sijui kulelewa! Mtatunga tungo na nyimbo kuniimba Taikon lakini Mimi ndio nimeshaamua.
Muhammad alikula pesa za Bi. Khadija. Haya wewe ni Muhammad Nani anaheshimika hapa duniani, Nani anajulikana?

Yesu Kristo keshakula Sana pesa za kina Maria Magdalena. Haya wewe na Yesu Nani anaheshima kwenye huu ulimwengu. Nani mashuhuri. Nani kaibadilisha Dunia.

Daudi Kala pesa ya Abigail. Haya wewe na Mfalme Daudi Nani anaheshimika, Nani mashuhuri!

Kama unatoka Familia Masikini basi kaa ukijua kuwa Bila kuwa na hekima katika kuchagua Mwanamke mzuri wa kuoa basi Future yako na future ya watoto wako iko mashakani.
Future ya watoto wako ipo mikononi mwa Mkeo.

Kuna watu hawawezi kunielewa, na sipo Kwa ajili Yao.

Usione watu ni wajinga kuoa wanawake kutoka makabila yenye kuchakarika, wanasababu zao. Moja ya sababu ni suala la malezi ya watoto.

Unaoa makabila au watu ambao wavivu wavivu kazi kuwaza vitu vya kipuuzi puuzi, unafikiri utafika wapi.
Jamii zote zenye wanawake wachapakazi Duniani ndizo zilizoendelea.

Ukitoka katika familia Masikini kaa ukijua maisha yako hayatakuwa rahisi, kuna kupanda na kushuka, na kupata na kukosa. Kuna kushinda na kushindwa.

Lazima uwe na Mwanamke atakayekupa backup. Usiogope changamoto za hawa wanawake ati ooh! Sijui wajeuri, ooh! Sijui akitoa pesa anakuwa na sauti.

Hakuna mwanamke mwenye sauti Kwa mwanaume anayempenda, hakuna na hajawahi kutokea.

Kwanza akupende, pili fanya wajibu wako kama Mwanaume, wanawake sio kwamba hawajui au hawaoni, wanamacho ya kuona kuwa Mumewe anahangaika sema ni vile labda ni Fungu la kukosa.

Weka akilini, Wanawake wanamacho Kwa wanaume wanaowapenda na kuwafikisha kileleni.

Kama Mwanamke hakupendi hawezi ona unachokifanya. Hata uvuje jasho vipi, hata uipiganie familia yako kiaje au umpiganie yeye lakini kamwe Mwanamke hawezi kuona ufanyacho Kama hakupendi. Mwanamke huona vile hisia zake zinavyoona. Hilo weka akilini.

Mwanamke Mchapakazi mwenye pesa madafu lazima watoto wako waende shule, yaani piga ya garagaza. Hiyo ni must. Atauza mitumba, genge, au kufanya biashara hata ya kutembeza ilimradi kuitunza familia yake.

Usikubali kuoa mwanamke MASIKINI, Hilo kila mara Taikon analisemaga,

Yaani mwanamke kama mdoli asiyejishughulisha. Usikubali.

Pesa ya mwanamke asiyejishughulisha hailiwi! Sijui umenielewa.

Na Kama pia haujishughulishi kamwe usile pesa ya mwanamke labda uwe mgonjwa.

Wanaume wa jamii ya Taikon, tunaoa wanawake wenye maarifa, na wenye kiu ya maendeleo. Kama hawana biashara au kazi tunawasaidia kupata kazi au tunawapa mitaji ya kufungua biashara ili baadaye tuonje Raha ya kuwa na Mke.

Raha ya Mke siku moja akununulie Suti au kiatu kikali, raha ya mke akitoa shopping anakuja anakuletea zawadi za hapa na pale. Raha ya Mke awe na uchumi bhana😀.

Wanaume wasiojiamini ndio wanaogopa wanawake wenye pesa au uwezo wa kiuchumi. Wanaume wasiojiamini ndio wanaogopa Kula pesa za Wake zao. Ni kutojiamini tu!

Sasa wewe utajiamini zaidi ya Muhammad au Yesu? Au Daudi 😂😂. Hizo njemba tunazungumzia Icon za Dunia.

Zingatia, mwanaume lazima uwe mjanja, uwe na Akili Sana ili uweze kumfurahia na kumfurahisha Mkeo.
Ni kweli kuwa na Mwanamke mmoja kwetu wanaume ni kipengele. Na wake wote Duniani wanalijua Hilo, ingawaje hawataki kuwa Mke mwenza lakini hawajakuzuia kuwa na wanawake wengine bila ya yeye kujua😀.

Sijasema umtegemee Mwanamke wala sijasema Mwanamke amtegemee Mwanaume. Yeyote anatemtegemea mwenzake hafai kuwa kwenye mahusiano ya ndoa.

Ninachosema kusiwe na Ubinafsi. Usione shida Kula pesa ya Mkeo kwani pia niyako. Pia mke asione shida Kula pesa ya Mumewe kwani pia ni yake.

Mfundishe mkeo kujitegemea hata bila ya uwepo wako. Kutokana na kuwa jamii zetu zilimuandaa mwanamke kumtegemea Mumewe Jambo ambalo sio zuri Kwenye ndoa.

Kumtegemea Mtu ni kumfanya kuwa Mungu mtu.

Ndio maana Taikon yeye kitu chakwanza kwenye mahusiano ni Upendo, kisha uaminifu, alafu mwisho Uhuru.
Uhuru ndio kujitegemea kwenyewe.

Usiogope kuachwa 😂😂 ooh! Nikimpa mtaji ataniacha Kama mnawatoto usiogope kuachwa. Kuachana ni lazima iwe mkiwa hai au siku mmoja wenu akifa😀.

Taikon ni mtu wa mfumo Dume ambao siku zote ndio unaotawala Dunia. Muandae Mkeo kujitegemea na kuitunza familia bila uwepo wako. Au ukiwa unaumwa au katika Hali mbaya.

Kama hujanielewa utanielewa ukishakuwa mtu mzima. Baadhi watachelewa kunielewa ikiwa ni Too late.

Unapoambiwa nyuma ya mafanikio ya wanaume wengi kuna Mwanamke elewa kuwa Pesa ya Mwanamke inaliwa, jasho la mwanamke linaliwa. Na wala sio kosa.

Waliofanikiwa wengi katika Nyanja nyingi tunalielewa Jambo Hilo.

Pia zingatia kuwa kila Mwanaume aliyeanguka nyuma yake yupo Mwanamke.

Usikubali kuwa na Mwanamke nyongaji, mdoli, asiye na msaada.

Yaani umsaidie yeye tuu! Kumbuka falsafa ya wanawake wote Duniani ni kuwa kwako atapata nini.

Kama hujanielewa shauri yako!

Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Umeeleweka Sana Mkuu.

Inahitaji akili kubwa kukuelewa. Wanaume wengi tumekalili kuoa au kuishi na wanawake tuliowazidi kiuchumi, Kielimu,. Na kijamii.

Huwa hatuwezi kuwatengeneza wake zetu kuwa ni watu wenye kuweza kujitegemea, Tunaamini wakiwa na nguvu ya kiuchumi watatudharau,watatupuuza kitu ambacho si kweli.

Nimekuelewa zaidi uliposema mwanamke ana macho anaweza kuona jitihada anazofanya mwanaume katika kutafuta ikiwa Tu anakupenda. Maana ili aweze kuona unachofanya ni lazima awe na hisia na ww.

Kiufupi wanawake huongozwa zaidi na hisia Kwanza kabla ya akili. Ukipendwa mwanamke hawezi kuona shida kutoa pesa yake kwaajili yako. Ubinafsi wa mwanamke huanzia asipokuwa na hisia na ww.

Tofauti na wanaume Sisi tunaweza kukuhudumia mwanamke hata Kama hatumpendi. Kumtamani Tu mwanamke inaweza kuwa sababu tosha ya kuanza kutoa huduma bila kuwa na hisia nae.

Kiufupi mwanaume wanaotaka familia choka mbaya,au za Hali ya kawaida wanapaswa kuwa makini zaidi wanapofikia hatua ya kuoa. Wanahitaji mwanamke mwenye vision, mchakarikaji, ambaye anaweza kuclear bill zake mwenyewe sometimes bila msaada wa mume.
 
Upo sahihi Kabisa.
Mwanamke kama hakupendi hata umpe pesa bado atasema humpi😂😂
 
PESA YA MWANAMKE ILIVYOTAMU LAZIMA NIILAMBE; HUO NDIO MSIMAMO WANGU!

Anaandika, Robert Heriel

Ujumbe huu ni Kwa Hustlers wote. Vijana wote mliotokea kwenye Familia Masikini! Usiogope Kula au kutumia pesa ya Mkeo.

Ati nisiitegemee pesa ya mwanamke, Nani kasema?
Pesa ya mwanamke lazima Taikon ailambe! Kama ni Mama yangu lazima niile, Kama ni pesa ya Mke wangu lazima niile. Hao watu wawili lazima pesa Yao niilambe kivyovyote. Nao wanauhalali wa Kula pesa yangu kivyovyote.
Hakuna Raha Kama pesa ya Mwanaume ikiliwa na Mkewe au Mamaye. Raha tuu.

Tabia za ubinafsi ndio zinafanya watu washindwe Kula Bata Duniani. Kama unaogopa Kula pesa ya mwanamke na umetoka familia Masikini. Nakupa pole Sana.

Sijali ninyi Walimwengu mtasemaje, mtajijua wenyewe na unafiki wenu. Hata hivyo kila mtu anakanuni zake.

Kwanza pesa ya mwanamke ni tamu licha ya. Kuwa inamasimango.

Hakuna pesa tamu Kama pesa upewayo na Mama yako, na Ile upewayo na Mke wako.

Kwanza ukipewa pesa na Mkeo au mchumba wako unakuwa unachekacheka Kwa aibu nafsini ukijisemea hii pesa nitairudisha,lakini ukikiri kuwa huyu Mwanamke ni kweli ananipenda.

Kumbuka kuwa mwanamke kama hakupendi lazima awe mgumu na ajisikie vibaya kukupa pesa yake.

Lakini kama mwanamke anakupenda pesa zake utazila Sana. Zingatia, wanawake kiasili ni wachoyo na wachumi wa pesa. Yaani ili akupe pesa yake basi lazima akupende Sana, alafu mbili uwe mtoto wake wa kuzaa.

Mwanamke akikupa pesa yake wivu wake unaongezeka maradufu, na anataka uwe wake pekeake, yaani ni kusema achilia mbali kutaka kumiliki moyo wako lakini pia anataka na roho yako. Doooh! Lakini tavumilia Mimi!

Mario! Sijui umarioo! Sijui kulelewa! Mtatunga tungo na nyimbo kuniimba Taikon lakini Mimi ndio nimeshaamua.
Muhammad alikula pesa za Bi. Khadija. Haya wewe ni Muhammad Nani anaheshimika hapa duniani, Nani anajulikana?

Yesu Kristo keshakula Sana pesa za kina Maria Magdalena. Haya wewe na Yesu Nani anaheshima kwenye huu ulimwengu. Nani mashuhuri. Nani kaibadilisha Dunia.

Daudi Kala pesa ya Abigail. Haya wewe na Mfalme Daudi Nani anaheshimika, Nani mashuhuri!

Kama unatoka Familia Masikini basi kaa ukijua kuwa Bila kuwa na hekima katika kuchagua Mwanamke mzuri wa kuoa basi Future yako na future ya watoto wako iko mashakani.
Future ya watoto wako ipo mikononi mwa Mkeo.

Kuna watu hawawezi kunielewa, na sipo Kwa ajili Yao.

Usione watu ni wajinga kuoa wanawake kutoka makabila yenye kuchakarika, wanasababu zao. Moja ya sababu ni suala la malezi ya watoto.

Unaoa makabila au watu ambao wavivu wavivu kazi kuwaza vitu vya kipuuzi puuzi, unafikiri utafika wapi.
Jamii zote zenye wanawake wachapakazi Duniani ndizo zilizoendelea.

