Rais anashauriwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye kila jambo la mikataba na sheria, sasa mkataba huu baina ya Tanzania na Dubai unaosambaa kwenye mitandaoni hauna sahihi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Suala la Bandari sio la Wizara moja ni suala la nchi haliwezi kuamuliwa kiwizara, watanzania tulitegemea kuona sahihi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya kuwa amesoma na kujiridhisha juu ya vipengele vya mkataba wa kuipa bandari Kampuni ya Dubai kwa muda usiojulikana kuendeleza na kuendesha bandari zote Tanzania za Baharini na maziwa makuu yote.
Maana yake ni bandari zetu ikiwemo Bandari ya Dar es Salaam, Mtwara, Tanga, Mwanza, Bukoba, Musoma, Kigoma, Karema, Itungi, Mbamba Bay, kwa ufupi ni bandari zote.
Kinachoonekana huu mkataba hauna Baraka ya Mwasheria Mkuu wa Serikali na ndio maana hakuna sahihi yake, watanzania wengi wanajiuliza Rais alijiridhisha kupitia mamlaka gani kwamba vipengele na masharti ya mkataba yako sawa na vimezingatia maslahi mapana ya nchi yetu hadi kuweka sahihi.
Kikatiba sina uhakika kama Rais ana mamlaka kusaini mkataba wa nchi na nchi kabla ya kulishirikisha Bunge katika hatua za awali, serikali ilikuwa na nafasi ya kulishirikisha Bunge katika hatua za awali kwa kuipeleka MOU bungeni ambayo ilikuwa na vipengele vyote muhimu vinavyokwenda kutumika kutengeneza mkataba.
Mkataba mkubwa wa nchi na nchi una kasoro kubwa upande wa Tanzania Waziri na Rais wamesaini kwa majina yao na vyeo vyao lakini kwa upande wa Katibu Mkuu amesaini bila kutaja jina la Katibu Mkuu lakini eneo la Katibu Mkuu unaona imetumika saini mbili moja ya wino wa kijani na nyingine wino wa bluu na hazijulikani saini hizo ni za kina nani?
Lakini kwa upande wa Dubai kwenye mkataba amesaini msimamizi wa bandari badala ya Rais wa nchi ya Dubai wala Waziri mwenye dhamana ya uchukuzi huko dubai kama ilivyokuwa kwa upande wetu wa Tanzania na akasaini mtu mmoja kwenye maeneo yote ya mkataba.
Ikumbukwe kuwa Mwansheria Mkuu wa Serikali ndiye Mshauri wa mwisho wa Sheria kwa Serikali kwenye mkataba huu hakuna sahihi yake.
Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili ya Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources (Permanent Soveveighty) Act, 2017) imezingatiwaje? Mwanasheria Mkuu angetusaidia hapo.
Lakini kwenye Mkataba Waziri Mbarawa inaonekana ameghushi sahihi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuna wino wa Kijani wa kalamu ya Waziri alafu hapo hapo kuna wino wa bluu.
Lakini Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ina Makatibu wakuu wawili Balozi Mhandisi Aisha Amour (Katibu Mkuu Ujenzi) na Bw. Gabriel J. Migire (Katibu Mkuu Uchukuzi) sasa kwenye mkataba huu aliyesaini sehemu ya Katibu Mkuu ni nani?
Nini Hatma ya Taifa letu…