zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 19,060
- 28,706
Habari za jioni wanajukwaa....kama kichwa cha uzi kinavyosema ningependa tujadili mada hii Kutokana na hili swali swali kuulizwa mara nyingi kwenye thread zangu nimeona nifungue uzi wake ili tujaribu kulitatua hili swali
Je ni kwanini aliyetenda dhambi ya kumuangulia uchi wa babake ni HAM ila laana ikaenda kwa mwanaye ham aliyeitwa CANAAN....
STORI YENYEWE
Mwanzo 9
20 Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;
21 akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.
22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.
23 Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.
24 Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.
25 Akasema,Na alaaniwe Kanaani;Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.
26 Akasema,Na atukuzwe BWANA Mungu wa Shemu;Na Kanaani awe mtumwa wake
Mpaka hapa tunaona anayetajwa kuchungulia uchi ni Ham ila laana inaenda kwa Canaan why?? Embu tusome nadharia hii
NADHARIA #1
Kutoka vyanzo tofauti vya kihistoria na kidini vinaelezea kisa hiki kwamba Nuhu alipolewa Ham hakuona uchi kama uchi ila inaelezwa Ham alilala na Mke wa Nuhu yaani Ham alilala na mama yake mzazi na mwisho wa siku akabeba mimba na akazaliwa Canaan na hii ilipelekea Nuhu amlaani Canaan na sio Ham sababu alikuwa kizazi cha dhambi haramu kabisa..... Na vitabu hivi vinaenda mbali na kusema Ham alimuhasi baba yake alipokuwa amelewa hiyo nayo ikapelekea Nuhu kushindwa kuzaa mtoto mara baada ya gharika!!!
VITABU VYA DINI
Nadharia hii sio tu nje ya vitabu vya dini ila hta vitabu vya dini hasa biblia inaweza kutumika kuijengea hoja embu tuangalie tafsiri yake
Mambo ya walawi 20
11 Na mtu mume atakayelala pamoja na mke wa baba yake amefunua utupu wa baba yake; wote wawili hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao
Walawi 18:8
8 Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako
NB:Kitabu cha mwanzo na mambo ya walawi vyote viliandikwa mwanzoni na Nabii Musa hivyo kama tutachukua tafsiri yake ya ''KUANGALIA UCHI WA BABA YAKO'' inamaanisha kuna ukweli juu ya nadharia hii kuwa Ham alimlala mama yake mzazi/mke wa Nuhu
Na sio kwa baba tuu Musa alielezea zaidi
Walawi 20
20 Tena mtu mume akilala na mke wa mjomba wake, ameufunua utupu wa mjomba wake; watauchukua uovu wao; watakufa bila kuzaa mwana.
21 Tena mtu mume akimtwaa mke wa nduguye, ni uchafu; ameufunua utupu wa nduguye; hao watakuwa hawana wana
Biblia haikuishia hapo ila ukisoma kitabu cha habakuki kinakataza mtu kulewesha jirani yake ili KUMCHUNGULIA UCHI.... Ikimaanisha kama ambayo Ham alimfanyia baba yake alipokuwa amelewa basi ndio hiko anachokataza habakuk ila sio kuchungulia kwa macho kama wengi tulivyoaminishwa
Habakkuk 2:15
15 Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!
Mistari iko mingi zaidi ya 10 inayoeleza kwamba kumchungulia kaka baba au mjomba wako ni kulala na mke wake hivyo wa waliouliza swali hili naona tunaweza conclude kwa nadharia hii kuwa HAM alimlala mke wa NUHU ndio baada ya kuja kujua alichofanya na mimba aliobeba akamlaani Canaan sababu ndio zao la dhambi hiyo iliotendeka
NADHARIA #2
Ukisoma vitabu vya dini ya kiyahudi kma midrash vinasema Canaan aliona Nuhu akiwa uchi hivyo akaenda kumuhasi kwa kutumia kamba na alipotoka ndio baadae Ham alikuta Nuhu akiwa amevuliwa nguo yeye akaishia kucheka tu badala ya kumfunika na mwisho wa siku ndipo laana akapewa Canaan kwa kufanya hicho kitendo
NADHARIA #3
Hapa inadaiwa na wanatheolojia kuwa mwandishi wa kitabu hiki alikuwa anatafuta sababu ya kuhalalisha uvamizi wa israel kwenye nchi ya Canaan so akapachika jina Canaan badala ya HAM ili ahalalishe uvamizi wa israel kwa kigezo cha kwamba NENO LA MUNGU LILIANDIKA!!!
