Kwanini Canaan alilaaniwa na sio Ham?!

Yes aliyefanya kosa ni HAM ila laana ikaenda kwa CANAAN ndio nmetoa sababu kadhaa kwanni ikawa hivo soma nadharia #1 utapata mwanga
Hii pia inatoa mwanga wa pale Mungu anapokasirika na kutoa laana kwa kosa lililotendwa na kizazi cha kwanza.. Laana hiyo huenda mpaka kizazi cha tatu na cha nne! Let's try to connect the dots
 
Mkuu mitale na midimu.....hoja yako ya kuwa Nuhu hakumlaani Ham sababu ya Baraka aliyopewa na Mungu ina mashiko pia nafkiri inaweza saidia kutatua kizungumkuti hiki ILA nikiuliza mbona kuna instance nyingi ambazo Mungu anabariki na baadae analaani mfano wana wa israel walibarikiwa sana kwa maneno ya Mungu mwenyewe na baadae wakaja kulaaniwa na Mungu huyo huyo.... Hata Mungu alibariki uzao wa Abraham ila tunaona Yakobo alimlaani mtoto wake aliyelala na hawara yake na laana ilisimama !! Je kama huku kwa Yakobo mambo yalikuwa hivo je kwanini hayakuwa hivo kwa Nuhu pia as far as Genesis 9:1 is concerned
 
mkuu nakupata, ngoja tuendelee kufikili kibibiliabibilia zaidi wakati tunasubiri wasomi wa kiyahudi,kimushaf,kijubilee na kikaldayo.

Kuhusu Operation za laana za Mungu ninamaoni kadhaa.

yakijengwa katika mstari huu pia..
Kumb 30:19 ''Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;''

ni suala la UCHAGUZI, Kama Mungu anatuambia tuchague nadhani anajua huwezo huo wa kuchagua laana au baraka tunao.

Baadhi ya commentary zinasema, ahadi za Mungu ni conditional na reversible.
Ikiwa...... Nita....
pia kumbukumnu la torati 28 kuna laana na baraka pale ambazo chochote utakachochagua matokeo yake hayaepukiki.

Kwa Mungu unaweza kuchagua laana leo, kesho ukaghaili ukachagua Uzima na baraka na bado akakupokea.
Hasa sisi tunaoamini Mauti ya Yesu ambayo kwayo kwa neema tutairithi nchi suala la baraka na laana liko wazi.

Chagua Yesu -ubate baraka na ondoleo la laana ya uchaguzi uliofanya na adam na hawa na zaidi ya yote uzima wa milele na kuketi pamoja nae katika kiti cha enzi mahala ambapo shetani alitamani kukaa kwa hilana kiburi yakamkuta ya kumkuta.

Chagua Kuufuata Mwili (kubaki katika laana ya asili ya adamu ),Dunia na Shetani utakula matunda yake pia.

Hivyo nadhani Mungu sio kigeugeu bali hughaili bale tunapobadilika. Mfano mzuri Daudi mtoto wa Yese.

maoni mkuu. nadhani kuna chembechembe ndani yake zinaweza kuwa na mashiko.
 
Hapa na Mimi nilitaka kuuliza hiv hivi
Mkuu nakuelewa sana.......INA...kama kumchungulia baba Ni kulala na mkewe.....jee.....kumfunika inaweza kuwa na tafsiri gani?
Tusubiri majibu
Mkuu ambacho nataka kieleweke ni kwamba Nuhu kweli alilewa pamoja na mkewe alafu Ham kuona mama yake yupo kihasara akamuingilia hivyo hapo ndipo ALIFUNUA UCHI WA BABA YAKE hivyo wakifunika UCHI itakuwa kinyume chake labda walienda kumzuia HAM kuendelea kufanya kitendo hicho kwa Mama yao so kwakuzuia WAMEFUNIKA UCHI WA BABA YAO ndio maana wakabarikiwa

Najaribu kufikiri tu ngoja wataalam watakuja nisahihisha
 
Mwanzo 9

22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.

Inapingana na hiyo Dhana ya kumzuia asimzini
 
Mkuu ambacho nataka kieleweke ni kwamba Nuhu kweli alilewa pamoja na mkewe alafu Ham kuona mama yake yupo kihasara akamuingilia hivyo hapo ndipo ALIFUNUA UCHI WA BABA YAKE hivyo wakifunika UCHI itakuwa kinyume chake labda walienda kumzuia HAM kuendelea kufanya kitendo hicho kwa Mama yao so kwakuzuia WAMEFUNIKA UCHI WA BABA YAO ndio maana wakabarikiwa

Najaribu kufikiri tu ngoja wataalam watakuja nisahihisha
aiseee"" hawakumpiga hata makofi huyo ham ""?...jinga kabisa
 
NAOMBA NIWEKE BOLD.
Mkuu ndani ya Qur-an ipo hoja kama hio au mfano wa hio,,ingawa simulizi yako bado haijatiririka kama ilivyo ndani ya Qur-an.
Kwa kifupi yupo mtoto wa Nuhu aliekufa kwenye gharika,,wakati anahangaika(anatapatapa) ndipo Nuhu akamwambia mola wake Ee mola wangu uliniahidi kwamba wanangu hawataangamia.Mwenyezimungu akamwambi "Huyo si katika Ahali yako(watu wa nyumbani kwako),na usiuombe jambo ambalo hauna elimu nalo"...soma maneno hayo between line ili ujazie utafiti wako.
 