Ukitoka katika familia Masikini kaa ukijua maisha yako hayatakuwa rahisi, kuna kupanda na kushuka, na kupata na kukosa. Kuna kushinda na kushindwa.

Lazima uwe na Mwanamke atakayekupa backup. Usiogope changamoto za hawa wanawake ati ooh! Sijui wajeuri, ooh! Sijui akitoa pesa anakuwa na sauti.

Hakuna mwanamke mwenye sauti Kwa mwanaume anayempenda, hakuna na hajawahi kutokea.

Kwanza akupende, pili fanya wajibu wako kama Mwanaume, wanawake sio kwamba hawajui au hawaoni, wanamacho ya kuona kuwa Mumewe anahangaika sema ni vile labda ni Fungu la kukosa.

Weka akilini, Wanawake wanamacho Kwa wanaume wanaowapenda na kuwafikisha kileleni.

Kama Mwanamke hakupendi hawezi ona unachokifanya. Hata uvuje jasho vipi, hata uipiganie familia yako kiaje au umpiganie yeye lakini kamwe Mwanamke hawezi kuona ufanyacho Kama hakupendi. Mwanamke huona vile hisia zake zinavyoona. Hilo weka akilini.

Mwanamke Mchapakazi mwenye pesa madafu lazima watoto wako waende shule, yaani piga ya garagaza. Hiyo ni must. Atauza mitumba, genge, au kufanya biashara hata ya kutembeza ilimradi kuitunza familia yake.

Usikubali kuoa mwanamke MASIKINI, Hilo kila mara Taikon analisemaga,

Yaani mwanamke kama mdoli asiyejishughulisha. Usikubali.

Pesa ya mwanamke asiyejishughulisha hailiwi! Sijui umenielewa.

Na Kama pia haujishughulishi kamwe usile pesa ya mwanamke labda uwe mgonjwa.

Wanaume wa jamii ya Taikon, tunaoa wanawake wenye maarifa, na wenye kiu ya maendeleo. Kama hawana biashara au kazi tunawasaidia kupata kazi au tunawapa mitaji ya kufungua biashara ili baadaye tuonje Raha ya kuwa na Mke.

Raha ya Mke siku moja akununulie Suti au kiatu kikali, raha ya mke akitoa shopping anakuja anakuletea zawadi za hapa na pale. Raha ya Mke awe na uchumi bhana.

Wanaume wasiojiamini ndio wanaogopa wanawake wenye pesa au uwezo wa kiuchumi. Wanaume wasiojiamini ndio wanaogopa Kula pesa za Wake zao. Ni kutojiamini tu!

Sasa wewe utajiamini zaidi ya Muhammad au Yesu? Au Daudi . Hizo njemba tunazungumzia Icon za Dunia.

Zingatia, mwanaume lazima uwe mjanja, uwe na Akili Sana ili uweze kumfurahia na kumfurahisha Mkeo.
Ni kweli kuwa na Mwanamke mmoja kwetu wanaume ni kipengele. Na wake wote Duniani wanalijua Hilo, ingawaje hawataki kuwa Mke mwenza lakini hawajakuzuia kuwa na wanawake wengine bila ya yeye kujua.

Sijasema umtegemee Mwanamke wala sijasema Mwanamke amtegemee Mwanaume. Yeyote anatemtegemea mwenzake hafai kuwa kwenye mahusiano ya ndoa.

Ninachosema kusiwe na Ubinafsi. Usione shida Kula pesa ya Mkeo kwani pia niyako. Pia mke asione shida Kula pesa ya Mumewe kwani pia ni yake.

Mfundishe mkeo kujitegemea hata bila ya uwepo wako. Kutokana na kuwa jamii zetu zilimuandaa mwanamke kumtegemea Mumewe Jambo ambalo sio zuri Kwenye ndoa.

Kumtegemea Mtu ni kumfanya kuwa Mungu mtu.

Ndio maana Taikon yeye kitu chakwanza kwenye mahusiano ni Upendo, kisha uaminifu, alafu mwisho Uhuru.
Uhuru ndio kujitegemea kwenyewe.

Usiogope kuachwa ooh! Nikimpa mtaji ataniacha Kama mnawatoto usiogope kuachwa. Kuachana ni lazima iwe mkiwa hai au siku mmoja wenu akifa.

Taikon ni mtu wa mfumo Dume ambao siku zote ndio unaotawala Dunia. Muandae Mkeo kujitegemea na kuitunza familia bila uwepo wako. Au ukiwa unaumwa au katika Hali mbaya.

Kama hujanielewa utanielewa ukishakuwa mtu mzima. Baadhi watachelewa kunielewa ikiwa ni Too late.

Unapoambiwa nyuma ya mafanikio ya wanaume wengi kuna Mwanamke elewa kuwa Pesa ya Mwanamke inaliwa, jasho la mwanamke linaliwa. Na wala sio kosa.

Waliofanikiwa wengi katika Nyanja nyingi tunalielewa Jambo Hilo.

Pia zingatia kuwa kila Mwanaume aliyeanguka nyuma yake yupo Mwanamke.

Usikubali kuwa na Mwanamke nyongaji, mdoli, asiye na msaada.

Yaani umsaidie yeye tuu! Kumbuka falsafa ya wanawake wote Duniani ni kuwa kwako atapata nini.

Kama hujanielewa shauri yako!

Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Ni wapi yesu alikula Hela za kina maria madgidalena ?
 
Luka 8:1
Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye,

Luka 8:2
na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba,

Luka 8:3
na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao.
 
Hivi mkuu Taikoni wa fasihi umeandika vitabu gani na vitabu gani ?

1. Maisha YANANJIA yake.
2. Usisahau Mambo haya.
3. Nyota ya Tibeli.

RIWAYA
1. MLIO WA RISASI HARUSINI
2. WAKALA WA SIRI
3. SABOKA
4. Siku yangu ya kufa ILIPITA
5. Kaburi la Mwanamuziki
6. Mtoto wa MSUKULE
7. Kilio Pasipo machozi.

Vilivyosokoni
1. Mlio WA RISASI HARUSINI
2. Wakala wa Siri.
 
1. Maisha YANANJIA yake.
2. Usisahau Mambo haya.
3. Nyota ya Tibeli.

RIWAYA
1. MLIO WA RISASI HARUSINI
2. WAKALA WA SIRI
3. SABOKA
4. Siku yangu ya kufa ILIPITA
5. Kaburi la Mwanamuziki
6. Mtoto wa MSUKULE
7. Kilio Pasipo machozi.

Vilivyosokoni
1. Mlio WA RISASI HARUSINI
2. Wakala wa Siri.
Safi mkuu.Kwa nini umeweka viwili sokoni mkuu ? Hivyo vengine vipi
 
Zingatia, mwanaume lazima uwe mjanja, uwe na Akili Sana ili uweze kumfurahia na kumfurahisha Mkeo.
Ni kweli kuwa na Mwanamke mmoja kwetu wanaume ni kipengele. Na wake wote Duniani wanalijua Hilo, ingawaje hawataki kuwa Mke mwenza lakini hawajakuzuia kuwa na wanawake wengine bila ya yeye kujua😀.

Sijasema umtegemee Mwanamke wala sijasema Mwanamke amtegemee Mwanaume. Yeyote anatemtegemea mwenzake hafai kuwa kwenye mahusiano ya ndoa.

Ninachosema kusiwe na Ubinafsi. Usione shida Kula pesa ya Mkeo kwani pia niyako. Pia mke asione shida Kula pesa ya Mumewe kwani pia ni yake.

Mfundishe mkeo kujitegemea hata bila ya uwepo wako. Kutokana na kuwa jamii zetu zilimuandaa mwanamke kumtegemea Mumewe Jambo ambalo sio zuri Kwenye ndoa.

Kumtegemea Mtu ni kumfanya kuwa Mungu mtu.
TAKEN FOR ACTION
 
Back
Top Bottom