NADHARIA #4
Inasema Canaan hakuwa mtoto wa Nuhu ila ndio alirudisha damu ya wanefili baada ya gharika baada ya Malaika aliyeitwa SHAMAEL siku chache kabla ya gharika alimlala mke wa HAM aliyeitwa Neitamuk na kumpa mimba ya mnefili CANAAN na ndio alisababisha maasi na roho ya shetani kupata nguvu upya immediately baada ya gharika na ndiye alipelekea kuzaa wanefili kama wale wa kabla ya gharika hivyo kwa kuona uovu wa HAM aliofanya, hasira za Nuhu zikaishia kwa CANAAN sababu ndio alikuwa uzao wa roho ya kishetani (SHAMAEL) iliosababisha hadi dhambi kurudi baada ya gharika
BAADA YA LAANA
Tunaona canaan akizaa watoto walioishi miji kama sodoma Gomorrah na Gaza zote israel ya sasa na walikuwa na falme zenye nguvu sana ila kwa kuwa laana hii ya Nuhu iliwafuata ilikuja kutimizwa na watoto wa yakobo (uzao wa SHEM) waliokuja kuwapora nchi yao ya CANAAN na wakawachinja takribani kizazi chote rejea kitabu cha joshua na kumbukumbu la torati na hata wachache waliobaki waliendelea kuteswa sana na waisrael na BIFU hili lilienda hadi kwa Yesu alipokataa kumponya mwanamke wa kanaani
Mathayo 15:22
22 Na tazama, mwanamke Mkanaani wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
23 Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.
24 Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
25 Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie.
26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa
CANAAN NA WANEFILI
Hoja ya kwamba canaan huenda alikuwa uzao wa malaika shamael ama uzao wa ajabu wa Ham na mama yake watoto wake wote walikuwa wanefili yaani majitu ya futi mpaka 28..... Kati ya watoto wote wa ukoo wa Nuhu hakuna mtu aliyezaa wanefili kuliko Canaan na makabila yote ya warefai kipindi hicho walitoka familia ya canaan wawe wayebusi wagilgal waamori wahiti wahivi n.k je huu unaweza kuwa ushahidi kuwa hakuwa mtoto wa uzao wa kawaida ndio maana akazaa wanefili watupu huku na yeye akiwa mnefili???
HAM KWENYE UISLAM
Sijapata popote kwenye Quran inapoandikwa kuhusu laana hii ya Canaan ila kwenye ukristo ma uyahudi ndipo imetajwa. Ila ukisoma hadeeth mbalimbali na machapisho ya wasomi nguli wa kiislam wa mwanzo kabisa kina Muhammad ibn-jarir al tabari pamoja na ibn khaldun wanaeleza kwamba HAM alilaaniwa sababu akiwa kwenye Safina ya Nuhu alimlala mke wake kitu kilichokatazwa hivyo alilaaniwa kwa kupewa ngozi nyeusi na ndio maana watoto wake wote wakawa weusi!!! So hawa angalau wamesema HAM alilaaniwa ila kwa kosa tofauti.... Hivyo bado hawajatupa jibu la kisa cha Nuhu na Canaan
HITIMISHO
Mada hii imetumiwa sana na wazungu wakoloni hasa karne ya 19 kuhalalisha ukoloni wa watu weusi kwa kigezo kuwa mwafrika alilaaniwa ila hoja hii naipinga sababu canaan alilaaniwa peke yake na kizazi chake kwa ukubwa kilishafutwa ila waafrika 80% walitokana na kizazi cha wale watoto 3 wa HAM ambao laana hii haikuwahusu hivyo natumia fursa kupinga propaganda hiyo rasmi na ni vizuri waafrika tupende kusoma historia yetu ili wahuni wachache wasipotoshe ukweli
Naomba kuwasilisha
Karibuni wanajukwaa wote tusaidiane kujadili kuhusu nadharia hizi,