Nashukuru mkuu kwa Ilimu yako bila shaka yatoka kwenye Quran takatifu surat Hud..... Huyo mtoto kwenye sura hii anaitwa Kanaan pia naanza kupata picha kubwa zaidi....

Barikiwa mkuu
 
mkuu nimefuatilia kwa ufupi, nimegundua kuna nadharia rundo kuhusu hilo tukio.
na wengine wameenda mbali nadhani umekwepa kuiandika kwa sababu ya kimaadili Huyo Ham alimsodoma (homosexuality) baba yake au hiyo hoja ya castration pia. hii ni kwa mujibu wa babylonian talmud na tafsiri za baadhi ya marabbi. wameenda mbali hadi kutafsiri neno la kigiriki (kutoka kwenye septugiant ) "akamuona" wametafsiri au weka maana ya kimapenzi zaidi.

MAONI YANGU ZAIDI:
Naendelea kujikita kwenye maandiko matakatifu (bibilia ) tu kujenga baadhi ya hoja.

1:Hakuna mambo ya kusodomana, wala kuziniana kwenye hilo tukio, nadhalia hizo naona zinamadhaifu hata jitihada za kuzihusianisha na aya za mbele zisizoumana kimaana.

2: Kwa nini Ham asilaaniwe alaaniwe mwanaye?
*Kumbuka laana hiyo imetolewa na Nuhu sio Mungu. hivyo inatufikirisha zaidi.
*Mungu alikuwa amekwishambariki HAMU.
" Naye Mungu akambariki Noa na wanawe(ham,shem na yapheti), akawaambia: “Zaeni, muwe wengi, mjaze dunia." Mwanzo 9:1
hapo ni wazi Mungu kambariki HAMU hivyo laana ya nuhu inaweza isifanye kazi, na wenda imeandikwa kuwa inaenda kwa kaanani kwa sababu ndio mzao wake ambae alikuwa hana hizo baraka zilizotolewa na Mungu.
Maoni haya ambayo nayaunga mkono yanaumana na Magombo ya kale yaliyochimbuliwa (dead sea scrolls 4Q252) wakizungumzia tukio hilo.

3:Maoni ya mwanahistoria wa kiyahudi ambaye anatambulika kwa wananzuoni Josephus anasema nuhu hakumlaani HAM kwa sababu ya ukaribu wao hivyo akaamua badala yake amlaani mtoto wa mtoto wake. (maoni haya yanaweza kuleta mantiki ukijumuisha na yale ya mwanzo9:1).

TUKIRUDI KWENYE BIBILIA
kwa sababu ya ukinzani wa nadhalia nyiiingi ambazo nimegundua kuna maelfu ya watu, wasomi wameamua kupiga kambi mahala ambapo bibilia imenyamaza na wao kupajaza na kupashindilia na nadhalia lukuki inanifanya niamini facts ni zile zilizoandikwa katika bibilia.

1:Nuhu alilewa.
2:Kwa Mujibu wa Bibilia Kulewa ni Dhambi (walevi hawatairithi nchi, isipokuwa wametubu. 1Cor6:9-18)
3:Mtoto wake Ham alimchungulia aliuona UCHI wa baba yake.
4:Nuhu sio Mungu, akaamua kumlaani mtoto wa Ham Kaanani kwa sababu zake aliporudiwa na fahamu.
5:Ukiangalia ndugu zake hamu walikuja kumfunika uchi wa baba yao bila kuuangalia, kwa mtiririko wa matukio utaona hakuna element yoyote ya ngono katika tukio hilo lililohusisha wanaume wanne.
5:Hakuna Ushahidi kuwa Laana hiyo ya kifamilia inauhusiano na Uweusi wetu katika bibilia.

magap katkati ya hizo biblical facts yanaweza kujazwa na nadharia yoyote ile mkuu.

nyongeza ya maoni, katikati ya nadharia zote nashikilia hizo biblical facts kama msingi mkuu.

barikiwa mkuu.
Chief ktk hoya No.2 hapo wakati Nuhu anamlaani Kanaani, kanaani alikua ameshazaliwa au alimlaani kupitia mgongo wa Ham?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom